
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani wa Tarime uliofanyika juzi.
Mgombea ubunge wa chama hicho, Charles Mwera, alitangazwa kumrithi Chacha Wangwe aliyekufa ajalini Julai mwaka huu, baada ya kushinda kwa kupata kura 34,545 huku mgombea wa CCM Christopher Kangoye akipata kura 28,996.
Mgombea wa NCCR-Mageuzi, Haruni Marwa alipata kura 949 wakati mgombea wa DP Benson Makanya alipata kura 305.
Kwa ushindi huo wa ubunge na udiwani Chadema inaendelea kuongoza halmashauri ya wilaya ya Tarime huku CCM ikiendelea kubaki chama cha upinzani katika halmashauri hiyo.
Kwa habari zaidi
bofya hapa
Michuzi,
ReplyDeleteUshindi huu sio kwa Tarime au CHADEMA pekee, bali kwa AMANI, UMOJA, HAKI NA UDUGU kwa WATANZANIA WOTE dhidi ya mbegu ya UKABILA ambayo ilikuwa inaanza kupandwa
Huu ni uthibitisho kuwa ikiwa watu watavinjari kweli kweli na kukataa vitisho vya kushushiwa virungu vya FFU na kucharazwa mapanga, basi CCM inaweza kun'goka. Hakuna njia nyengine.
ReplyDelete