Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ukombozi Baraka James(kushoto)akisalimiana na Vodacom Miss Tanzania Nasreem Karim wakati wa makabidhiano ya madawati 55 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation leo. Kati ni Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba, Shule ya Uwanja wa ndege ilifaidika kwa msaada huo pia na kupata madawati 55.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi ya uwanja wa ndege wakiwa wamekalia moja ya madawati 55 na kuonyesha alama ya dole kuashiria kufurahia kwao kwa msaada wa madawati waliyopata leo. shule ya msingi Ukombozi alifaidika kwa msaada wa madawati 55 kutoka Vodacom Foundation ambapo imeanzisha kampeni yake ya kugawa madawati 400 katika shule za msingi za Mkoa wa Dar
Mwalimu wa shule ya Msingi ya Uwanja wa ndege Benard Shao(kushoto)akimuonyesha mazingira Mkuu wa Vodacom Foundation alipofika shuleni hapo kutoa msaada wa madawati 55, ambapo Vodacom imeanzisha kampeni yake ya kugawa madawati 400 katika shule za msingi za Mkoa wa Dares Salaam,(katikati)Vodacom Miss Tanzania Nasreem Karim.
Mkuu wa Mfuko wa kutoa misaada wa Vodacom(Vodacom Foundation)Mwamvita Makamba(katikati) akiongea jambo wakati alipokuwa anatembelea moja ya madarasa ambayo hayana madawati katika shule ya msingi ya uwanja wa ndege leo na kutoa msaada wa madawati 55. Mwenye blauzi ya buluu Mwalimu mkuu wa shule hiyo Edita Semkali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2009

    Waosha vinywa mbona mko kimya? Mnapenda mno mambo ya kizushi. Mtu akifanya kitu cha kweli, midomo mnajaza maji ya chumvi. Hongera Vodacom kwa jitihada zenu. Madawati hayo yanaweza yakawaletea IT managers wazuri in the future. Inawezekana kuwa sio sponsors wote wanapata chance kuwekwa kwa Supu, ila wale wasiofanya inabidi waige mifano hiyo mizuri.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2009

    Picha ya pili bado kidogo initoe machozi! Nimeangalia sura za watoto wetu hawa na kujiuliza maswali mengi.

    Swali kubwa wakati naangalia sura za hawa watoto wetU ni future yao itakuwaje? Nimeona kuna uwezekano mmoja wao akawa daktari hapo, mwanasheria, mwanasiasa na mfanyabiashara.

    Lakini swali lingine kubwa ni how these kids watakavyopata hiyo bright future?

    I hope wanasiasa na wananchi watajiuliza haya maswali na kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kwa bidii na kujenga Taifa letu kwa pamoja.

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2009

    hii shule ya msingi uwanja wa ndege ni tofauti na ile shule ya msingi Kipawa ?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2009

    Kazi nzuri Voda walao mnaonyesha jinsi mnavyotujali baada ya kutunyofolea vishilingi vyetu kwa kulonga masaa 24! Lakini kikubwa nimebaki mdomo wazi na kushindwa kuelewa nchi yetu inakwenda wapi. JK na mawaziri wake wamekuwa wakitamba jinsi walivyoboresha elimu! sasa hii ni shule ya uwanja wa ndege (bila shaka wa Mwalimu JKN), mwaka 2009, darasa halina madawati! Je, vifaa vingine viko katika hali gani? je huko Kantalamba si ndio watakuwa hawana hata hicho chumba!!! Mwaka kesho watajipitisha (wameishaanza kufagiliana) kuomba kura ili waendelee kutawala! Ili wafanye nini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2009

    kwa kweli tungekuwa na vodacom kama tatu nne hivi basi watu wangeneemeka.vodacom mnaongoza kwa kutoa misaada everywhere , sio tu kwa sababu michuzi anawarusha bali nafuatilia na vyombo vingine vya habari kwa upande wangu naona mpo juu
    cha muhimu mmsisite kuendelea.

    ReplyDelete
  6. Wadau samahani sana maana mimi hapa hata hayo madawati siyaoni... namuona Mwamvita tu mmmhhhh!! ....''nitalipataje tunda lalaaaaa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...