mzinga huu umelia usiku wa kuamkia leo barabara ya bagamoyo rodi, karibu na moroko baada ya hiace kuibamiza ubavuni na zote kuingia mtaroni, hili likibamizwa tena kwenye mstimu. ishukuriwe hakuna aliepoteza uhai na jamaa watatu waliokuwemo humu walikimbizwa hospitali wakiwa na majeraha. ushauri umetolewa wadau kuwa waangalifu barabarani katika wakati huu wa msimu wa sherehe na funga mwaka



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. HAPO NDO UKUTE NI YA MKOPO HATA NUSU HAIJARUDI, AFU IMEPIGWA BIMA THIRD PARTY!!!!!!

    HAO JAMAA NAUHAKIKA WAKO KATIKA HARAKATI ZA KUAMBULIA CHOCHOTE MANA HAKUNA SURA YA USAMALIA WEMA HAPO ....WIZI MTUPU HAPO!!!!!!!!!

    NINGEKUWA NA UWEZO DALADALA ZISINGETEMBEA BARABARANI WALLAH WEHU SANA!

    ReplyDelete
  2. Maeneo hayo hayo ya morocco jana usk kuna coaster moja lenye ufito wa rangi nyekundu route za morogoro road kama sijakosea lilitumbukia morocco upande wa kushoto mwa barabara inayoenda mwenge(yani kushoto kama unaelekea mwenge), sikuweza kupata maelezo zaidi, so tuwe waangalifu jamani.

    ReplyDelete
  3. Dah Michuzi mbona hujatumbia hao mafundi wametoka kampuni gani maana inaonekana wanajali sana wateja.. si unaona mwenyewe walivyofika eneo latukio haraka na kuanza kushughulika!!

    ReplyDelete
  4. Hao wanaokoa au wanastrip gari ya watu. Police wa kupima hiyo ajali hamna na towing company vipi?

    ReplyDelete
  5. BONGO TAMBARARE POMBE NA MAGARI!+ hamna sheria barabani.Hufungwi ukishikwa umelewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...