Huyu kakwapua simu kutoka kwenye daladala leo asubuhi posta mpya akawa anakimbia .wananchi wenye hasira walimtoa baru kakamatiwa karibu na ofisi za BMTL na kupewa kichapo cha maana. Polisi walitokea baada ya kama dk 45 baada ya tukio.

Pascal,
Posta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Sasa Bro Michu! Huyo kibaka kafaaa au? Mbona watu wanashangaa huku damu zikivuja kichwani mwa kibaka..Bongo! simu tu, huondoa uhai wa binadamu!

    ReplyDelete
  2. acha wakomeshwe wamezidi kutuweka roho juujuu, ndiyo mana wengine wanachomwa moto mpaka wanateketea kabisa, lakini cha ajabu hawaachi. Labda sasa wakikamatwa wakatwe mikono yote.

    ReplyDelete
  3. Bwana Pascal sasa mlimwacha mzima ?
    Mngemaliza kabla ya polisi hawajatokea

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli kero ya vipaka inasikitisha sana,kuona wanawaliza watu.

    Lakini pia kitendo cha wanachi kujichulia hatua mikoni sio cha kuunga mkono.Maana sasa hivi kuna mtindo wa baadhi ya vibaka inaweza kuwa usiku wakikutana na wewe wanakugeuzia kibao na kuanza kukupiga wakidai wewe ndio kibaka ili wakuibie.Kwa stahili hii inakuwa usalama wa watu upo hatari

    Hata lugha aliyotumia kaka Michu ina kaushabiki fulani ka kuunga mkono kitendo cha hao "WAVUNJA SHERIA" ambao michu na vyombo vya habari vinawatakatifuza kwa kuwaita "WENYE HASIRA"

    Yaani wananchi wanakuwa wenye hasira kwenye simu ya mshindi kutoka china ya tshs elfu 15 wakati ahatuoni wananchi wenye hasira kwa MAJIZI ya mabilioni kwenye mikataba inayosababisha huyo dogo hadi akwapue simu.

    Wananchi wenye hasira mpeleke hasara kwa MAFISADI pia ndio nitaona mnamchungu kweli.

    ReplyDelete
  5. OOh NOO..It's not fair kuchukua sheria mikononi.kweli ametenda kosa adhabu alopewa ni kubwa sana.In real fact kosa kubwa limefanywa na wale waliompiga (sina hakika kama yuko hai looks kama amekufa).
    Jamani watanzania mbona tunakuwa watu wa roho mbaya kweli simu moja utafananisha na value ya roho ya mtu.Put in your shoes labda huyo ni ndugu yako au mtoto wako ungependa afanyiwe hivyo?
    Serekali ichukue hatua kukomesha vitendo hivyo vya uuwaji.

    ReplyDelete
  6. Jamani this is Bad!!! Japokuwa wizi ni kitu kibaya kinachokatazwa na dini zote na sheria za nchi pia, lakini kutoa roho ya mtu au kumpa mtu kichapo cha kufisha, mi naona sio sawa na ni dhambi mbele za Mungu na ni kosa chini ya sheria za nchi vile vile.

    Jamani taratibu zifuatwe katika kushughulikia watuhimiwa, kama vile kuwakamata kiubinadamu bila ya kichapo wala kuwakwida, kuwafikisha polisi na hatimae mahakamani, ili mahakama, chombo pekee chenye mamlaka ya kusulubu watuhumiwa, kipate kuamua juu ya hatma ya mtuhumiwa husika.

    Pia Serikali ijaribu ku-address chanzo cha watu kuiba, kama vile ukosefu wa ajira, mifumo mibovu ya elimu na umasikini.

    Inaniuma sana, pengine aliiba au hakuiba, kabambikiziwa tu, au hata kama aliiba hiyo simu yenyewe hata hai-cost laki, ndo imgharimu maisha yake?

    ReplyDelete
  7. huyu ni mvulana au msichana

    ReplyDelete
  8. Huyu ni demu? Aisee bongo noma yaani SIMU tuu unataka kupoteza maisha yako?

