Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya (kulia) akipokea cheti kutoka mwa Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khalid Muhtadi baada ya kuibuka mfanyakazi bora wa kitengo cha uhusiano wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuuaga mwaka 2008, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wiki hii.
Mameneja Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto) na Costantine Magavilla wakitumbuiza kwa kuimba wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008

Mmoja wa wafanyakazi wa Zain Tanzania, Godfrey Kavishe akionyesha kipaji cha kuimba kwa hisia wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.

Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Zain Tanzania, wakishangilia huku akiinua juu kombe baada ya kuibuka washindi wa kudansi wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008

Meneja Kumbukumbu wa Zain Tanzania, Hilda Nakajumo (mbele) akiwaongoza wenzake kucheza dansi wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.

Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya (kulia) na Dangio Kaniki wakiwaongoza wenzao wa idara ya utawala na uhusiano wa umma kucheza mdumange wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. WHATS UP WITH THE BOOTS WHEN PEOPLE ARE COMPLAINING HOW HOT DAR IS?

    ReplyDelete
  2. Hi Beatrice
    Hongera dada kwa kupewa zawadi ya mfanyakazi bora najua lazima iwe hivyo kwani unakumbuka zile shughuli za kifungilo zinatufundisha mambo mengi tumshukuru sister Fide japo tulikuwa tunaumia lakini hayo ndiyo matunda yake hongera mpenzi ni tunakupata vilivyo huku na hiyo ngoma nafikiri unakumbuka kifungilo miaka ya 1994 kama sikosei big up shost

    ReplyDelete
  3. Mie Namefika kwa huyo bi Hilda, naona binti mungu amekujalia.Umbo na courage pia.mmh kweli fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

    ReplyDelete
  4. Anon wa kwanza kabisa hapo juu... Nakuunga mkono, mguu, shingo na kila kitu. Huyo dada wa Mabuti kweli jamani hata hapa Bongo unatuvalia mabuti pia. Mbona unatuaibisha. Sasa na walio Marekani huko kwenye Winter wavae nini. Jamani... hivi Bongo nako kuna baridi kiasi cha kuvaa buti au ni kuiga walio nchi za nje? Au kuna hata snow siku hizi mie sijui... Naomba nifahamishwe!
    This is too much!!! Michuzi hebu elimisha ndugu zetu basi maana na wewe safari za Ukerewe unazipiga sana mzee!!

    ReplyDelete
  5. we mwanamke acha ushamba bwana mbona unajidhalilisha hivyo joto lote ilo boot miguni za nini, acheni ushamba bongo mbona joto ndio lina viwalo kibao na bongo sasa hivi tambalale sasa we inakuwaje shoga mbona unakuwa kama mgeni wa mambo

    ReplyDelete
  6. Hilda Nakajumo!! Umependeza dada!!

    ReplyDelete
  7. huyo aliyevaa mabuti ukiangalia sana atakuwa mchaga huyo

    ReplyDelete
  8. NYIE SEMENI YOTE MWENZENU NDO ANAPETA NA USHAMBA WAKE,AJIRA SAFI NA MSHAHARA MNONO NYINYI JE?NYIE SI MPO KWA AJILI YA KUANGALIA MAKOSA!!

    ReplyDelete
  9. heheheh nyie watu nyie ati mchagga.....

    Na boots zake kaletewa zawadi au ni sagura sagura sasa mnategemea ata vaa wapi

    Na anayesema mishahara minono who knows it is true lakini watu hawahami kwa baba. I don't get that.....Mishahara minono waishi wenyewe basi. Mpiga box mashuhuri lakini nina kwangu. Summer nilikua bongo rafiki zangu bado wanaishi kwa baba zao. Wanalalia chumba kile kile walichokulia.

    Wazuri wa kulemea wengi ni maeneo ya upanga, masaki, kimara na Obay. Tokeni kwa wazazi basi kama mnamake good money. Hamtaolewa mkikaa kwa wazazi jamani.

    ReplyDelete
  10. WE INAONEKANA UMESAHAU MILA ZETU MWANAMKE AONDOKI NYUMBANI MPAKA AOLEWE,NAFIKIRI NDO MAANA BADO WAKO HOME.

    ReplyDelete
  11. dangio kaniki ndie aliyesomaga zanaki au majina yanafanana??kama ni yeye amerudi lini bongo? si alikuwa ughaibuni? poa dada mungu akujalie udumu katika ajira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...