meneja wa kilaji cha redds george kavishe akieleza jambo wakati wa mkutano wa kuwatambulisha rasmi mamodo wa east africa model search hoteli ya southern sun (zamani holiday inn) dar leo. redds ndio wadhamini wakuu wa mchuano huo wenye mamodo toka kenya, uganda, rwanda, burundi na wenyeji bongo. wengine toka shoto ni judy felician ambaye ni mratibu mkuu, bona kaluwa ambaye ni mkurugenzi mkuu wa michuano hiyo na celine njunju afisa habari wa zain ambaye kampuni yake ni wadhamini.
mamodo wa ist afrika mashariki wakionesha miondoko yao leo
mkufunzi mkuu wa mamodo wa east africa model search, supa modo mkongwe fideline ilanga (kati) akila pozi la nguvu na mamodo wake hao ambao watachuana novemba 29, 2008 hapa dar kupata washindi wanne wataopata mikataba ya kufanyia umodo ughaibuni

Jonie Mashaka huko wapi? msaada tutani hapo. changamkia vimwana hivyo, lakini vina chuna ile mbaya ukiwa mpare basi kula kona kwa maana hivo vimodo vina gharama sana
ReplyDeleteKumbe Fideline bado yupo kwenye mikiki ya modelling?
ReplyDeleteSuper-model my butt.
ReplyDeleteHuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!
ReplyDeleteNatafuta mchumba, Nyie mamodo kuna atakaye nimid? Mimi ni mkulima A.KA Lorkisalie. Mashamba eka 3000 na ngombe yapata 2000 na mbuzi na kandoo idadi sijui hata. Mwaka jana walifikia 10,000 na bado sijawauza wa krsmasi. Modos channgamkieni hiyo dili. Najua wengi hamjaolewa msinizingue akaa?!!!!!!!!!!!!!!
Ati hii ni boarding skool ya wapi?Hi inafanana na Iringa Gals skool
ReplyDeleteMimi jameni mkulima mtanichanganya sana. Kwani niuze mbuzi, kondoo wangapi ili niweze kwenda kutizama.?
Hebu niende kufunga mbuzi wangu
asanteni jameni
Ni mimi mkulima
jamani namhurumia huyo dada aliyevaa natural stockings. Kwa November Dar atakuwa naungua ile mbaya!!!!
ReplyDeleteTanzania tutatoka kweli?
ReplyDeletesiku hizi umodo na ulimbwende unapagaisha kuliko hata shule!!
Laiti tunge mzawadia msichana wa kwanza kila mwaka katika masomo ya sayansi Escudo mpya badala ya ma-Miss na kumpokea kwa shangwe JKN airport kila Mtanzania anayetelemka na PhD badala ya anayetoka kutuahibisha Big Braza Afrika!
Ndivyo ilivyo dunia, yaani mimi nakula machimbuzi MIAKA MINGI toka ujana wangu wote mpaka utu uzima hakuna anayetaka kujua ninachokifanya;
Vibinti vinatoka na vitopu na kajinzi kenye mpindo chini na baada ya WIKI MBILI TU, Wooote tunaacha kazi zote tunatafuta 50,000 - 100,000 hata kwa mkopo tuingie tuone wanavyotembea kwa staili ya miguu kuingiliana na mavazi hadimu tusiyoyaona tena barabarani.
CCM kwani hatuwezi kuanzisha UWT- mbadala,yaani Umoja wa Wanaume wa Tanzania?
we anonymous wa kwanza ushindwe na ulegee.
ReplyDelete