    ReplyDelete
  9. jamani,toba yarabi,huyu si mwanamke,au macho yangu?

    ReplyDelete
  10. Inawezekanaje binadamu kuuliwa au kuumizwa kiasi hicho kwa ajili ya simu??? Hiyo simu ilikuwa na gharama gani ikilinganishwa na maisha au afya ya huyo kijana?? Inabidi nijiulize kama kweli hao waliompiga kama ni binadamu au wanyama pori:-( Pascal hicho kitu kimekufurahisha???

    ReplyDelete
  11. Michuzi tunakuheshimu sana bro lakini kitendo chako cha kuandika hiyo habari kiushabiki na kuonyesha kama ni habari nzuri na haki sio haki kabisa na ninakulaumu sana na nilitegemea kwa sababu blog yako inasomwa na watu wengi ungeitumia kuonyesha na kukemea kitendo kama hiki kwa nguvu zote,huo ni unyama wa hali ya juu na punishment does not fit the crime!

    ReplyDelete
  12. Unajuwa, Mimi kila siku nakuwa nauliza kama sisi watanzania tuna ubinadabu pia tunaelewa na tunataka kuweka sheria mbele yetu. nimekuja kuelewa sisi watanzania, We are uncivilized society. Kama watu wanaweza kufanya mambo kama haya. Lazima hili swali tuweke mbele yetu kama tunataka kuleta maandeleo katika nchi yetu. haiwezekani watu wakamfanyia mtu mambo kama haya.

    Yangu machache,

    Jimmy K

    ReplyDelete
  13. guys stop being defensive
    mi nasema hata ningekuwepo ningesupport apigwe. Like 2 weeks ago, nimechoka nimetoka kazini, then went to have these professional exams. nimetoka saa1 na nusub usiku, very tired, congested feeling like fainting. najidrive kurudi home, nikaona kama ac inaniumiza kichwa tu, nikashuisha kioo half way. Jamani mume wangu akanipigia simu pale salender just after kituo in bagamoyo rd going to mwenge. Ile napokea tu weka sikioni na niko ktk mwendo from nowhere jamaa kaichukua N93 yangu. I felt so angry nilitamani niwe na bastola ningemlipua... na pale kusimama huwezi utagongwa. ila nashukuru mungu hakuniumiza na nimenunua nyingine ila guys msiombe!!

    ReplyDelete
  14. Huyo leo kaanza na simu, kesho atenda kwenye magari ya watu then atahamia majumbani. Hivi ni mara ngapi tumesikia majambazi yanaua watu halafu wanaondoka na laki moja au mali ya elfu hamsini? Kama wao wanaweza kuuwa mtu halafu wampore laki moja basi na wananchi wawatendee hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  15. Mnalalamika nini? Hiyo ndio bongo yenu, wezi wa mamilioni wanapeta, wenye njaa(kwasabbu ya wezi wengi wa mamilioni)wanuwawa!

    ReplyDelete
  16. KWA NINI NA MAFISADI NAO TUSIWACHUKULIE HATUA? AU KWA SABABU WAO WANAHUSIKA NA "WHITE COLLAR" CRIME, AU KWA SABABU WIZI WAO NI SOPHISTICATED. KAMA TUNAUA VIBAKA NA MAFISADI NAO TUWARUSHIE MAWE KWANZA TUNAWAJUA.

    ReplyDelete
  17. Dhambi ni dhambi. Hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Aliyeiba ana dhambi na aliyempiga huyo mwizi ana dhambi vilevile. Sema serikali na wananchi wanatakiwa kukemea watu kuchukua sheria mkononi.

