Ooooh narudi nyumbani oooh!
ohhh narudi bongo,
ooh narudi kijitonyama eeh!
Nimeamua kurudi nyumbani!
nyumbani ni nyumbani
hata kama kuna mgao wa maji,
hata kama taka na vumbi kila kona,
Maisha ya box kwa Obama yamenishinda eeeeh!
Mdau Lilly
(njiani kurudi nyumbani.
Tuonane American Chips J'Mosi P'se!!!)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2009

    Aisee umesahau mgao wa umeme, ununue na jenereta, halafu ukibadilisha hela uwe na buku buku ya kugawa,teheheee si umetoka majuu!!!. Jihadhari utapeli kila kona hata kama ni nduguyo anaweza kukuliza.wamachinga ndio usiseme, kitu cha Tsh 200 watakuliza kwa Tsh2,000, halafu utafikiri umepata kwani bei walioanzia ni Tsh.20,000.Usiwasahau wale wazoefu wa kutaja hela nyingi mfano milion 100, mabilioni lakini mwisho wa maongezi wanakuomba mia tano.

    Otherwise mambo ni shwari, Bongo tamabarare.

    Mdau Trondheim Norway

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2009

    Genious!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2009

    MBONA UTENZI KAA WA DR SHAYO NA JOHNI MASHAKA AMBAO WANARUDI KUCHUMA PESA BWANA???

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2009

    wewe siyo bure lazima una deportation notice,morgage zimekuzidia,or may be child support zinakusumbua.maisha marekani ni matamu ni juhudi yako na heshimu system yao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2009

    Credit Crunch imewafanya mbaya mtu kibao. Mtu kibao zinatoa visingizio visivyo na msingi eti sijui mda muafaka ulifika wa kurudi home, ila ukweli ni kwamba credit crunch imeua...

    Tumekuelewa dada.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2009

    shwenga karibu tupo pamoja nilifikiri ni mimi tu nimechoka kukaa mbuga ya serengeti "kwa Obama", nami nimechoka box, narudi nyumbani, nawaachia wengine wajaribu bahati yao na wakaribisha kwa mzee Obama.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2009

    yeyote atakayempinga huyu dada basi ni mshenzi. achana nao da' lily wewe una akili sana karibu tanzania tena. karibu nyumbani.
    eti ooh maisha marekani matamu...acha ulimbukeni wewe. matamu kwani kwenu hapa!!! utabeba box hadi kufa kwako kisa maisha matamu badala ya kupeleka vyeti bongo ukapate kazi yenye heshima umekalia box kuosha vyoo vya watu, cha kwako nyumbani ukioshe na wananyea wenzio pia uvioshe wapi na wapi bwana!!! da' lily hongera sana. ningependa nikuone pale amerikan chips sababu nami ntakuwa bongo that day. nipe mawasiliano basi tukae2009@hotmail.co.uk

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2009

    absolutely brilliant!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2009

    Karatasi zake zilioza zamani kashaambiwak urudi kaa ibiak ukaa we mwisho yamembana hana wakumsaidia karudi nyooo huku ndio bongo tuone na huku? utaweza kama hujaishia Leo brazameni huyu kesho brazameni huyo Keshokutwa Angaza unapima unawacha kipimo palepale haaha. Bongo tumia Ubongo dada wee njooo tu utakuwa gunia la mazoezi la wageni na wenyeji. Teja.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2009

    kwani katoa kisingizio gani si kasema hapo kwamba kubeba box kumemshinda.....karibu dada. watu bwana mtu akiamua kubaki huku mnasema anadahrau nchi yake akiamua kurudi mwaanza kumsema tena khai!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 10, 2009

    Hongera Dada Lily kwa uamuzi wako wa kishujaa, kwani hata kama ni Global Financial Crisis lakini umekubali kujishusha na kuanza alifu, usikonde unaweza ukafanikiwa hapa bongo kwa muda mfupi mpaka ujute muda uliopoteza huko majuu,
    karibu bongo

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 10, 2009

    Wewe ndiyo mwenye busara ... kama una elimu yako ya maana rudi tu baada ya muda mfupi utagundua kwamba uamuzi wako ni mzuri sana.

    Karibu nyumbani tusaidiane kuinuia jamii yetu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 10, 2009

    Maisha Bongo matamu sana! Bongo kila kitu easy kazi kidogo kuku kwa mrija, Mimi mwenyewe nimechoka na pressure za huku uzunguni! Bongo Gari ya 199.. ni mpya! na ukiingia barabarani respect kama kawaida! Utasikia waswahili wanasema! JAMAA ANA GARI YULE...! Mianya ya biashara ipo!!!!!!! Shida iko wapi! Welcome Home baby!

