Ooooh narudi nyumbani oooh!
ohhh narudi bongo,
ooh narudi kijitonyama eeh!
Nimeamua kurudi nyumbani!
nyumbani ni nyumbani
hata kama kuna mgao wa maji,
hata kama taka na vumbi kila kona,
Maisha ya box kwa Obama yamenishinda eeeeh!
Mdau Lilly
(njiani kurudi nyumbani.
Tuonane American Chips J'Mosi P'se!!!)
Aisee umesahau mgao wa umeme, ununue na jenereta, halafu ukibadilisha hela uwe na buku buku ya kugawa,teheheee si umetoka majuu!!!. Jihadhari utapeli kila kona hata kama ni nduguyo anaweza kukuliza.wamachinga ndio usiseme, kitu cha Tsh 200 watakuliza kwa Tsh2,000, halafu utafikiri umepata kwani bei walioanzia ni Tsh.20,000.Usiwasahau wale wazoefu wa kutaja hela nyingi mfano milion 100, mabilioni lakini mwisho wa maongezi wanakuomba mia tano.
ReplyDeleteOtherwise mambo ni shwari, Bongo tamabarare.
Mdau Trondheim Norway
Genious!!!
ReplyDeleteMBONA UTENZI KAA WA DR SHAYO NA JOHNI MASHAKA AMBAO WANARUDI KUCHUMA PESA BWANA???
ReplyDeletewewe siyo bure lazima una deportation notice,morgage zimekuzidia,or may be child support zinakusumbua.maisha marekani ni matamu ni juhudi yako na heshimu system yao.
ReplyDeleteCredit Crunch imewafanya mbaya mtu kibao. Mtu kibao zinatoa visingizio visivyo na msingi eti sijui mda muafaka ulifika wa kurudi home, ila ukweli ni kwamba credit crunch imeua...
ReplyDeleteTumekuelewa dada.
shwenga karibu tupo pamoja nilifikiri ni mimi tu nimechoka kukaa mbuga ya serengeti "kwa Obama", nami nimechoka box, narudi nyumbani, nawaachia wengine wajaribu bahati yao na wakaribisha kwa mzee Obama.
ReplyDeleteyeyote atakayempinga huyu dada basi ni mshenzi. achana nao da' lily wewe una akili sana karibu tanzania tena. karibu nyumbani.
ReplyDeleteeti ooh maisha marekani matamu...acha ulimbukeni wewe. matamu kwani kwenu hapa!!! utabeba box hadi kufa kwako kisa maisha matamu badala ya kupeleka vyeti bongo ukapate kazi yenye heshima umekalia box kuosha vyoo vya watu, cha kwako nyumbani ukioshe na wananyea wenzio pia uvioshe wapi na wapi bwana!!! da' lily hongera sana. ningependa nikuone pale amerikan chips sababu nami ntakuwa bongo that day. nipe mawasiliano basi tukae2009@hotmail.co.uk
absolutely brilliant!
ReplyDeleteKaratasi zake zilioza zamani kashaambiwak urudi kaa ibiak ukaa we mwisho yamembana hana wakumsaidia karudi nyooo huku ndio bongo tuone na huku? utaweza kama hujaishia Leo brazameni huyu kesho brazameni huyo Keshokutwa Angaza unapima unawacha kipimo palepale haaha. Bongo tumia Ubongo dada wee njooo tu utakuwa gunia la mazoezi la wageni na wenyeji. Teja.
ReplyDeletekwani katoa kisingizio gani si kasema hapo kwamba kubeba box kumemshinda.....karibu dada. watu bwana mtu akiamua kubaki huku mnasema anadahrau nchi yake akiamua kurudi mwaanza kumsema tena khai!
ReplyDeleteHongera Dada Lily kwa uamuzi wako wa kishujaa, kwani hata kama ni Global Financial Crisis lakini umekubali kujishusha na kuanza alifu, usikonde unaweza ukafanikiwa hapa bongo kwa muda mfupi mpaka ujute muda uliopoteza huko majuu,
ReplyDeletekaribu bongo
Wewe ndiyo mwenye busara ... kama una elimu yako ya maana rudi tu baada ya muda mfupi utagundua kwamba uamuzi wako ni mzuri sana.
ReplyDeleteKaribu nyumbani tusaidiane kuinuia jamii yetu ya Tanzania.
