
kujibu swali lako noamba niseme ni ngumu, ikizingatiwa kwamba kila taswira ina ladha yake kwa mtazamo wa mtu na mtu. nasisitiza tena na tena kwamba taswira si hesabu unayoweza kugawa na kuzidisha na kupata jibu ambalo halibadiliki. picha ni kama uzuri wa mrembo ambao unaonekana na mpendaji. wewe utamuona ana chongo mwenzio atasema hilo ni kengeza tu.
tukija kwenye kama hizo za juu ambazo ukiondoa kasoro ndogondogo (maiki zimekula uhondo wake, monita ama spika zinaonekana haraka kabla ya watu kutokana na ukubwa wake, zote ni za mbali, ungetupatia za karibu tuone urembo wa watu na mavazi) kwa maoni yangu nadhani inategemea unazipiga kwa ajili ya msomaji ama muangaliaji yupi.
kama ni kwa ajili ya magazeti taswira zimekidhi haja moja tu; muonekano wa unadhifu na ustadi jukwaani wa wachezaji na ukubwa wa jukwaa pamoja na makorokoro yake. kama ingekuwa ni taswira ya sanaa basi ya karibu (close-up) ya mmoa ama wawili ama hata watatu kuonesha nyuso, mavazi na vibuyu ingekuwa bomba.
ya juu ni nzuri inagwa sio sana kwani siku ingine jaribu kupiga bila flashi. hapo unatakiwa uwe na taimingi kwani ukipiga wakati wanatikisika picha itacheza. ukiipatia hali (atmosphere) ya hiyo sehemu ingekupa bonge la muonekano.
kumbuka hayo ni maoni yangu na tasfiri, sio ndio jawabu la mwisho la swali lako ambalo jibu utalipata kama utajiuliza ni nani ataziona hizi taswira na angependa kuona kitu gani.
-michuzi
-------------------------------------------
KUTOKANA NA USHAURI WA WADAU WENGI, HASA WAPENZI WA TASWIRA NIMEAMUA LEO KUANZISHA RASMI GLOBU MAALUMU ITAYOENDELEZA LIBENEKE LA TASWIRAZZZ AMBALO NAONA LINASHIKA HATAMU KWA KASI KWANI HAPA NILIPO NINAZO KIBIDONI TASWIRA KIBAO AMBAZO NIKIBANIKA ZOTE ITAKUWA BALAA.
GLOBU HIYO INAITWA
NA TAYARI IMESHAANZA KAZI IKO HEWANI TOKA LEO JIONI. PAMOJA NA KUPOKEA TASWIRA TOKA KWA WADAU PIA KUTAKUWA NA DARASA LA MARA KWA MARA JUU YA HILI NA ILE KATIKA FANI HII ADHIMU. HUKO PIA UTAPATA NAFASI YA KUULIZA MASWALI, KUTOA MAONI NA HATA KUKOSOA.
HIVYO KARIBUNI libenekelataswira.blogspot.com TUENDELEZE LIBENEKE
-MICHUZI
Unajua kaka michuzi wewe umejaaliwa sana na mwenyezi mungu kwa kupendwa na watu wengi kwa ajili ya moyo wako mzuri.nasema hivi kwa sababu huko tayari kukosolewa na kupongezwa na hilo jambo muhimu sana kwa mwanadamu.
ReplyDeleteSiku nilipo tuma comment ya ushauri wa kufunguliwa blog nyingine ya taswiraz peke yake siku hiona comment yangu nikajua nimekukera kwa kusema vile.sasa leo naona umeweza kupima na kugundua kweli inahitajika blog hio tofauti.nashukuru sana.na huwe unaitangaza kila wiki hili kuwakumbusha watu wengine wapya kwamba kuna glob ya taswirazz.
Hongera sana kwa kazi nzuri na kutjali wadau wako.
Yaani mimi kama mdau nina furaha kuona unasikiliza ushauri wetu .
Mungu akujalia na moyo mzuri zaidi na neema zako utalipwa.
Mdau mzawa.
Umenifurahisha sana kwa kuanzisha lebeneke la taswiri,mark my words this is going to be very popular and congratulations
ReplyDeleteTuwekee direct link maana hapa kwetu bado tuna matatizo to log on
Jee ulipokea picha yangu niliyoleta ama umeitia kwenye pakacha la takataka
Wakatabahu
...mitchu, hii imekaa vizuri, balozi wa nanihii.. ombi maalum: japo kuwe na utaratibu wa 'kulink' globu ya taswira na neshno letu la jamii... kwa mfano kupitia taswira ya mwezi, itokee na ituzwe huku 'neshno'...yaani vijimambo kama taswirazz ndo vitachachandua zaidi huku globuni ya jamii. pia nna wasiwasi kuwa kuna wengine wasingelitaka kunasa kwenye 'moramu' la kiufundi la nyinyi mnaougua kagonjwa ka taswirazz. Yaani tungependa tuone vile ambavyo vimemeng'enyuliwa tayari, libeneke jingine libaki hukohuko hospitali, wenye maradhi walifate huko- ni mtazamo tu.
ReplyDeleteUZENGERE
Mbona haifanyi kazi hiyo libeneke la taswirazz....mzee michuzi?
ReplyDeleteMdau...
Michuzi
ReplyDeleteIt is a wonderful present to photography addicts. Safi sana na tunashukuru sana, next move ni uanzishe shule au courses za photography.
Tunashukuru wa zawadi hii maridhawa.
Regards
Swadakta... Nadhani hilo litakuwa sio tu darasa kwa sisi wapenda taswirazzzz na wakwapuajizzzz bali ni albamu ya dunia kama sio funika bovu! May God bless y'all mtakaoshirika kwa namna moja ama nyingine. Ubarikiwe Balozi.
ReplyDeleteUfuuu, asavali, maana hizo taswira zilikua zinakula nafasi tu, bora uwape blog yao wenye hoby yao na sisi tuhabarishe zaidi, hasa hasa habari za huko nyumbani Tz.
ReplyDeleteMdau ughaibuni.
Mdau hapo juu asema link haifanyi kazi na Michuzi kama nilivyomoumba aweke link mpaka sasa hajatimiza ombi hilo.Basi wenye matatizo nawajulisha waende google kuna link safi, na hakika blog hiyo mpya yaleta mnoga
ReplyDeleteWakatabahu
asante kwa blog ya kileo nafurahia sana
ReplyDelete