Mheshimiwa,
Nilikuwa napenda kuuliza swali tu, kama mtu ameshang'ata tunda halafu ukapewa sehemu iliyobakia utakula au utanunua/chuma au kwenda tafuta la kwako? Miye nimepata kigugumizi.
Nile nimepewa nile,
Nile wakijiji nile,
Nile alivyokula yule,
Nile tunda lile lile?
Nilile au nisile,
Nilile au nilale,
Nisilile au nile,
Nile tunda lile lile?
Nile kama vile yule,
Nile nami vilevile,
Nile hapa au pale,
Nile tunda lile lile?
Nile bila ya simile,
Nile lile kama Chale,
Nilile hapa si pale,
Nile tunda lile lile?
Nilile mwana wa yule,
Nile walokula wale,
Nile hilo pole pole,
Nile tunda lile lile?
Nile au sote tule,
Nile au tukalile,
Nile au nisilile,
Nile tunda lile lile?
Nile jingine nilile
Nile hilo siyo lile,
Nile la kwangu nilile,
Nile tunda lile lile?

Nitembelee:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Utakulaje tunda analokula mwenzio? Kama umelipenda, katafuta la kwako kama hilo au lifananlolo na hilo pia nawe ujidai.

    ReplyDelete
  2. unaweza kulila ila inategemea na mlaji alilikataje wakati wa kulila,(kwa kutumia kisu,mdomo,mikono au kulidondosha chini na kupasukaau nk)

    ReplyDelete
  3. Nimejaribu kuingia site ya mwanakijiji.com lakini files hazifunguki,hebu jaribu na wewe labda kwangu kuna miwaya!give us the feed back MM!

    ReplyDelete
  4. WATU WENGINE WAKISHAKUA HAWANA KAZI TU BASI HUBUNI VIJIMAMBO VYAO ILI WATUUMIZE KICHA SISI WABEBA MABOX...SASA MIMI NI JIBU LANGU UKISUSA WENZIO WALA....

    ReplyDelete
  5. Mjomba kula tu but anza kulipima kama zima or tunda limeshaoza. Kama ni zima basiwaweza kula.
    Mjomba pia kabla hujala naomba uchunguze kama mwenyewe kaliacha or kaweka kiporo, kwani mla tunda ndie hujuwa ladha yake.
    Pia jitahidi mjomba usile kama vile yeye alikuwa anakula, lile kwambinu mpya za kisasa, tena lipambe lisikupe kinyaa na aliyelitupa alionee hamu na asilipate mjomba.

    Lakini mjomba wakati ukila tunda lako usikwazwe na usemi wa malenga "GANDA LA MUA LA JANA CHUNGU KAONA KIVUNO"!!!

    nI AYO TU mJOMBA.

    g7
    TZ

    ReplyDelete
  6. Kula tunda acha maulizo
    Ukila kwa hisia utapata wazo
    Ule usile ni tunda liliwalo
    Kijijini mnamegeana kweli hamnazo

    ReplyDelete
  7. Mla kala sasa, wa jana kala nini?
    Kula bila visa, kama bado watamani
    Yaache tisa, la kumi ulithamini.
    Mla kala sasa, wa jana kala nini.

    Mchwa kupukusa, au funza ndani
    Mwenzio kutomasa, au kuuma pembeni
    Usije kulisusa, moyoni walitamani
    Mla kala sasa, wa jana kala nini?

    Si papai hasa, au ndizi za shambani
    Tusome kurasa, vitabu madhebahini
    Tunda limekunasa, kama Adam peponi
    Mla kala sasa, wa jana kala nini


    Tunda ni asusa, ya maisha duniani
    Sio chenza hasa, au dodo mtini
    Tunda lina visa, nalo linakutamani
    Huwezi kulisusa, moyo unalitamani

    Tunda acha visa, mwenzio kawa laini
    Tunapenda kuku-asa, ame 'fall' jamani
    Mla kala leo, wa jana kala nini?

    ReplyDelete
  8. Fafanua Tunda maanake ni nini. Wazee wa fasihi tunaona kunautata hapo.

