Michu,
Natumaini uko gado kama kawaida yako na unaendeleza libeneke.
Niko Juba - Sudan, napiga mzigo kwa siku mbili tatu, katika kutafuta mkate wa kila siku. Ile kutinga hotelini, Juba Grand Hotel, nikaiona hii ndinga.
Kwa kuwa mimi binafsi nahusudu sana mandinga, hii ikanichanganya sana, afu sio siri, back home, sija itia machoni kabisa! Afu sikujua kama Toyota nao wana mandinga kama haya. Ukiiangalia kwa fasta inaonekana kama Hammer.
Sasa naomba wadau wanisaidie kunifahamisha hii in Toyota ya aina gani?
Asante
Jay.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Toyota fj cruiser

    ReplyDelete
  2. oyaa mdau jay hiyo ni TOYOTA FJ huku mitaa ya dubai ni zakumwaga.

    ReplyDelete
  3. Jay, hiyo ni Toyota FJ Cruiser. Unaweza kutafuta maelezo yake kwenye intaneti.

    Toyota FJ Cruiser zilitengenezwa chache tu kwa ajili ya soko la Amerika ya Kaskazini lakini kutokana na mahitaji mengi zimekuwa nyingi zaidi.

    Toyota FJ Cruiser ni gari ya kifahari, kama zilivyo Hammer na nyingine.

    ReplyDelete
  4. Ebwana hiyo huku kwetu Sydney twaita Toyota mkojo shehee.

    ReplyDelete
  5. Hello

    Bwana mkubwa hiyo ni FJ CRUISER zina kama miaka 3 au 4 ,I am not sure lakini nadhani hi ni model mpya za zile ngiri mnazikumbuka jamani?

    ReplyDelete
  6. this is FJ CRUISER.
    In the future please check official web sites. In this case try:www.toyota.com and http://www.toyota.com/fjcruiser/index.html

    ReplyDelete
  7. KWA MACHO YANGU NADHANI HIYO NI JOHN DEERE AU MASSEY FERGUSON mwenye macho .....

    fundi kishushu

    ReplyDelete
  8. hiyo ni FJ cruiser 2008 model

    ReplyDelete
  9. Hiyo gari dar ipo na mimi mwenyewe naidrive ni ya rangi ya blue. Toyota Hammer. Ninatafuta mteja No. yangu ni: 0784 390 310

    ReplyDelete
  10. Kaka hiyo ni toyota ule muundoulikuwa ukijulikana hapa bongo kama "DUBE" angalia picha kwenye link (http://en.wikipedia.org/wiki/Image:TBJ40.JPG) Kwa kuwa ndiyo aliyokuwa akiiendesha Dumisani Dube, raia wa afrika kusini na kuligonga gari la marehemu Sokoine pale morogoro miaka ya 80........... nilipofuatilia kwenye net nimekuta hii-Toyota has recently introduced the FJ Cruiser, a modern SUV styled after the original FJ40. The FJ Cruiser (FJC) went on sale in the spring of 2006.(Source:http://en.wikipedia.org/wiki/Toyota_FJ40)

    ReplyDelete
  11. You better GO and ask Simba Sports Club fanatic members I think they will be in the position of clearing your doubt as you can see that the MV is registered with their club abbreviation i.e. SSC 5108, what they can do is just to clearly peruse the registration card (original) where they can find the particulars of the MV.

    ReplyDelete
  12. Hii ni ushuzi tu, eti kuna jamaa hapo juu anasema gari la kifahari, wewe magari ya kifahari ndo yanauzwa US$23,000 si hata Mzee Makamba angenunua.

    ReplyDelete
  13. Hahah! Asante kwa wote mliomjibu lakini mimi nataka kumshauri huyo mdau siku nyingine usipate shida na kukosa usingizi sogelea gari kwa karibu soma maandishi yote na ukishindwa uliza hapo hapo ulipo kwani kuuliza si ujinga. Asante kwa picha

    ReplyDelete
  14. Ni nyumbu special edition hiyo. Zinatengenezwa nyingi mno Kibaha for export only. Ingia site hii nyumbuspecialeditionforexportnakudanganya.com

    Ha ha haaaaaa

    ReplyDelete
  15. sasa wewe ukiwa unaishangaa hiyo gari ya kawaida tu ukija viwanja vya watu si unaweza ukapata matatizo wewe kwa kushangaa, hiyo toyota iko mitaani siku nyingi tu ni gari ya kawaida tu wala hakuna anayo ishangaa kwani kuna magari mengi tu ambayo unaweza ukayashangaa kabala ya hilo, any way kama ulivyo kwisha sema kuwa uko sudani basi sikushangai kwa kushangaa kwako pole mwanawani
    kazi unayo, uwe makini lakini kwani siku hizi watu huwa wanashangaa kibitozi kwani ukiwa unageuza shingo kila saa unaweza ukaishiwa kuwekewa hogo, kama bado unampago wa kuendelea kutembea hapa duniani

