Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Mzee Chediel Yohana Mgonja aliyewahi kushika nyazifa tofauti Serikalini ikiwemo Waziri wa Elimu, Waziri wa Utamaduni na Michezo na Waziri wa Mambo ya nje katika serikali ya awamu ya kwanza. Mzee Mgonja alifariki juzi kutokana na ugonjwa wa kisukari. Anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Same mkoa wa kilimanjaro.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na kuagana na Mzee Ibrahim Kaduma Shemeji wa Marehemu Chediel Yohane Mgonja wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mlimani jijini Dar es salaam leo kufariji wafiwa na kuaga mwili wa marehemu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. http://www.youtube.com/watch?v=bvXdQziITGA&eurl=http://nukta77.blogspot.com/2009/02/video-ajali-ya-kutisha-iliyotokea.html&feature=player_embedded

    ReplyDelete
  2. Sad, very sad ..... Poleni sana. May his SOUL rest in peace. This is from an Old Friend of Nashanda from 30yrs ago.

    ReplyDelete
  3. Mgonja na Katibu mkuu Tiba Kwetira walikuwa viongozi katika wizara za Michezo na vijana wakati wa Mwalimu nyerere. Hii ni pamoja na mzee wangu Nhigula senior siyo mbunge na balozi ambaye alikuwa katibu mkuu msaidizi ardhi. Hawa wazee very humble na serikali ya Tanzania ya sasa lazima wajiulize kwa nini viongozi wa sasa hawafuati mfano wa hawa wazee...

    ReplyDelete
  4. NAKUMBUKA MGONJA ALIPOKUJA KUWA MKUU WA MKOA WA MTWARA NA MAGWANDA YAKE YA JKT YA MWANZO KABISA YALIKUWA YA KADETI, ALIKUWA KIJANA MACHACHARI NA ALIKUWA ANAPENDWA NA NYERERE. HATA MIMI NILIMPENDA WAKATI HUO NIKO PRIMARY SCHOOL

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi,
    Nadhani ungetugeuzia hiyo picha ya marehemu tukaiona badala ya hao wakubwa wanaotia sahihi tungefaidika zaidi. Hao walio hai tutaendelea kuwaona tu.

    Asante!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...