    ReplyDelete
  18. ndugu zangu hapa tatizo sio kwamba watanzania tuna roho mbaya,tatizo ni national trauma ambayo kama nchi tu suffer.hii trauma unatokana na ukweli kwamba watanzania kwa namna moja au nyingine tumeathirika na wezi/majambazi na hii ni kwa aidha kuvunjiwa,kuibiwa,kujeruhiwa na hata kuuawa ndugu zetu,rafiki,majirani etc.hivyo tukimdaka kibaka inaamsha ile deep seated anger kwamba 'ah ndo hawa hawa'and we go for the jugular,na hapo reasoning inawekwa pembeni ni unyama unyama tu,actually hii ndio asili ya neno 'wenye hasira kali'.

    ReplyDelete
  19. MICHUZI, TAFADHALI USIWAITE WAUWAJI - WANANCHI WENYE HASIRA, SI UNAONA WAMEUA HAWA!
    MICHUZI VIPI? BINAADAMU AMEKUFA.

    WAUWAJI NA WEZI NANI WANA MAKOSA ZAIDI? KAMA UNAMUAMINI MWENYEZI MUNGU JIBU NI WAUWAJI.

    MUUWAJI NI MUUWAJI TU. HAKUNA MJADALA KIJANA KAIBA PENGINE ANA NJAA. NDIO MNAMUUWA?.

    SHAME ON YOU MURDERERS, SHAME ON THE GOVERMENT THAT OVERLOOK THIS BARBARIC ACTIVITIES. SAME ON THAT TYPE OF SOCIETY.

    HIKI NI KITENDO CHA UNYAMA, UOGA NA AIBU. SASA MBONA MMESIMAMA HAMCHUKUI VISU MKAMLA TUKAJUA MOJA - WALA WATU, WANAUWA KATIKATI YA MJI, MCHANA AND THEY GET AWAY WITH IT!.

    MNAPENDA KUSEMA "NCHI ZINGINE WANAPIGANA NA KUUWANA", MBONA NYIE MNAUWANA KILA SIKU - WAUWAJI WAKUBWA.
    UNCIVILIZED!

    ReplyDelete
  20. ale wapi??

    Ney-bham

    ReplyDelete
  21. Nyie watu vipi? Mnamlaumu Michuzi aliyewaonyesha hali halisi ya bongo, mnawalaumu watu wanaopiga vibaka....sijui nyie vipi!!!! wa kulaumiwa ni serikali. Kama polisi wanafika baada ya dakika 45????. Wacha watu wafanye wanavyotaka. Na pia huyo kibaka kama kaipasi hiyo phone kwa mwingine basi akienda mahakamani kesi itaishia hewani na simu haitarudi. Wewe unategemea watu wafanyeje? Waache wawabonde vibaka mpaka wajue kesho wakiiba cha moto wanakiona. Na pia serikali iweke sheria kali za vibaka hawa. Sio kuwa mtu anaiba phone anaachiwa baada ya week. Kosa ni kosa. Ukiiba simu au ukivunja nyumba adhabu iwe sawa. Hawa vibaka ndio hao hao. Wanaenda pugu week mbili wamerudi mitaani. What do you expect? Unamuona alikua anakimbilia polisi kwa vile anajua huko kuna heri....waizi wa nchi za nje wakiiba wanakimbilia mitaani na hawataki kabisa kushikwa na polisi...lakini nchi yetu safe haven ya vibaka ni polisi

    ReplyDelete
  22. sheria za kiarabu alitakiwa akatwe mkona huyo.sasa lipi bora ,kaachwa kama somo hapo?na wakome mi walishaniliza simu hao.

