Mheshimiwa,
Nilikuwa napenda kuuliza swali tu, kama mtu ameshang'ata tunda halafu ukapewa sehemu iliyobakia utakula au utanunua/chuma au kwenda tafuta la kwako? Miye nimepata kigugumizi.
Nilikuwa napenda kuuliza swali tu, kama mtu ameshang'ata tunda halafu ukapewa sehemu iliyobakia utakula au utanunua/chuma au kwenda tafuta la kwako? Miye nimepata kigugumizi.
Nile nimepewa nile,
Nile wakijiji nile,
Nile alivyokula yule,
Nile tunda lile lile?
Nilile au nisile,
Nilile au nilale,
Nisilile au nile,
Nile tunda lile lile?
Nile kama vile yule,
Nile nami vilevile,
Nile hapa au pale,
Nile tunda lile lile?
Nile bila ya simile,
Nile lile kama Chale,
Nilile hapa si pale,
Nile tunda lile lile?
Nilile mwana wa yule,
Nile walokula wale,
Nile hilo pole pole,
Nile tunda lile lile?
Nile au sote tule,
Nile au tukalile,
Nile au nisilile,
Nile tunda lile lile?
Nile jingine nilile
Nile hilo siyo lile,
Nile la kwangu nilile,
Nile tunda lile lile?
Nitembelee:
Utakulaje tunda analokula mwenzio? Kama umelipenda, katafuta la kwako kama hilo au lifananlolo na hilo pia nawe ujidai.
ReplyDeleteunaweza kulila ila inategemea na mlaji alilikataje wakati wa kulila,(kwa kutumia kisu,mdomo,mikono au kulidondosha chini na kupasukaau nk)
ReplyDeleteNimejaribu kuingia site ya mwanakijiji.com lakini files hazifunguki,hebu jaribu na wewe labda kwangu kuna miwaya!give us the feed back MM!
ReplyDeleteWATU WENGINE WAKISHAKUA HAWANA KAZI TU BASI HUBUNI VIJIMAMBO VYAO ILI WATUUMIZE KICHA SISI WABEBA MABOX...SASA MIMI NI JIBU LANGU UKISUSA WENZIO WALA....
ReplyDeleteMjomba kula tu but anza kulipima kama zima or tunda limeshaoza. Kama ni zima basiwaweza kula.
ReplyDeleteMjomba pia kabla hujala naomba uchunguze kama mwenyewe kaliacha or kaweka kiporo, kwani mla tunda ndie hujuwa ladha yake.
Pia jitahidi mjomba usile kama vile yeye alikuwa anakula, lile kwambinu mpya za kisasa, tena lipambe lisikupe kinyaa na aliyelitupa alionee hamu na asilipate mjomba.
Lakini mjomba wakati ukila tunda lako usikwazwe na usemi wa malenga "GANDA LA MUA LA JANA CHUNGU KAONA KIVUNO"!!!
nI AYO TU mJOMBA.
g7
TZ
Kula tunda acha maulizo
ReplyDeleteUkila kwa hisia utapata wazo
Ule usile ni tunda liliwalo
Kijijini mnamegeana kweli hamnazo
Mla kala sasa, wa jana kala nini?
ReplyDeleteKula bila visa, kama bado watamani
Yaache tisa, la kumi ulithamini.
Mla kala sasa, wa jana kala nini.
Mchwa kupukusa, au funza ndani
Mwenzio kutomasa, au kuuma pembeni
Usije kulisusa, moyoni walitamani
Mla kala sasa, wa jana kala nini?
Si papai hasa, au ndizi za shambani
Tusome kurasa, vitabu madhebahini
Tunda limekunasa, kama Adam peponi
Mla kala sasa, wa jana kala nini
Tunda ni asusa, ya maisha duniani
Sio chenza hasa, au dodo mtini
Tunda lina visa, nalo linakutamani
Huwezi kulisusa, moyo unalitamani
Tunda acha visa, mwenzio kawa laini
Tunapenda kuku-asa, ame 'fall' jamani
Mla kala leo, wa jana kala nini?
Fafanua Tunda maanake ni nini. Wazee wa fasihi tunaona kunautata hapo.
