simba ndiyo washindi watatu wa kombe la kagame cup baada ya watani wao wa jadi kuingia mitini. hivi ninavyosema simba wameshakaguliwa peke yao, na wimbo wa taifa umepigwa kuashiria kwamba mchezo unaanza.
naam florian kaijage anatangaza kwamba zinasubiriwa dakika 15 na kama yanga hawatafika basi simba ndio wameula kwenye sahani ya fedha
Hawa watu wa TFF wamenenepa hivyo kuna ulaji huko, ebu muangalie FLORIAN NA MWAKALEBELA!!!!!!!
ReplyDeleteMwakalebela mtoto wa juzi cheki alivyozeeka kwanini lakini wewe???? hebu tafuta ufumbuzi wa afya yako
ReplyDeleteHuu upuzi wa timu kutoufika uwanjani au kugomea mechi, utaisha lini? Inabidi TFF iwawajibishe wahusika, kama adhabu kali zingetolewa sidhani kama upuuzi kama huu ungekuwepo. Makosa yenu hayo ya kuletana ufaza kwenye mambo muhimu, matokeo yake kila siku tunakuwa wasindikizaji. halafu lawama nyingi kwa makocha, kumbe matatizo yapo kwenye viongozi. Tuangalie TFF itatoa adhabu gani kwa Yanga. Ila ni kitendo cha aibu, ukizingatia mashindano yameshirikisha timu za kigeni, je watajifunza nini kutoka kwetu? Ndio maana timu za kibongo, refa akiwapa penati timu pinzani hata kama ilikua sio penati ya halali, hukata tamaa na kulalama saana. Utakuta timu nyingine ikitokea makosa ya refa, huendelea na mchezo na baadae huibuka na ushindi. Inabidi TFF iwe inayapiga vita mambo kama haya, mie nilifikiri yatakua yameisha toka enzi zile za Twalib Hilal kunawa mpira Simba kugomea penati, hadi Yanga kuruka ukuta. Kumbe mpaka leo Millenium bado sie tupo kule kule? Tunategema kweli kuwakilisha World Cup siku za karibuni kwa tabia kama hii ya moja ya Timu no.1 Tz kuleta hulka potovu za soka kama hizi? Kazi bado mbichi!
ReplyDelete