kwa kawaida kaburi alilozikwa mpendwa huwa linajengwa vizuri sio tu katika kulihifadhi bali pia kumuenzi marehemu. kwa mchezaji wa yanga hayati saidi mwamba 'kizota' aliyefariki februari 11, 2007 baada ya kugongwa na daladala akiwa sheli ya temeke vetenari, ni kinyume kama taswira hizi zilizopigwa katika makaburi ya kisutu jijini dar zinavyoonesha



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2009

    Mwenyezimungu amuweke mahali pema peponi mwenzetu yupo kwenye haki.
    mbona sijawaelewa hapo limesahaulika vipi? Nyie kwani mnafikiri Makaburi ni nyumba? sioni kilichosahaulika kazikwa inavyotakiwa ni kwenda tu kumsomea kwani mnataka kaburi liwe vipi? Gorofa? tumuache mwenzetu apumzike. MZ. Au ndugu yangu unamaanisha Tarehe kama Tarehe ni sawa labda kama unaishi Marekani utasema hapo Mwezi wa 11 tarehe 2. Ila sijaona kilicho sahaulika Tunakuomba tufafanulie vizuri nini kimesahaulika?.

    ReplyDelete
  2. Pat-MagazetiJune 21, 2009

    Saidi Mwamba Kizota alikuwa kama role model kwa Watanzania wengi walikuwa wanafuatilia mchezo wa mpira wa miguu Tanzania. Vile vile wapo wachezaji wengi sana waliopita kama Rosta Nduguru, Mohamedi Kajole, Omar Mahadhi, Steven Chibichi, Saleh Sonda, Method Mogella "Fundi", Justin Mtekere, Hamis Gaga, Ramadhani Lenny, Issa Athumani, Athumani Mambosasa, Rafael Paul, Innocent Haule, na wengine hata majina yao siwezi kuyakumbuka. Hawa wachezaji walikuwa role model kwa vijana wengi Tanzania na walichenza mpira wa miguu kwa tabia nzuri bali hali ya maradhi iliwakuta na sasa mungu walaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2009

    Kujengea makaburi ni kinyume na Sunnah za Mtume Muhammad s.a.w
    Someni dini muelimike msikurupuke kufanya mambo ndivyo sivyo..
    Kama ilivyo kwa taaluma nyingine, huwezi kukurupuka ukajijengea nyumba yako mwenyewe, au kumchoma mkeo sindano akiumwa au kurusha ndege pasi na utaalamu basi heshimuni na elimu hii takatifu kabisa kutoka kwa Allah.
    "Fasalu ahla aldhikri inkuntum laa taalamun (Na muwaulize wanaofahamu iwapo hamfahamu)", "Hal yastawi aladhiina yaalamuun wa aladhina laa yaalamun (Hivi wako sawa wanaofahamu na wasiofahamu?)" Nukuu kutoka katika Qura'n.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2009

    Swadakah Anonymous.
    Kaka ISSA Michuzi naona Injili imejaa zaidi kuliko Quran.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2009

    Inalillah wainaillah rajiun!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2009

    kwa kweli hapo kisutu wanakataza kujengea makaburi lakini watu wakubwa na maarufu na hao hao wanaokataza wanayajengea ya ndugu zao!
    binafsi tulikatazwa kujengea kaburi la mzazi wangu, lakini cha kushangaza nilikuwa huko dar mwaka jana nikaenda hapo kisutu na kukuta makaburi ya watu nnaowafahamu wamefariki baada ya mzazi wangu na makaburi yao yamejengewa vibanda kabisa nafkiri mwenyewe umeshuhudia! kaburi la mzee wangu kibao bado kidogo kianguke na kingeanguka ndo basi tena limepotea bahati mbaya watoto wote tuko nje ya nchi hakuna wakulizuru kila siku kuhakikisha alama haipotei, nani atakae penda apoteze mahala alipozikwa mzee wake?
    kwa hiyo vibaya ni kujengea kwa kupitiliza lakini alama kama kuzungushia matofali na kulitunza kwa kufanyiwa usafi ni muhimu.
    na mwisho maustadhi hapo juu:-
    kutokujengea makaburi ni sunnah na si fardhi, kwa hiyo si lazim kufata sunnah na ndiyo maana ikatofautishwa na fardhi ambayo ni LAZIM! TAFADHALI msitake kuyakuza hapa! Nyinyi ndo mnaifanya dini ionekane ngumu kwa kuyakuza mambo kwa kuzifanya sunnah kuwa fardhi!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2009

    Mdau hapo juu, kwa taarifa yako Innocent Haule ni mzima wa afya. Rekebisha kumbukumbu zako!!

    ReplyDelete
  8. zitto kiaratuJune 22, 2009

    jamani marehemu said nassor si yule alichezea cosmopolitan ya dar miaka ya sabini au ni nassor mwingine

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2009

    duh! kaka michuzi,tupo pamoja lakini kwenye hili la mambo ya makaburi naona huna uraia wa uislam,inabidi tusikilize hata suratul kadhaa toka kwako,maana mmh! tafuta muda usome hadithi wakati mwingine,ni kwa imani tu.ila poa sana maana wengine pia walikuwa hawajui.inshaallah wataelewa sasa.pia waeleze wadau kuwa kulijengea kaburi na kuliwekea nakshi zoote sio kuwa ndio kuonyesha mapenzi yetu kwake.swala ni kumuombea kwa mwenyezi mungu yeye na wengine waliotangulia mbele ya haki.
    akihito

    ReplyDelete
  10. ndugu yangu hapo juu, angalia kauli zako. inaposemwa sunna si lazima haimaanishi tunaweza kuidharau. inapotokea unadharura na ukashindwa kuitekeleza sunnah hapo swadakta, lakini unapaswa kuitekeleza sunnah popote inapobidi, kwa maana waislamu tumeimizwa kuishi kwa kufuata Qur'an na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W). na dini haiwezi kua ngumu kama utajikumbusha wajibu wako wa kuumbwa i.e. kuabudu.

    ReplyDelete
  11. Mimi sijui Koran(sababu ni Mkristo) inasema nini hata kusoma kiarab sijui.Napenda kuuliza hawa wanaonukuu koran na mafundisho ya Mtume Mohammed S.A.W,je huko Arabuni(Saudi Arabia,Oman nk) watu wa huko hawajengei makaburi ya wapendwa wao au ni wa-Afrika tu wanaotakiwa kufuata mafundisho kama yanavyosema?
    Najua hapa USA (toka sehemu mbalimbali duniani)waislam wanajengea makaburi ya wapendwa wao.
    NI swali tu.Sina nia ya kuchafua Hali ya hewa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 22, 2009

    WENGINE WALIOTUTANGULIA MBELE ZA HAKI NI HAWA WAFUATAO:- EDWARD CHUMILA (EDO BOY),SAID MWAIBAMBE ZIMBWE, MUHEHE KIHWELO, RIFAT SAID, JOSEPH KATUBA, SAHAU SAID KAMBI, JAMES TUNGARAZA etc. MOLA AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI.. AMEIN

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2009

    Pia Steven chibichi bado yupo hai

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 22, 2009

    Vingine tuwaachie ndugu wa marehemu. Ni mapenzi yao kuweka au kutoweka. Sio kila kitu kifanyike tupendavyo sisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...