    ReplyDelete
  14. dada lily mie nakuunaga mkono watu tunaogopa kurudi nyumbani tu,waliotangulia sasa wako mbali uzuri nyumbani ukiwa na ujasiri hat maji utauza,kuana kila aina ya biashara ni kujituma tu mie namalizia masomo yangu nitajichanganyapia,kajitume dada wanawake wanapiga bao siku hizi bongo biashara kibao,kuna ambao hata ulaya hawaijui na maisha tambarare 'kinoma MAY GOD BE WITH' huku uk kuna hadi waliorudishwa miaka miwili iliyopita sasa hivi ni kitu kingine,kujituma kwako tu,

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 10, 2009

    Brilliant! achana na winter, makoti, jackets,jeans,min skirts etc.karibu nyumbani kwenye maisha ya maraha, bongo unakandamiza pambazzz zenye akili muda wote na unaingia barabarani na mchuma wako kila mtu ataheshimu,maisha bongo ni mazuri sana kila siku bongo ni kama sikukuu. karibu sana mwanawane, wabeja sana.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 10, 2009

    karibu nyumbani

    welcome home babe

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 10, 2009

    lily umefanya uamuzi sawa kabisa,kuna wengine wako huko wanatamani kurudi walikotoka lakini ndo wameshazoea kubeba box na hata wakirudi nyumbani heshima itakua hamna...big up girl...all the best

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 10, 2009

    Yaani we Lilly sijui nikuambiaje? mimi nimechoka kupita kiasi Ulaya, bili kila kona, hujalipa hii, hii imejitokeza, nyumbani mama anataka pesa kila mwezi,baridi huthubutu hata kutoka nje labda uende shule, kazini na market au sivyo wewe ni ndani tu, Mtunda kama miwa, mafenesi, maembe, mapera na nk huwezi kununua hata kidogo, yaana lilly kikubwa kwangu kinachoniweka ni kuwasomesha watoto wangu,wakimaliza mimi nitakuwa nyuma yako mdogo wangu.Mademe

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 10, 2009

    Lili nakufagilia mimi nimerudi nyumbani nimekuta kina mama wanapesa kama hawana akili, wanaenda china, Dubai, Marekani, kibiashara kweli wameendelea sana, nyumbani mikopo ipo, ukituliza akili utafanikiwa sana dada.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 10, 2009

    Mdau fanya uingize sauti basi halafu bandika kitu kwa Youtube.

    Hii tungo nzuri sana.

    Wabeba box mliojaaliwa sauti nzuri za kuimba hebu fanyeni Shindano la kuingiza vocal mumsaidie mdau mwenzenu.

    Wadau wa Bongo Tambarare tutatoa zawadi ya one way ticket to Dar es Salaam au Arusha kwa mshindi.

    Tehe tehe teh teh ...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 10, 2009

    Najua nyumbani ni nyumbani lakini kama umezoea ya majuu ya yhapo yatakuwa magumu!! Acha sisi tuendelee kupiga box while tunakula jasho letu!! Bye bye nenda najua karatasi limeisha ukipata tena we njooo tu kazi hapa za kubeba box zinasubiri!!!!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 10, 2009

    Kama una beba box marekani maan yake huna elimu, Bongo bila elimu utalikumbuka hilo box. I hope you have a plan lilly.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 10, 2009

    Uende tuu Dada, wengine watakufuata, sisi tutarudi B'dae.

    B.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 10, 2009

    Da' Lillian wewe rudi home bwana unaweza kujaribu huko kama mambo huku hayakuwa safi. Kote kunawezekana kunalipa karata uchezwa sehemu zote sio US tu. Maisha ya bongo tunayafahamu na tuyasoma na tunayajua hakuna mtu anaweza kumdanganya mtu. Maisha ya US waliopata kuishi na kukaa wanajua yakoje na ubaya na utamu wake. Kwa hiyo ujafanya kosa kurudi home. Wewe salimia familia huko bongo wacha sisi tuendelee kula maisha. US inzuri kama unajua unafanya nini lakini. Nafahamu wengine wanakuwa hawajapata muongozo mzuri then wanaingia kwenye matatizo. Ni machache yangu

