meneja wa kilaji cha redds george kavishe akieleza jambo wakati wa mkutano wa kuwatambulisha rasmi mamodo wa east africa model search hoteli ya southern sun (zamani holiday inn) dar leo. redds ndio wadhamini wakuu wa mchuano huo wenye mamodo toka kenya, uganda, rwanda, burundi na wenyeji bongo. wengine toka shoto ni judy felician ambaye ni mratibu mkuu, bona kaluwa ambaye ni mkurugenzi mkuu wa michuano hiyo na celine njunju afisa habari wa zain ambaye kampuni yake ni wadhamini.
mamodo wa ist afrika mashariki wakionesha miondoko yao leo
mkufunzi mkuu wa mamodo wa east africa model search, supa modo mkongwe fideline ilanga (kati) akila pozi la nguvu na mamodo wake hao ambao watachuana novemba 29, 2008 hapa dar kupata washindi wanne wataopata mikataba ya kufanyia umodo ughaibuni



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Jonie Mashaka huko wapi? msaada tutani hapo. changamkia vimwana hivyo, lakini vina chuna ile mbaya ukiwa mpare basi kula kona kwa maana hivo vimodo vina gharama sana

    ReplyDelete
  2. Kumbe Fideline bado yupo kwenye mikiki ya modelling?

    ReplyDelete
  3. Super-model my butt.

    ReplyDelete
  4. Huuuuuuuuuuuuuuuuu!!!

    Natafuta mchumba, Nyie mamodo kuna atakaye nimid? Mimi ni mkulima A.KA Lorkisalie. Mashamba eka 3000 na ngombe yapata 2000 na mbuzi na kandoo idadi sijui hata. Mwaka jana walifikia 10,000 na bado sijawauza wa krsmasi. Modos channgamkieni hiyo dili. Najua wengi hamjaolewa msinizingue akaa?!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Ati hii ni boarding skool ya wapi?Hi inafanana na Iringa Gals skool
    Mimi jameni mkulima mtanichanganya sana. Kwani niuze mbuzi, kondoo wangapi ili niweze kwenda kutizama.?
    Hebu niende kufunga mbuzi wangu

    asanteni jameni

    Ni mimi mkulima

    ReplyDelete
  6. jamani namhurumia huyo dada aliyevaa natural stockings. Kwa November Dar atakuwa naungua ile mbaya!!!!

    ReplyDelete
  7. Tanzania tutatoka kweli?
    siku hizi umodo na ulimbwende unapagaisha kuliko hata shule!!

    Laiti tunge mzawadia msichana wa kwanza kila mwaka katika masomo ya sayansi Escudo mpya badala ya ma-Miss na kumpokea kwa shangwe JKN airport kila Mtanzania anayetelemka na PhD badala ya anayetoka kutuahibisha Big Braza Afrika!

    Ndivyo ilivyo dunia, yaani mimi nakula machimbuzi MIAKA MINGI toka ujana wangu wote mpaka utu uzima hakuna anayetaka kujua ninachokifanya;

    Vibinti vinatoka na vitopu na kajinzi kenye mpindo chini na baada ya WIKI MBILI TU, Wooote tunaacha kazi zote tunatafuta 50,000 - 100,000 hata kwa mkopo tuingie tuone wanavyotembea kwa staili ya miguu kuingiliana na mavazi hadimu tusiyoyaona tena barabarani.

    CCM kwani hatuwezi kuanzisha UWT- mbadala,yaani Umoja wa Wanaume wa Tanzania?

    ReplyDelete
  8. we anonymous wa kwanza ushindwe na ulegee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...