Kaka michuzi, mimi ni Mtanzania nipo Chuo kimoja kinaitwa Syracuse University, kipo NY, tunajiandaa kufanya kumbukizi ya miaka 10 baada ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyrere, J.K. Nadhani hili litakua ni kumbukizi pekee rasmi katika jimbo zima la New York. Hivyo basi naomba msaada wako, moja, katika kupata picha nzuri ya mwalimu kwa ajili ya kutengenezea bango, na pili kama una video yoyote ya hotuba ya mwalim, ikiwa ya kiingereza itakua nzuri zaidi maaha sehemu kubwa ya hadhira yetu ni wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza. NB; Kama itakuwa ngumu kwako kupata basi naomba uniwekee kwenye libeneke huko ili wadau waweze kunisaidia.
Natanguliza shukrani zangu za dhati,
Wilbert Mahenge,Graduate Assistant - The Africa Initiative
Wilbert Mahenge,Graduate Assistant - The Africa Initiative
M.A. Candidate, Pan African Studies '11
Hongereni sana Wilbert kwa kuwa wazalendo wa nchi yenu coz most of Tanzanian youth wakiwa nje ubongo wanautupilia mbali, Just keep it up! Am praying 4 U ili tukio liwe la kihistoria....... All the best!
ReplyDeleteFROM UR YOUNG BRO
STANLEY!
aah papaa mahenge a.k.a mzee wa mboga ya matunda. kumbe bado upo kwa mjaluo obama!safi sana.mzee mawasiliano yamekata baada ya kupoteza mail address si unajua pirika za kusaka shilingi bongo.unaweza kunipata katika hamnazo@gmail.com
ReplyDeletekila la heri katika maandalizi ya tamasha lenu.
wadau wote wa Tabora Boys "old boys" - Hi.
mimi "Mufti Boka"
OMBI lako peleka JAMII FORUM,vichwa vya tanzania viko kwenye hiyo forum.
ReplyDeletenadhani ingekuwa jambo bora ukiwasiliana moja kwa moja na office ya raisi tanzania..
ReplyDeleteAngalia Youtube kuba baadhi ya clip. Vile vile unaweza kutumia online resource ambayo inatolewa na library ya hapo college kwenu. Ukiingia kwenye database za International studies au Politics then search Julius Nyerere. Kuna publications zake nyingi sana. I mean nyingi sana mimi nime collect nyingi sana.
ReplyDeleteKama unaitaji hizi publications then unaweza kunitumia email
Mtanganyika01@yahoo.com
Mchumi wa Texas
Video zipo nyingi katika google.com
ReplyDeletekama ukienda google.com halafu type: Mwalimu Nyerere halafu changua video section zipo kibao.unaweza uka-download. Zipo za kiingereza na kiswahili.
Asante
You can go to google and type
mwalimu nyerere and then select Video on the top of the page and should should lots of videos in Swahili and English.
Ghue ghojo Mahenge, jibidi ovandhekhele avanu avihusika katika amakhitaba
ghataifa. Avanu khatika omutandao ogho navakhawese okhokhopela isideo syakhengelesi. Jaribu okholonda katika e-google.com
siolusu ghue. Andekha tu "mwalimu Nyerere halafu minya search" jibidi odaunilodi.
Khepwamwelelo.
mdau oni lang tu, kanumba au joni mashaka si wote wako malekani na wanaweza kuja kuto mihadhala ya kiingereleza? wanaandikahga maatiko mazuli kwa hiyo watafute. email yake ni jonimashaka2008@yahoo.com na mwenzie ni stevekanumba@gmail.com
ReplyDeleteMshkaji unasoma degree mbovu mno, pole.
ReplyDeleteNd. Mahenge, ukiwa wewe ni mkazi wa Sirakuza katika jimbo kuu la Nuyoka, Marekani, basi, tuma maombi (e-meili) yako kwenye:
ReplyDeleteI.
LIBRARY OF CONGRESS (Washington DC)
African and Middle Eastern Division
Ask a Librarian through e-mail.
There are thousands of great photos and speeches (on video/dvd)of Mwalimu Julius K Nyerere, dating back to the 1940s, 50s, 60s and 70s. My favourite dvd of Mwalimu is the based on his moving and prophetic speech during his last trip (stop over) to the USA. Get it by all means for the celebration and in honour of Mwalimu's memory.