Maisha Bongo matamu sana! Bongo kila kitu easy kazi kidogo kuku kwa mrija, Mimi mwenyewe nimechoka na pressure za huku uzunguni! Bongo Gari ya 199.. ni mpya! na ukiingia barabarani respect kama kawaida! Utasikia waswahili wanasema! JAMAA ANA GARI YULE...! Mianya ya biashara ipo!!!!!!! Shida iko wapi! Welcome Home baby!
ReplyDeletedada lily mie nakuunaga mkono watu tunaogopa kurudi nyumbani tu,waliotangulia sasa wako mbali uzuri nyumbani ukiwa na ujasiri hat maji utauza,kuana kila aina ya biashara ni kujituma tu mie namalizia masomo yangu nitajichanganyapia,kajitume dada wanawake wanapiga bao siku hizi bongo biashara kibao,kuna ambao hata ulaya hawaijui na maisha tambarare 'kinoma MAY GOD BE WITH' huku uk kuna hadi waliorudishwa miaka miwili iliyopita sasa hivi ni kitu kingine,kujituma kwako tu,
ReplyDeleteBrilliant! achana na winter, makoti, jackets,jeans,min skirts etc.karibu nyumbani kwenye maisha ya maraha, bongo unakandamiza pambazzz zenye akili muda wote na unaingia barabarani na mchuma wako kila mtu ataheshimu,maisha bongo ni mazuri sana kila siku bongo ni kama sikukuu. karibu sana mwanawane, wabeja sana.
ReplyDeletekaribu nyumbani
ReplyDeletewelcome home babe
lily umefanya uamuzi sawa kabisa,kuna wengine wako huko wanatamani kurudi walikotoka lakini ndo wameshazoea kubeba box na hata wakirudi nyumbani heshima itakua hamna...big up girl...all the best
ReplyDeleteYaani we Lilly sijui nikuambiaje? mimi nimechoka kupita kiasi Ulaya, bili kila kona, hujalipa hii, hii imejitokeza, nyumbani mama anataka pesa kila mwezi,baridi huthubutu hata kutoka nje labda uende shule, kazini na market au sivyo wewe ni ndani tu, Mtunda kama miwa, mafenesi, maembe, mapera na nk huwezi kununua hata kidogo, yaana lilly kikubwa kwangu kinachoniweka ni kuwasomesha watoto wangu,wakimaliza mimi nitakuwa nyuma yako mdogo wangu.Mademe
ReplyDeleteLili nakufagilia mimi nimerudi nyumbani nimekuta kina mama wanapesa kama hawana akili, wanaenda china, Dubai, Marekani, kibiashara kweli wameendelea sana, nyumbani mikopo ipo, ukituliza akili utafanikiwa sana dada.
ReplyDeleteMdau fanya uingize sauti basi halafu bandika kitu kwa Youtube.
ReplyDeleteHii tungo nzuri sana.
Wabeba box mliojaaliwa sauti nzuri za kuimba hebu fanyeni Shindano la kuingiza vocal mumsaidie mdau mwenzenu.
Wadau wa Bongo Tambarare tutatoa zawadi ya one way ticket to Dar es Salaam au Arusha kwa mshindi.
Tehe tehe teh teh ...
Najua nyumbani ni nyumbani lakini kama umezoea ya majuu ya yhapo yatakuwa magumu!! Acha sisi tuendelee kupiga box while tunakula jasho letu!! Bye bye nenda najua karatasi limeisha ukipata tena we njooo tu kazi hapa za kubeba box zinasubiri!!!!
ReplyDeleteKama una beba box marekani maan yake huna elimu, Bongo bila elimu utalikumbuka hilo box. I hope you have a plan lilly.
ReplyDeleteUende tuu Dada, wengine watakufuata, sisi tutarudi B'dae.
ReplyDeleteB.
Da' Lillian wewe rudi home bwana unaweza kujaribu huko kama mambo huku hayakuwa safi. Kote kunawezekana kunalipa karata uchezwa sehemu zote sio US tu. Maisha ya bongo tunayafahamu na tuyasoma na tunayajua hakuna mtu anaweza kumdanganya mtu. Maisha ya US waliopata kuishi na kukaa wanajua yakoje na ubaya na utamu wake. Kwa hiyo ujafanya kosa kurudi home. Wewe salimia familia huko bongo wacha sisi tuendelee kula maisha. US inzuri kama unajua unafanya nini lakini. Nafahamu wengine wanakuwa hawajapata muongozo mzuri then wanaingia kwenye matatizo. Ni machache yangu
ReplyDeleteDada hata mie katibu narudi home. Huku nina makaratasi kazi nzuri sana vyeti vya uhakika lakini nyumbani ni nyumbani hata nikalale kwenye mkeka. Pia nimechoka kukimbiza pesa western union wacha tukapambane wote huko huko kama sina basi tuangaliane wote.
