Kaka michuzi, mimi ni Mtanzania nipo Chuo kimoja kinaitwa Syracuse University, kipo NY, tunajiandaa kufanya kumbukizi ya miaka 10 baada ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyrere, J.K. Nadhani hili litakua ni kumbukizi pekee rasmi katika jimbo zima la New York. Hivyo basi naomba msaada wako, moja, katika kupata picha nzuri ya mwalimu kwa ajili ya kutengenezea bango, na pili kama una video yoyote ya hotuba ya mwalim, ikiwa ya kiingereza itakua nzuri zaidi maaha sehemu kubwa ya hadhira yetu ni wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza. NB; Kama itakuwa ngumu kwako kupata basi naomba uniwekee kwenye libeneke huko ili wadau waweze kunisaidia.
Natanguliza shukrani zangu za dhati,
Wilbert Mahenge,Graduate Assistant - The Africa Initiative
M.A. Candidate, Pan African Studies '11

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hongereni sana Wilbert kwa kuwa wazalendo wa nchi yenu coz most of Tanzanian youth wakiwa nje ubongo wanautupilia mbali, Just keep it up! Am praying 4 U ili tukio liwe la kihistoria....... All the best!
    FROM UR YOUNG BRO
    STANLEY!

    ReplyDelete
  2. aah papaa mahenge a.k.a mzee wa mboga ya matunda. kumbe bado upo kwa mjaluo obama!safi sana.mzee mawasiliano yamekata baada ya kupoteza mail address si unajua pirika za kusaka shilingi bongo.unaweza kunipata katika hamnazo@gmail.com

    kila la heri katika maandalizi ya tamasha lenu.
    wadau wote wa Tabora Boys "old boys" - Hi.

    mimi "Mufti Boka"

    ReplyDelete
  3. OMBI lako peleka JAMII FORUM,vichwa vya tanzania viko kwenye hiyo forum.

    ReplyDelete
  4. nadhani ingekuwa jambo bora ukiwasiliana moja kwa moja na office ya raisi tanzania..

    ReplyDelete
  5. Angalia Youtube kuba baadhi ya clip. Vile vile unaweza kutumia online resource ambayo inatolewa na library ya hapo college kwenu. Ukiingia kwenye database za International studies au Politics then search Julius Nyerere. Kuna publications zake nyingi sana. I mean nyingi sana mimi nime collect nyingi sana.

    Kama unaitaji hizi publications then unaweza kunitumia email

    Mtanganyika01@yahoo.com
    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  6. Video zipo nyingi katika google.com
    kama ukienda google.com halafu type: Mwalimu Nyerere halafu changua video section zipo kibao.unaweza uka-download. Zipo za kiingereza na kiswahili.
    Asante

    You can go to google and type
    mwalimu nyerere and then select Video on the top of the page and should should lots of videos in Swahili and English.


    Ghue ghojo Mahenge, jibidi ovandhekhele avanu avihusika katika amakhitaba
    ghataifa. Avanu khatika omutandao ogho navakhawese okhokhopela isideo syakhengelesi. Jaribu okholonda katika e-google.com
    siolusu ghue. Andekha tu "mwalimu Nyerere halafu minya search" jibidi odaunilodi.

    Khepwamwelelo.

    ReplyDelete
  7. mdau oni lang tu, kanumba au joni mashaka si wote wako malekani na wanaweza kuja kuto mihadhala ya kiingereleza? wanaandikahga maatiko mazuli kwa hiyo watafute. email yake ni jonimashaka2008@yahoo.com na mwenzie ni stevekanumba@gmail.com

    ReplyDelete
  8. Mshkaji unasoma degree mbovu mno, pole.

    ReplyDelete
  9. Nd. Mahenge, ukiwa wewe ni mkazi wa Sirakuza katika jimbo kuu la Nuyoka, Marekani, basi, tuma maombi (e-meili) yako kwenye:

    I.
    LIBRARY OF CONGRESS (Washington DC)
    African and Middle Eastern Division
    Ask a Librarian through e-mail.

    There are thousands of great photos and speeches (on video/dvd)of Mwalimu Julius K Nyerere, dating back to the 1940s, 50s, 60s and 70s. My favourite dvd of Mwalimu is the based on his moving and prophetic speech during his last trip (stop over) to the USA. Get it by all means for the celebration and in honour of Mwalimu's memory.