ReplyDeleteMuulize kocha wa dunia mtaalam wa ma-tunda,
ReplyDeleteAlikula la Tam - Tam kisha akaliacha tunda,
Akala la double M, akalitelekeza tunda,
Ndipo akashiriki na mzee wa farasi katika Double extra, kwa mwezi mmoja wakalikacha tunda,
Akalivamia achimenengule, mbele ya Mjeshi-Mneki,akalitema tunda,
Sasa analiosha na kulitomasa la Bwagamoyo sound,anasema tamu sukari, gusa unase tunda,
Mwanakijiji, kuna yale yanayoachwa kwa uozo,mengine kwa imani hayaliwi matunda,
kuna yanayotemwa kwa tamaa, baada kwa kuona kama lingine linameremeta tunda,
kuna yanayotafunwa na wengi bila kujua,lakini yapo pia yanayowatafuna wanadamu matunda,
kula la kwako unalolijua, ukitaka lingine muulize kocha wa dunia mtaalam wa matunda.
yako
kama tunda ni la kifisadi bora usilile kwani uiklila utakua fisadi amelila salva ikulu sasa tunashindwa mfahamu.Salva tuliye mfahamu sasa anapoteza sula simlaumu kweni kwenye mduara wa mafisadi nawe utakua fisadi usilile usilile usilile tunda hilo ni SUMU.UKILILA UTAKUA FISADI
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA.
Advocate Jasha.
Ulile nani kakupa?
ReplyDeleteUlile kijijini kwa kukopa?,
Kuna bango tunda limetupwa?
Ulile nani kaukaribisha?
Ulile umelitolea jasho?
Ulile kwa ubave na vitisho
au ni mabavu na mipasho?
Ulile nani kakupa?
Nile tunda lile lile?
Eti nami kama yule,
Nawe ule vilevile,
Hustahili hapa wal kule,
Ulile nani kakupa?
Vyakukuliwa na masharti
iwe vya chini au vya kati
Vilipendwa au vina chati
Ulilie nani kakupa?
Eti ule kama chapati,
Au za Azam biskuti,
Ule pole au harakati,
Ulile nani kakupa?
Tunda hupandwa shambani
Mwenye shamba si hayawani
Kafukuza ndege na nyani
Ulile kakaupa nani?
Mwenye tunda kalienzi
Kwa ushujaa na mapenzi
Kwa rehema za mwenyezi
Ulile nani kakupa?
Ewe tunda kuwa makini
mafisadi wapo kazini
Walile kwa kisirani
Ufisadi uko kichwani
Sheria za chetu kijiji
Tunda la kujifariji
Posa adhima twataraji
Mzee Ali na Miraji
kwa heshima na adabu
Tunda si tunda doa
wala si tunda poa
Tunda tunu limetulia
Acha kulipapia
Mwanakijiji sahau
ReplyDeleteTunda sikama pilau
Kwamba akila Bahau
Halifai kurudia
Tunda halina makombo
Jilie usende kombo
Usilete zako nyimbo
Tunda umetunukiwa
Hakuna cha peke yako
Vitamu ule na wenzako
Ukijilia kivyako
Utakufa peke yako
Tamati natia nanga
Usiseme nakusimanga
Tunda usije linanga
Kula ushatunukiwa
Wajameni kwa kweli mmenifurahisha na hizo ngano zenu! Ndugu yangu Mwanakijiji mimi binafsi huwa sipendi kula kitu kilichoshikwa na mikono ya watu wengine!huwa naona kinyaa! halafu huwezi juwa mtu aliyekula au kumega alinawa mikono, alivaa gloves au meno yake hayakuoza?
ReplyDeletehahahahahahahaaaa teh teh teh uwiiiii jamani mmeshindikana wana-blogu hii,,,hahahahaaa
ReplyDeletekila mtu na tafsiri yake
Hili tunda, ni tunda gani?
ReplyDeleteLinatoka Mpanda, Au Usambaani?
La mtini tunda, au tunda akilini?
Tunda ni kinda, moyo majaribuni?
Si yako halali, nawe umeibaini
Hujapata iqbali, kulitia mdomoni
Cha mwenzio ghali, sumu kijiini
Tunda ni kinda, moyo majaribuni
Jiziwiye kwa hali, upate makini
La mwenzio muhali, hili ulibaini
Lile wala hili, usilete tafrani
Tunda ni ghali, moyo majaribuni
Sheria za mwili, twahara moyoni
tunda batili, utaingia motoni
Ule vya halali, vibudu usitamani
Tunda ni ghali, moyo majaribuni
Virusi vya mwili, tena asilani
Sikubali wawili, kumega kilaini
Unaijua hali, vumilia jamani
Tunda ni ghali, moyo majaribuni
Subiri lako, la mwenza si lako
Huko yatokako, na lako liko
Fanya msako, usijali masumbuko
Tunda ni ghali, salama kusubiri
Jamaa ushapata majibu, au hujaridhika?
ReplyDelete