    Mbega

    ReplyDelete
  16. wabongo bwana nyodo sana sijui tu watoto au vipi....Yaani mtu akishajua kitu basi inakuwa tabu....yeyey kauliza na ndio mara yake ya kwanza kuiona sasa nyie kama mmeshaiona si mumjibu yaishe...Kwani shida ipo wapi mpaka museme huko aliko sijui nini....that is very low.....kama wewe ulishaliona na hutaki kumjulisha cool let other people do it for you .........Inakatisha tamaa sana na inaonyesha jinsi tulivyoimmature....tembelea blog zingine za nchi za Africa ...people are so willing to help one another....We need to grow up and/or we need to change our attitudes

    ReplyDelete
  17. ISE MDAU UMENIFURAHISHA SANA KWAKUWATOLEA UVIVU HAWA WANAO ONGEA MAMBO YAKUKATISHA TAMAA ILI TUENDELEE INAPASWA KUSAIDIANA KIMAWAZO LAKINI KUULIZA INAKUWA NONGWA WATU WENGINE WANAJIFANYA NDIO WANAJUA SAAAAANA HATA UJUE SANA VIPI LAKINI LAZIMA KUNAWANAOJUA ZAIDI YAKO NDIO MAANA WENZETU WA NCHI NYINGINE WAKIWA NJE YA NCHI ZAO WANASHIRIKIANA KULIKO SISI SISI TUNABAKI NYUMA KWASABABU YA MDOMO MDOMO WETU NA FITNA TENA MNAOONGOZA KWAKUSEMA OVYO WENGI NI WALIO NJE KUTOKANA NA KAULI TUNAZOZISOMA LAKINI UKWELI SISI TULIOBONGO NDIO TUNAONA WALIO NJEE KAMA WAMECHELEWA KIMAISHA SIO KWAMBA HATUJUI LINALOENDELEA HUKO
    MDAU

    ReplyDelete
  18. Ni kweli wa-Tanzania tuna matatizo hasa wengi waliojifanya kwenda nje ndio wanaongoza kusema ovyo, mimi nahisi ni limbukeni na hasa hawa wanaoenda sasa wanajifanya kujuwa kila kitu, ukilinganisha na wale waliokuwa wanaenda zamani wengi wao walikuwa wanaenda kusoma, wasomi, si hawa wa sasa wanaoenda kwa green card, wengine kwa kusota na kudanganya bolozi kuwa wanaenda kusoma kumbe wanaenda kufuta mavi wazee wa kizungu basi wanaona kama ndo wao wanajuwa kila kitu, kumbe maisha yao hayana hata tofauti na maisha ya Tanzania na pengine wako watu Tanzania wana maisha mazuri na hata elimu nzuri kuliko wao, jamani tuache hii tabia ya kujibishana ovyo tustarabike na tuwe kitu kimja tusaidiane, na kama mnataka kujifunzi tembeleeni blogs za ki-Uganda na ki-Kenya mtaoni wanavyoongea na vitu wanavyoandika ni vya msingi na kusaidiana ndo maana unaona kun a idadi kubwa ya waganda na wakenya wanoenda nje kuha ngaika a maisha kwa vile huwa wanapeana maelekezo namna ya kwenda mahala na kupata kazi hata hiyo green card Kenya kila mwaka huondoka watu zaidi ya 5000, wakati Tanzania siyo zaidi ya 200 kila mwaka, kwa vile watu hawaam,bizani kama kuna kitu kama hicho, wanafanya siri na uchoyo wa kusaidiana

    ReplyDelete
  19. Mdau nakushauri ukipata kamuda tembelea na Japan,utaona gari ambazo haujawahi hata kuzifikiria kama zingekuwepo.
    Asante

    ReplyDelete
  20. Vipi WADAU kuhusu jibu alilotoa Bw. KICHWABUTA MWENDANTWALA hapo juu ???? Je linakidhi haja ????

    ReplyDelete
  21. hapa bongo lipo na nimeliona. lina rangi ya blue na mashavu meupe

    ReplyDelete
  22. Wabongo wengine majishebedua. Kuweni wastaarabu. Mjibu mlichoulizwa. Kwenda huko imekuwa tabu. For your information kwa nyie mnajishebedua,kila mtu hapa dunianiani lazima kuna jambo asilofahamu kiufasaha na lazima alishangae. Huwezijua kila kitu bwana.

    ReplyDelete
  23. BILA SHAKA HIYO ITAKUWA NI VALMET.

    ReplyDelete
  24. hiyo ni Honda Civic ;)


    J/k ni FJC kama wanavyosema wazushi hapa,

    Boost3D.

    ReplyDelete
  25. ni kweli wabongo tumatatizo, mfanonilishashuhudia wabongo ulaya wanatembea kwenye theluji halafu mwenzao katereza kadondoka wakaanza kumcheka na kumkebehi jinsi asivyojua kutembea kwenye theluji, nyuma yao kaja mzungu mwenyeji kamsaidia kamwinua, yaani noma wazungu wote wanawaangalia wale wenzao walipata aibu sana. Wabongo tuache kujifanya tunajua tusaidiana, hamna mtu aliyezaliwa anajua kila kitu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...