    II.
    Call 914-941-7636 ext. 2219 (press room), ext.2500 (archives) or send your requests to mkweb@maryknoll.org and ask for any greet speeches (on videos/dvd) of Mwalimu at Butiama, Nyegezi (Musoma)and Maryknoll (NY).

    II.
    Uikose kwenda kenye maktaba ya United Nations hupo jijini Nuyoka (NY). It holds three of his greet speeches.

    III.
    Usisahau au kukosa kuwasiliani na nduguzetu walioko hapo ubalozini, mjini Washington DC. They maybe able to help in many ways than one.

    Go Orange!!!!

    From a fellow 'Orange Man' class of 95.

    ReplyDelete
  10. wewe mdau wa 05:52:00, degree yako ni ya nini?unataka watu wote wasome the same degree?mimi sipendi watu wanaojidai na kukatisha wengine tamaa!
    mdau mpenda haki.

    ReplyDelete
  11. Fanya kuwasiliana na Mwana Historia Mohammed Said, muulize kaka Michuzi atakupa namba yake ya simu na hata email ana picha na maandiko mengi ya kumbukumbu kuhusu Mwalimu ni vyema tukamuongelea Bwana Nyerere kwa Mtazamo wa Kihistoria zaidi

    ReplyDelete
  12. We unayesoma kwamba jamaa anasoma degree mbaya hivi unajua unachikiongea??hakuna degree mbaya ila ishu ni we mwenyewe unaweza kufanya nini na degree yako...Mkuu kaza buti ingawa sikujui ila am very proud of you kama mbongo mwenzangu..naamini wadau wengi wamekupa mwanga wa kutosha...tuwakilishe mzee...kila la kheri..

    ReplyDelete
  13. Wadau wanaosema anasoma digrii mbaya hawajui wasemalo. Hongera sana mzalendo kwa kwenda kuongeza kisomo, tena kwenye chuo chenye heshima yake ndani ya Marekani.

    ReplyDelete
  14. acha kutufunga kamba zako wewe,eti jimbo lote la NY watasherekea siku hiyo,nani anamjua nyerere huku kama sio wewe tuu na wenzako toka bongo?kwanza FYI Nyerere huku anaonekana kama alikuwa dikteta tuu na hata alipokufa kuna vichwa vya magazeti vilimwita a longtime dictator...

    ReplyDelete
  15. Tatizo baadhi ya watu vichwa vyenu vimeoshwa na propaganda za kimagharibi kama vile batiki lililomwagiwa dawa ya kuondelea madoa wakati batiki lenyewe ni kitambaa kilichowekwa madoa. Kwa hiyo CNN propagandists wakimwita Nyerere dikteta, wakati hao hao walimwita Mobutu 'Comrade' wewe unawasikiliza na kuwatumia kama nguzo yako ya kujengea hoja? Utachekwa! Ni chuo gani kingine kwa NY wana tukio kama hilo?
    Sikiliza 'vichwa' vya wanazuoni visivyo na bias vinasema nini. Mwacheni mdau afanye kazi yake bwana, dogo endelea na maandalizi achana na watoto wa mafisadi hao!

    ReplyDelete
  16. Very much impressed, please get hold of Prof Horrace Campbel .. (he is there in Campus) I am sure he has a lot to contribute in this regard. (dRU)

    ReplyDelete
  17. NAKUSHUKURUNI SANA WADAU KWA MICHANGO YENU, KWANI IMENISAIDIA KWA KIASI KIKUBWA NA MWITKIO WA WADAU HAPA CHUONI UMEKUA MKUBWA. HII IMENIPA MOYO NA KUJIONA NI BALOZI MZURI WA NCHI YANGU HASA KWA KUTHAMINI MAISHA NA MCHANGO WA WALE WALIOIFANYA TANZANIA KUWA KAMA ILIVYO.
    WADAU MLIODHARAU SHAHADA YANGU NAOMBA NIWASEMEHE BURE(BILA MASHARTI) KWANI YAWEZEKANA SANA MNA MAWAZO MGANDO MNAOSUBIRI SHAHADA ZENU ZIWAPE THAMANI BADALA YA NYIE KUZIPA THAMANI HIZO SHAHADA.
    MDAU
    Wilbert Mahenge.
    wmahenge@syr.edu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...