    ReplyDelete
  9. Muulize kocha wa dunia mtaalam wa ma-tunda,

    Alikula la Tam - Tam kisha akaliacha tunda,

    Akala la double M, akalitelekeza tunda,

    Ndipo akashiriki na mzee wa farasi katika Double extra, kwa mwezi mmoja wakalikacha tunda,

    Akalivamia achimenengule, mbele ya Mjeshi-Mneki,akalitema tunda,

    Sasa analiosha na kulitomasa la Bwagamoyo sound,anasema tamu sukari, gusa unase tunda,

    Mwanakijiji, kuna yale yanayoachwa kwa uozo,mengine kwa imani hayaliwi matunda,

    kuna yanayotemwa kwa tamaa, baada kwa kuona kama lingine linameremeta tunda,


    kuna yanayotafunwa na wengi bila kujua,lakini yapo pia yanayowatafuna wanadamu matunda,



    kula la kwako unalolijua, ukitaka lingine muulize kocha wa dunia mtaalam wa matunda.






















    yako

    ReplyDelete
  10. kama tunda ni la kifisadi bora usilile kwani uiklila utakua fisadi amelila salva ikulu sasa tunashindwa mfahamu.Salva tuliye mfahamu sasa anapoteza sula simlaumu kweni kwenye mduara wa mafisadi nawe utakua fisadi usilile usilile usilile tunda hilo ni SUMU.UKILILA UTAKUA FISADI
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    Advocate Jasha.

    ReplyDelete
  11. Ulile nani kakupa?

    Ulile kijijini kwa kukopa?,
    Kuna bango tunda limetupwa?
    Ulile nani kaukaribisha?

    Ulile umelitolea jasho?
    Ulile kwa ubave na vitisho
    au ni mabavu na mipasho?
    Ulile nani kakupa?

    Nile tunda lile lile?
    Eti nami kama yule,
    Nawe ule vilevile,
    Hustahili hapa wal kule,
    Ulile nani kakupa?

    Vyakukuliwa na masharti
    iwe vya chini au vya kati
    Vilipendwa au vina chati
    Ulilie nani kakupa?

    Eti ule kama chapati,
    Au za Azam biskuti,
    Ule pole au harakati,
    Ulile nani kakupa?

    Tunda hupandwa shambani
    Mwenye shamba si hayawani
    Kafukuza ndege na nyani
    Ulile kakaupa nani?

    Mwenye tunda kalienzi
    Kwa ushujaa na mapenzi
    Kwa rehema za mwenyezi
    Ulile nani kakupa?

    Ewe tunda kuwa makini
    mafisadi wapo kazini
    Walile kwa kisirani
    Ufisadi uko kichwani

    Sheria za chetu kijiji
    Tunda la kujifariji
    Posa adhima twataraji
    Mzee Ali na Miraji
    kwa heshima na adabu

    Tunda si tunda doa
    wala si tunda poa
    Tunda tunu limetulia
    Acha kulipapia

    ReplyDelete
  12. Mwanakijiji sahau
    Tunda sikama pilau
    Kwamba akila Bahau
    Halifai kurudia

    Tunda halina makombo
    Jilie usende kombo
    Usilete zako nyimbo
    Tunda umetunukiwa

    Hakuna cha peke yako
    Vitamu ule na wenzako
    Ukijilia kivyako
    Utakufa peke yako

    Tamati natia nanga
    Usiseme nakusimanga
    Tunda usije linanga
    Kula ushatunukiwa

    ReplyDelete
  13. Wajameni kwa kweli mmenifurahisha na hizo ngano zenu! Ndugu yangu Mwanakijiji mimi binafsi huwa sipendi kula kitu kilichoshikwa na mikono ya watu wengine!huwa naona kinyaa! halafu huwezi juwa mtu aliyekula au kumega alinawa mikono, alivaa gloves au meno yake hayakuoza?

    ReplyDelete
  14. hahahahahahahaaaa teh teh teh uwiiiii jamani mmeshindikana wana-blogu hii,,,hahahahaaa
    kila mtu na tafsiri yake

    ReplyDelete
  15. Hili tunda, ni tunda gani?
    Linatoka Mpanda, Au Usambaani?
    La mtini tunda, au tunda akilini?
    Tunda ni kinda, moyo majaribuni?

    Si yako halali, nawe umeibaini
    Hujapata iqbali, kulitia mdomoni
    Cha mwenzio ghali, sumu kijiini
    Tunda ni kinda, moyo majaribuni

    Jiziwiye kwa hali, upate makini
    La mwenzio muhali, hili ulibaini
    Lile wala hili, usilete tafrani
    Tunda ni ghali, moyo majaribuni

    Sheria za mwili, twahara moyoni
    tunda batili, utaingia motoni
    Ule vya halali, vibudu usitamani
    Tunda ni ghali, moyo majaribuni

    Virusi vya mwili, tena asilani
    Sikubali wawili, kumega kilaini
    Unaijua hali, vumilia jamani
    Tunda ni ghali, moyo majaribuni

    Subiri lako, la mwenza si lako
    Huko yatokako, na lako liko
    Fanya msako, usijali masumbuko
    Tunda ni ghali, salama kusubiri

    ReplyDelete
  16. Jamaa ushapata majibu, au hujaridhika?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...