Mbunge mpya wa Tarime, Charles Mwera (kushoto) na Diwani mpya wa Kata ya Tarime Mjini, John Heche, wakiongoza maandamano ya kuwapongeza katika mitaa ya mji huo, baada ya kutangazwa washindi jana


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani wa Tarime uliofanyika juzi.


Mgombea ubunge wa chama hicho, Charles Mwera, alitangazwa kumrithi Chacha Wangwe aliyekufa ajalini Julai mwaka huu, baada ya kushinda kwa kupata kura 34,545 huku mgombea wa CCM Christopher Kangoye akipata kura 28,996.


Mgombea wa NCCR-Mageuzi, Haruni Marwa alipata kura 949 wakati mgombea wa DP Benson Makanya alipata kura 305.


Kwa ushindi huo wa ubunge na udiwani Chadema inaendelea kuongoza halmashauri ya wilaya ya Tarime huku CCM ikiendelea kubaki chama cha upinzani katika halmashauri hiyo.
Kwa habari zaidi
bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Ushindi huu sio kwa Tarime au CHADEMA pekee, bali kwa AMANI, UMOJA, HAKI NA UDUGU kwa WATANZANIA WOTE dhidi ya mbegu ya UKABILA ambayo ilikuwa inaanza kupandwa

    ReplyDelete
  2. Huu ni uthibitisho kuwa ikiwa watu watavinjari kweli kweli na kukataa vitisho vya kushushiwa virungu vya FFU na kucharazwa mapanga, basi CCM inaweza kun'goka. Hakuna njia nyengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...