richard akipozi na miss tz uk 2008
richard akisalimiana na balozi mwanaidi maajar london
richard na wadau wa london
london ilikuwa ni mikonozzz mtindo mmoja
richard, pinto, hafsa na banana walipowasili london
richard akisalimiana na mchezaji wa zamani wa yanga athumani china london

mapicha haya ni baadhi tu kati ya mengi na habari zake utazozikuta katika tovuti binafsi ya mshindi wa big brother II richard iendayo kwa address ya http://www.richardbba2winner.com/

nimeyaweka hapa makusudi ili kwanza kutoa hongera kwa richard kwa kuwa na tovuti inayovutia na ambayo ni mfano wa kuigwa sio tu kwa vile ina jipya karibu kila siku bali pia imetengenezwa kwa weledi unaotakiwa.

hii ni changamoto kubwa anayotoa richard katika dunia ya sasa kwani globu na tovuti nyingi zinadoda aidha kwa kukosa cha kuandika na kubandika ama ufinyu wa ubunifu katika kuendeleza libeneke kama hili. rai ni kwamba globu ama tovuti ni maktaba ya kisasa ambayo unashea na wenzio bila kuwa na wasiwasi wa picha kupotea ama kuharibika tofauti na kutegemea albamu ya mapicha inayododa kabatini baada ya muda kuopita.

natoa wito, hasa kwa wadau wenye majina katika jamii kuunda kitu kama hiki kwani dunia ya sasa ni mawasiliano na mawasiliano yenyewe yamerahisishwa sana kiasi hata inakuwa raha. inasikitisha kuona nyota wetu karibu wote (wanamuziki, wanamichezo, wanasiasa, wataalamu wa fani mbalimbali n.k) wa bongo hawana tovuti, ingawa wanafanya mengi katika jamii. natumai changamoto hii ya richard itaawaamsha ili mambo yawe mswano.

wataohitaji msaada hata wa mawazo wa namna ya kuanzisha na kuendesha globu ama tovuti tunaweza kuwasiliana ili tusaidiane kupitia issamichuzi@gmail. com




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2008

    Balozi wetu alikuwa na wakati wa kuonana na huyu jamaa enh? sijui aliweka appoitment muda gani na kama ilikuwa ni siku ile ambayo ndiyo iliyowekwa kumuona mheshimiwa. i don't think so.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2008

    What are all these beutiful Tanzanian malaikas doing in the UK We jamaa Richard nakuonea wivu kwa hiyo mikonos Mtoto aliyeshinda ni kisura lakini too much bones

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2008

    Kama huyo ndiye Miss UK 2008 basi mwaka huu huko hakuna mtu.
    bora angepewa huyo dada wa pili kutoka kushoto mwenye black picha ya tatu kutoka chini hata kama hakushiriki.
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2008

    lisa, get in touch with me at jstella36@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2008

    mnasura nzuri sana wadada mmependeza.
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2008

    Comment yangu sio ya urembo, bali napenda kumpongeza Richard kwa kununua kiwanja kule Lushoto {Nundu ya Ngombe} Hata mimi nikienda huko nitajaribu kunua kasehemu kwa ajili ya nyumba ya mapumziko

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2008

    Mademu wa kibongo UK wazuri na wanajua kuvaa kuliko wabongo wa US

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2008

    mdau hapo juu,tatizo wanawake wa US kuvaa nusu ndo wanaona wamevaa na wanaume kuvaa manguo makubwa ndo wanaona wako juu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2008

    kumbe china yuko london, duh uk kweli sehemu ya wazee wa zamani,ametulia sana mzee yuko kimya au ashajipiga kisonji?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2008

    CHINA ANGEKUWA KAMA KINA KANU AU MICHAEL ESSIENEH ALIPATA MKATABA NA TIMU YA DARAJA LA TATU LAKINI AKAONDOKA. ANGEWEKA MIZIZI KWA NCHI YETU. LEO KARUDI KULE KULE LAKINI KWA STYLE YA BOX.
    PINTO UMEKUWA LUNDENGA WA UK?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2008

    pinto amekuwa lundenga wa UK? KWELLI CHINA ALIPOTEZA NAFASI YAKE AMGEKUWA ESSIENE AU KANU WA TANZANIA KAMA ANGETULIZA AKILI. ALIPATA MKATABA NA WALSALL.AKAUVURUGA KWENDA ARABUNI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...