II.
Call 914-941-7636 ext. 2219 (press room), ext.2500 (archives) or send your requests to mkweb@maryknoll.org and ask for any greet speeches (on videos/dvd) of Mwalimu at Butiama, Nyegezi (Musoma)and Maryknoll (NY).
II.
Uikose kwenda kenye maktaba ya United Nations hupo jijini Nuyoka (NY). It holds three of his greet speeches.
III.
Usisahau au kukosa kuwasiliani na nduguzetu walioko hapo ubalozini, mjini Washington DC. They maybe able to help in many ways than one.
Go Orange!!!!
From a fellow 'Orange Man' class of 95.
wewe mdau wa 05:52:00, degree yako ni ya nini?unataka watu wote wasome the same degree?mimi sipendi watu wanaojidai na kukatisha wengine tamaa!
ReplyDeletemdau mpenda haki.
Fanya kuwasiliana na Mwana Historia Mohammed Said, muulize kaka Michuzi atakupa namba yake ya simu na hata email ana picha na maandiko mengi ya kumbukumbu kuhusu Mwalimu ni vyema tukamuongelea Bwana Nyerere kwa Mtazamo wa Kihistoria zaidi
ReplyDeleteWe unayesoma kwamba jamaa anasoma degree mbaya hivi unajua unachikiongea??hakuna degree mbaya ila ishu ni we mwenyewe unaweza kufanya nini na degree yako...Mkuu kaza buti ingawa sikujui ila am very proud of you kama mbongo mwenzangu..naamini wadau wengi wamekupa mwanga wa kutosha...tuwakilishe mzee...kila la kheri..
ReplyDeleteWadau wanaosema anasoma digrii mbaya hawajui wasemalo. Hongera sana mzalendo kwa kwenda kuongeza kisomo, tena kwenye chuo chenye heshima yake ndani ya Marekani.
ReplyDeleteacha kutufunga kamba zako wewe,eti jimbo lote la NY watasherekea siku hiyo,nani anamjua nyerere huku kama sio wewe tuu na wenzako toka bongo?kwanza FYI Nyerere huku anaonekana kama alikuwa dikteta tuu na hata alipokufa kuna vichwa vya magazeti vilimwita a longtime dictator...
ReplyDeleteTatizo baadhi ya watu vichwa vyenu vimeoshwa na propaganda za kimagharibi kama vile batiki lililomwagiwa dawa ya kuondelea madoa wakati batiki lenyewe ni kitambaa kilichowekwa madoa. Kwa hiyo CNN propagandists wakimwita Nyerere dikteta, wakati hao hao walimwita Mobutu 'Comrade' wewe unawasikiliza na kuwatumia kama nguzo yako ya kujengea hoja? Utachekwa! Ni chuo gani kingine kwa NY wana tukio kama hilo?
ReplyDeleteSikiliza 'vichwa' vya wanazuoni visivyo na bias vinasema nini. Mwacheni mdau afanye kazi yake bwana, dogo endelea na maandalizi achana na watoto wa mafisadi hao!
Very much impressed, please get hold of Prof Horrace Campbel .. (he is there in Campus) I am sure he has a lot to contribute in this regard. (dRU)
ReplyDeleteNAKUSHUKURUNI SANA WADAU KWA MICHANGO YENU, KWANI IMENISAIDIA KWA KIASI KIKUBWA NA MWITKIO WA WADAU HAPA CHUONI UMEKUA MKUBWA. HII IMENIPA MOYO NA KUJIONA NI BALOZI MZURI WA NCHI YANGU HASA KWA KUTHAMINI MAISHA NA MCHANGO WA WALE WALIOIFANYA TANZANIA KUWA KAMA ILIVYO.
ReplyDeleteWADAU MLIODHARAU SHAHADA YANGU NAOMBA NIWASEMEHE BURE(BILA MASHARTI) KWANI YAWEZEKANA SANA MNA MAWAZO MGANDO MNAOSUBIRI SHAHADA ZENU ZIWAPE THAMANI BADALA YA NYIE KUZIPA THAMANI HIZO SHAHADA.
MDAU
Wilbert Mahenge.
wmahenge@syr.edu