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 11, 2009

    Dada hata mie katibu narudi home. Huku nina makaratasi kazi nzuri sana vyeti vya uhakika lakini nyumbani ni nyumbani hata nikalale kwenye mkeka. Pia nimechoka kukimbiza pesa western union wacha tukapambane wote huko huko kama sina basi tuangaliane wote.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 11, 2009

    Dada lily mimi nitakuunga mkono siku si nyingi kwani nami box limenishinda. kwanza limekuwa gumu kupatikana halafu ukilipata ni la muda mfupi. Niko shule mungu akipenda namaliza Dec, punde nimalizapo nitajiunga na wewe. Nakutakia kila la kheri naamini utafanikiwa usisahau usemi usemao mtu kwao.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 11, 2009

    lily ujue kila siku kuna vikwazo maishani mfano utakutana na watu ambao kazi yao kukatisha tamaa watu wengine, wewe kama umeamua kufanya kazi au kujiajili fanya tu utakapo fika Bongo usiogope kujichangaya, usisikilize watu wa kukatisha tamaa, tumia ujuzi na akili ulioipata kutoka huko ughaibuni, utafanikiwa, nasema hivyo kwani mimi sasa nina kampuni yangu mara baada ya kurejea kutoka ughaibuni mpaka watu wakasema si bure kaaga kwao, ila maisha mazuri, mambo yametulia. nakamata million(vijisenji).

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 11, 2009

    jamani hebu tuongee ukweli maisha ni sehemu yoyote ulipo it doesnt matter upo marekani au TZ au uchina so longer as unaededesha maisha yako vizuri and you play yr cards well so hao wanoijifanya wamechoka kubeba mabox ni wazushi sio kila aliye marekani anabeba box please! unaweza ukasota bongo vilevile tz watu hawalipi bills ndio maana umaskini hauishi ile nchi ulaya billis they have to be paid na ndio maana nchi hizi zinaendela so kila mtu na choice yake ulipokuja marekani hukubisha hodi so unapoondoka nenda kama ulivyokuja waacha wenzio wanoendelea kutafuta ku keep kusingizia mabox ni "denial" unataka hutaki njia nyeupe....

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 11, 2009

    dada lilian tairo nakuonea huruma maana shule hujaenda ulikuwa ukibeba box tu na kumlea mzahamu,sasa umepoteza mda unarudi bongo bila elimu uamuzi wako ni mzuri ila ingia hata chuo bongo maana vijana wadogo wamesoma na wana hela,wewe unafikilia kwenda american chips kuvizia mabuzi au?beba box la mwisho upate pesa zako za tax mwakani ili ukafanye jambi la maana usikurupuke kisa umechoka ndo maisha uliyoyachagua toka mwanzo la kulea mwanaume na kubeba box,kuwa mjanja na akili ukiridi bongo sasa umekuwa mtu mzima tengeneza maisha yaliyobaki

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 11, 2009

    Unarudi mwenyewe au umefukuzwa. Unabahati hata wewe unaweza kuaga. Manake nasikia kuna mhaya mmoja New Jersey yupo jela anangoje akurudishwa bongo. Hata kwenda kukusanya vitu vyake hawajamruhusu kaka wa watu.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 11, 2009

    DAH KAKA HAPO JUU UMEMALIZA KABISA KUMBE UNAMJUA LILY VIZURI HIVYO?ANYWAY KAMA NI KWELI BASI LILY TULIZANA KWANZA HAPA PIGA SHULE KWANZA,WENGINE TUMETOKA BONGO JUZI TU TUNASAKA MASHULE ZAIDI MITAA HII KAMA UJAPIGA SHULE YA MAANA BONGO UTAISHIA JOLLY CLUB BUREE MANAKE KULE BONGO AKUNA BOX,NA NEXT TIME UWE WISE ACHAKULEA WEHU!!NA MARA NYINGI WANAORUDI KIUKWELI UWA AWATANGAZI MICHUZI!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 12, 2009

    MDAU LILY TUANDAE MKEBE KUKUPOKEA AU PICK-UP? TUELEZE UNAKUJA NA SANDUKU NGAPI AU BOKSI NGAPI...
    KARIBU SANA NYUMBANI, HUKU HATUNA RED CARPET TUNA VUMBI LINAKUSUBIRI

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 12, 2009

    Kuna Lily mwingine karudi home toka kwa Malkia ila yeye kashapiga Masterz yake. Kufika home aka-angusha kilio cha nguvu yaani haamini kama kweli kaachana na maisha ya Box sio mchezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...