Je ni mambo gani ya kuzingatiwa hasa katika upigaji picha wa kwenye hizi concert zetu,vipi kwa hizo kadhaa ambazo nilizipiga wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Zain pale viwanja vya Karimjee,Hilo ni wasanii wa kundi la UMOJA kutoka afrika kusini.
Ahmad Michuzi Jnr.
-----------------------------------
Ahmad!
kwanza nikupongeze kwa bidii yako katika kuendeleza libeneke. najisikia praudi sana kuonan unavyokata mbuga kule michuzijr.blogspot.com kwa picha na habari motomtot kila siku. endelea tu, faida utaiona baadaye. kwa kweli nakufagilia sana sana kwa hilo

kujibu swali lako noamba niseme ni ngumu, ikizingatiwa kwamba kila taswira ina ladha yake kwa mtazamo wa mtu na mtu. nasisitiza tena na tena kwamba taswira si hesabu unayoweza kugawa na kuzidisha na kupata jibu ambalo halibadiliki. picha ni kama uzuri wa mrembo ambao unaonekana na mpendaji. wewe utamuona ana chongo mwenzio atasema hilo ni kengeza tu.

tukija kwenye kama hizo za juu ambazo ukiondoa kasoro ndogondogo (maiki zimekula uhondo wake, monita ama spika zinaonekana haraka kabla ya watu kutokana na ukubwa wake, zote ni za mbali, ungetupatia za karibu tuone urembo wa watu na mavazi) kwa maoni yangu nadhani inategemea unazipiga kwa ajili ya msomaji ama muangaliaji yupi.

kama ni kwa ajili ya magazeti taswira zimekidhi haja moja tu; muonekano wa unadhifu na ustadi jukwaani wa wachezaji na ukubwa wa jukwaa pamoja na makorokoro yake. kama ingekuwa ni taswira ya sanaa basi ya karibu (close-up) ya mmoa ama wawili ama hata watatu kuonesha nyuso, mavazi na vibuyu ingekuwa bomba.

ya juu ni nzuri inagwa sio sana kwani siku ingine jaribu kupiga bila flashi. hapo unatakiwa uwe na taimingi kwani ukipiga wakati wanatikisika picha itacheza. ukiipatia hali (atmosphere) ya hiyo sehemu ingekupa bonge la muonekano.

kumbuka hayo ni maoni yangu na tasfiri, sio ndio jawabu la mwisho la swali lako ambalo jibu utalipata kama utajiuliza ni nani ataziona hizi taswira na angependa kuona kitu gani.

-michuzi

-------------------------------------------

KUTOKANA NA USHAURI WA WADAU WENGI, HASA WAPENZI WA TASWIRA NIMEAMUA LEO KUANZISHA RASMI GLOBU MAALUMU ITAYOENDELEZA LIBENEKE LA TASWIRAZZZ AMBALO NAONA LINASHIKA HATAMU KWA KASI KWANI HAPA NILIPO NINAZO KIBIDONI TASWIRA KIBAO AMBAZO NIKIBANIKA ZOTE ITAKUWA BALAA.

GLOBU HIYO INAITWA

libenekelataswira.blogsot.com

NA TAYARI IMESHAANZA KAZI IKO HEWANI TOKA LEO JIONI. PAMOJA NA KUPOKEA TASWIRA TOKA KWA WADAU PIA KUTAKUWA NA DARASA LA MARA KWA MARA JUU YA HILI NA ILE KATIKA FANI HII ADHIMU. HUKO PIA UTAPATA NAFASI YA KUULIZA MASWALI, KUTOA MAONI NA HATA KUKOSOA.

HIVYO KARIBUNI libenekelataswira.blogspot.com TUENDELEZE LIBENEKE

-MICHUZI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Unajua kaka michuzi wewe umejaaliwa sana na mwenyezi mungu kwa kupendwa na watu wengi kwa ajili ya moyo wako mzuri.nasema hivi kwa sababu huko tayari kukosolewa na kupongezwa na hilo jambo muhimu sana kwa mwanadamu.
    Siku nilipo tuma comment ya ushauri wa kufunguliwa blog nyingine ya taswiraz peke yake siku hiona comment yangu nikajua nimekukera kwa kusema vile.sasa leo naona umeweza kupima na kugundua kweli inahitajika blog hio tofauti.nashukuru sana.na huwe unaitangaza kila wiki hili kuwakumbusha watu wengine wapya kwamba kuna glob ya taswirazz.
    Hongera sana kwa kazi nzuri na kutjali wadau wako.
    Yaani mimi kama mdau nina furaha kuona unasikiliza ushauri wetu .
    Mungu akujalia na moyo mzuri zaidi na neema zako utalipwa.
    Mdau mzawa.

    ReplyDelete
  2. Umenifurahisha sana kwa kuanzisha lebeneke la taswiri,mark my words this is going to be very popular and congratulations
    Tuwekee direct link maana hapa kwetu bado tuna matatizo to log on
    Jee ulipokea picha yangu niliyoleta ama umeitia kwenye pakacha la takataka
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. ...mitchu, hii imekaa vizuri, balozi wa nanihii.. ombi maalum: japo kuwe na utaratibu wa 'kulink' globu ya taswira na neshno letu la jamii... kwa mfano kupitia taswira ya mwezi, itokee na ituzwe huku 'neshno'...yaani vijimambo kama taswirazz ndo vitachachandua zaidi huku globuni ya jamii. pia nna wasiwasi kuwa kuna wengine wasingelitaka kunasa kwenye 'moramu' la kiufundi la nyinyi mnaougua kagonjwa ka taswirazz. Yaani tungependa tuone vile ambavyo vimemeng'enyuliwa tayari, libeneke jingine libaki hukohuko hospitali, wenye maradhi walifate huko- ni mtazamo tu.
    UZENGERE

    ReplyDelete
  4. Mbona haifanyi kazi hiyo libeneke la taswirazz....mzee michuzi?

    Mdau...

    ReplyDelete
  5. Michuzi

    It is a wonderful present to photography addicts. Safi sana na tunashukuru sana, next move ni uanzishe shule au courses za photography.

    Tunashukuru wa zawadi hii maridhawa.

    Regards

    ReplyDelete
  6. Swadakta... Nadhani hilo litakuwa sio tu darasa kwa sisi wapenda taswirazzzz na wakwapuajizzzz bali ni albamu ya dunia kama sio funika bovu! May God bless y'all mtakaoshirika kwa namna moja ama nyingine. Ubarikiwe Balozi.

    ReplyDelete
  7. Ufuuu, asavali, maana hizo taswira zilikua zinakula nafasi tu, bora uwape blog yao wenye hoby yao na sisi tuhabarishe zaidi, hasa hasa habari za huko nyumbani Tz.


    Mdau ughaibuni.

    ReplyDelete
  8. Mdau hapo juu asema link haifanyi kazi na Michuzi kama nilivyomoumba aweke link mpaka sasa hajatimiza ombi hilo.Basi wenye matatizo nawajulisha waende google kuna link safi, na hakika blog hiyo mpya yaleta mnoga
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  9. asante kwa blog ya kileo nafurahia sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...