afisa habari wa tff florian kaijage akifanya matangazo
" halloooo madega eeee.....tunawasubiri jamani.... mnakuja???" anasema katibu mkuu wa tff frederick mwakalebela wakati muda unasogea na yanga hawaonekani


simba ndiyo washindi watatu wa kombe la kagame cup baada ya watani wao wa jadi kuingia mitini. hivi ninavyosema simba wameshakaguliwa peke yao, na wimbo wa taifa umepigwa kuashiria kwamba mchezo unaanza.



naam florian kaijage anatangaza kwamba zinasubiriwa dakika 15 na kama yanga hawatafika basi simba ndio wameula kwenye sahani ya fedha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2008

    Hawa watu wa TFF wamenenepa hivyo kuna ulaji huko, ebu muangalie FLORIAN NA MWAKALEBELA!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2008

    Mwakalebela mtoto wa juzi cheki alivyozeeka kwanini lakini wewe???? hebu tafuta ufumbuzi wa afya yako

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2008

    Huu upuzi wa timu kutoufika uwanjani au kugomea mechi, utaisha lini? Inabidi TFF iwawajibishe wahusika, kama adhabu kali zingetolewa sidhani kama upuuzi kama huu ungekuwepo. Makosa yenu hayo ya kuletana ufaza kwenye mambo muhimu, matokeo yake kila siku tunakuwa wasindikizaji. halafu lawama nyingi kwa makocha, kumbe matatizo yapo kwenye viongozi. Tuangalie TFF itatoa adhabu gani kwa Yanga. Ila ni kitendo cha aibu, ukizingatia mashindano yameshirikisha timu za kigeni, je watajifunza nini kutoka kwetu? Ndio maana timu za kibongo, refa akiwapa penati timu pinzani hata kama ilikua sio penati ya halali, hukata tamaa na kulalama saana. Utakuta timu nyingine ikitokea makosa ya refa, huendelea na mchezo na baadae huibuka na ushindi. Inabidi TFF iwe inayapiga vita mambo kama haya, mie nilifikiri yatakua yameisha toka enzi zile za Twalib Hilal kunawa mpira Simba kugomea penati, hadi Yanga kuruka ukuta. Kumbe mpaka leo Millenium bado sie tupo kule kule? Tunategema kweli kuwakilisha World Cup siku za karibuni kwa tabia kama hii ya moja ya Timu no.1 Tz kuleta hulka potovu za soka kama hizi? Kazi bado mbichi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...