wafanyabiashara soko kuu la kariakoo wakiwa waemduwaa ndani ya soko hilo baada ya askari polisi na mgambo kuzuia watu kuingia humo sokoni jana na leo katika hatua ya kuondoa wachuuzi nje ya jengo hili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tanzania ni Nchi huru lakini viongozi wake ni Wababe sana Hivi kabla ya kufunga soko 1)Je mmewatafutia MAENEO ya kufanyia kazi hao wananchi Wanaishi kwa kutegemea kipato chao hapo SOKONI KARIAKOO 2)Kuwafukuza wananchi bila ya kuwapa maeneo ya kazi hamuoni ni hatua ya kuongea uksefu wa KAZI na ongezeko la uhalifu (Vibaka na Majambazi)Naiomba Serikali Iwajali Wanchi wapiga kura kwanza Jenga SOKO jipya kwanza Ndio ufunge la zamani.HUU SI UUNGWANA KUWANYIMA WANANCHI RIZIKI ZAO Ahsante Mgosi wa Kaya U. K

    ReplyDelete
  2. Huenda sikumwelewa vizuri JK katika kampeni zake za kuomba urais.Hivi alisema anataka kutengeneza ajira za watu milion 2 au kubomoa ajira za watu million 2!?
    Hawa jamaa zetu waliondolewa hapo kkoo watakwnda wapi kama hakuna maeneo waliyoandaliwa?Serikali ingekuwa inaanda maeneo then kama watu wasipohama ndio unawatimuwa lakin sio kuwakurupua tu watu wamelalamika sana kupata hasara ya bidhaa zao kuharibiwa,..hela zenyewe za mikopo basi mawazo matupu na matatizo unawaingizia raia wema..halafu nasikia wanataka kwenda kwenye magereji bubu!!
    Mie sikatai mipango hii mizuri lakin hawa watu wanaotimuliwa wakale wapi sasa kama sio kuongeza vibaka mtaani?!

    ReplyDelete
  3. nakubaliana na nyie hapo juu kuhusu watu kukosa ajira lakini wengi wao wamekimbia vijiji kuja kujazana mjini tunahitaji wakulima vijijini wote tukiuza nguo nani ata produce chakula.kwahiyo it's a very good idea,warudi shamba wakalime alokwambia hao wanaouza hapo nje sio vibaka ni nani?wanajitia kuuza vitu mkononi jaribu kupita kioo chini anakugeukia kukuibia.

    ReplyDelete
  4. Masoko ya Kariakoo yako mengi ama ni hili moja tu?? Maana hapo pameandikwa "Shirika la Masoko ya Kariakoo"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...