ReplyDeleteDada lily mimi nitakuunga mkono siku si nyingi kwani nami box limenishinda. kwanza limekuwa gumu kupatikana halafu ukilipata ni la muda mfupi. Niko shule mungu akipenda namaliza Dec, punde nimalizapo nitajiunga na wewe. Nakutakia kila la kheri naamini utafanikiwa usisahau usemi usemao mtu kwao.
ReplyDeletelily ujue kila siku kuna vikwazo maishani mfano utakutana na watu ambao kazi yao kukatisha tamaa watu wengine, wewe kama umeamua kufanya kazi au kujiajili fanya tu utakapo fika Bongo usiogope kujichangaya, usisikilize watu wa kukatisha tamaa, tumia ujuzi na akili ulioipata kutoka huko ughaibuni, utafanikiwa, nasema hivyo kwani mimi sasa nina kampuni yangu mara baada ya kurejea kutoka ughaibuni mpaka watu wakasema si bure kaaga kwao, ila maisha mazuri, mambo yametulia. nakamata million(vijisenji).
ReplyDeletejamani hebu tuongee ukweli maisha ni sehemu yoyote ulipo it doesnt matter upo marekani au TZ au uchina so longer as unaededesha maisha yako vizuri and you play yr cards well so hao wanoijifanya wamechoka kubeba mabox ni wazushi sio kila aliye marekani anabeba box please! unaweza ukasota bongo vilevile tz watu hawalipi bills ndio maana umaskini hauishi ile nchi ulaya billis they have to be paid na ndio maana nchi hizi zinaendela so kila mtu na choice yake ulipokuja marekani hukubisha hodi so unapoondoka nenda kama ulivyokuja waacha wenzio wanoendelea kutafuta ku keep kusingizia mabox ni "denial" unataka hutaki njia nyeupe....
ReplyDeletedada lilian tairo nakuonea huruma maana shule hujaenda ulikuwa ukibeba box tu na kumlea mzahamu,sasa umepoteza mda unarudi bongo bila elimu uamuzi wako ni mzuri ila ingia hata chuo bongo maana vijana wadogo wamesoma na wana hela,wewe unafikilia kwenda american chips kuvizia mabuzi au?beba box la mwisho upate pesa zako za tax mwakani ili ukafanye jambi la maana usikurupuke kisa umechoka ndo maisha uliyoyachagua toka mwanzo la kulea mwanaume na kubeba box,kuwa mjanja na akili ukiridi bongo sasa umekuwa mtu mzima tengeneza maisha yaliyobaki
ReplyDeleteUnarudi mwenyewe au umefukuzwa. Unabahati hata wewe unaweza kuaga. Manake nasikia kuna mhaya mmoja New Jersey yupo jela anangoje akurudishwa bongo. Hata kwenda kukusanya vitu vyake hawajamruhusu kaka wa watu.
ReplyDeleteDAH KAKA HAPO JUU UMEMALIZA KABISA KUMBE UNAMJUA LILY VIZURI HIVYO?ANYWAY KAMA NI KWELI BASI LILY TULIZANA KWANZA HAPA PIGA SHULE KWANZA,WENGINE TUMETOKA BONGO JUZI TU TUNASAKA MASHULE ZAIDI MITAA HII KAMA UJAPIGA SHULE YA MAANA BONGO UTAISHIA JOLLY CLUB BUREE MANAKE KULE BONGO AKUNA BOX,NA NEXT TIME UWE WISE ACHAKULEA WEHU!!NA MARA NYINGI WANAORUDI KIUKWELI UWA AWATANGAZI MICHUZI!!
ReplyDeleteMDAU LILY TUANDAE MKEBE KUKUPOKEA AU PICK-UP? TUELEZE UNAKUJA NA SANDUKU NGAPI AU BOKSI NGAPI...
ReplyDeleteKARIBU SANA NYUMBANI, HUKU HATUNA RED CARPET TUNA VUMBI LINAKUSUBIRI
Kuna Lily mwingine karudi home toka kwa Malkia ila yeye kashapiga Masterz yake. Kufika home aka-angusha kilio cha nguvu yaani haamini kama kweli kaachana na maisha ya Box sio mchezo.
ReplyDelete