    ReplyDelete
  23. TENA ACHENI KUJITETEA NA KUTETEA WANYAMA, HAPANA SIO WANYAMA BALI WABAYA KULIKO WANYAMA. WANYAMA WANAUA ILI WAPATE CHAKULA HAWA WANAUA KWA KURIDHISHA ROHO ZAO.
    TUJIFUNZE KUFUATA SHERIA HATA KAMA HAIKIDHI HAJA AU INACHELEWA. VINGINEVYO WALE WOTE WALIOHUSIKA WANASTAHILI LAANA ZANGU NA LAANA ZA WOTE WANAOLAANI IKIWA NI PAMOJA NA MWENYEZI MUNGU.
    PIA NINGEPENDA KUILANI SEREKALI KWA KUTOCHUKUA HATUA YOYOTE WAKATI HAKI ZA BINAADAMU ZINAPOKIUKWA. NADHANI HII NI KWA SABABU VICTIMS NA MURDERERS NI MASIKINI. YOU KNOW WHAT DON'T BOTHER, IT DOES NOT AFFECT US AND IT MAKE THEM HAPPY - YOU SEE
    THE GOVERMENT THAT CAN'T PROTECT HER PEOPLE AGAINST SUCH INHUMAIN ACTS, IT IS FAILING TO PERFORM ONE OF ITS FUNDAMENTAL DUTIES I.E. TO PROVIDE SECURITY.

    ReplyDelete
  24. michuzi, mwalimu wako wa media ethics ni nani? inabidi abadilishwe nawe urudi darasani.

    ReplyDelete
  25. huyu kaiba kijisimu cha mkononi, mnapiga mpaka kafa! na mnachekelea eti nyie wananchi wenye hasira! mbona hao wanaomaliza mamilioni serikalini hamuwagusi,huku mkiwajua kwa majina na hata kunywa na kula nao kwa vicheko? jamaa mmoja kaua tena kwa risasi mbele ya watu waliojazana ndani ya daladala...mlimpiga? au uoga uliwaingia mkafyata mikia!!acheni sheria ichukue mkondo wake.

    ReplyDelete
  26. watu wote wanaotetea vibaka, ujue hayajawakuta, hakika vibaka wanarudisha sana nyuma maendeleo ya watu, mtu kahangaika weee kutafuta hako kasimu, hujui mtu kasafa vipi na maisha yenyewe yalivyo magumu, halafu mtu anakakwapua kirahisi namna hiyo. ngoja mtu uwe na kashilingi 1000 tu mfukoni, halafu kibaka kakapitia kwenye basi halafu konda anadai nauli, ndio mtu atajua vibaka wabaya au vipi!!!! mimi siwafagiliii kabisa wameshaniliza sana. sina hata hamu nao viumbe hao!!!!! NS.

    ReplyDelete
  27. EMMA vipi???...I FULLY SUPPORT annon wa 06:05, 06:08 na 07:04 ni jugular au TOFA tu!...ANNON WA 07:04 said it ALL!!! SOMENI MUMUELEWE...tuko na madonge nao ile mbaya hawa!!! ALAFU NYIE MNAOSEMA TUWALIME WALE WANAOIBA MABILIONI NA WANAOSAINI MIKATABA...are you serious??...if only we could set our hands on them in this ,anner!!!...we would have skinned them ALIVE!!!...PLZ REFER TO ANNON WA FRI 19th 07:04 BIG UP BUDDY!!!...

    ReplyDelete
  28. Uwizi na uchumi wa nchi unaendana hand by hand. Tuwalaumu viogozi wetu na sio vibaka, wapeni kazi na elimu, uwizi utapungua.

    ReplyDelete
  29. NILIPIGWA KABALI YA MBAO NA KUPORWA KITUO CHA BASI KWA MANYANYA SAA 2 USIKU.

    NYARAKA ZANGU MUHIMU ZILIPOTEA,

    PESA ZANGU ZILIPOTEA (HATA NAULI HAWAKUNIACHIA)

    SIMU YANGU ILIPOTEA

    NILITUMIA GHARAMA KWA KUJITIBU MADHARA NILIYOYAPATA BAADA YA KABALI

    KWA UFUPI NILIPATA USUMBUFU MKUBWA.

    NILIJAWA NA HASIRA KALI SANA.

    JE, HIVI NIKIMWONA KIBAKA NEXT DAY NITAFANYA NINI? (NITACHEKA, NITAMHURUMIA AU...) NISAIDIENI KWA HILI.

    ReplyDelete
  30. aka mwenzangu unamkata mikono tote miwili, tuone ataiba na nini. Tena hapo Manyanya Kinondoni ni pabaya sana, wamejaa tele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...