Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare (wa pili kushoto) zilizopatikana kupitia kampeni ya Vodafone Red Alert kwa ajili ya maafa yaliyotokea Same na Kilosa. Hafla hiyo ilifanyika katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kutoka Clouds FM.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akizungumza katika nhafla hiyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare Mwamvita Makamba (kulia) wa Vodacom Foundation.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare ( kushoto) akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa CloudsFm Joseph Kusaga cheti cha kutambua mchango wao wa kampeni ya Vodafone Red Alert kwa ajili ya maafa yaliyotokea Same na Kilosa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare mara baada ya kupokea msaada wa hundi yenye thamani ya shs milioni 50 zilizopatikana kupitia kampeni ya Vodafone Red Alert kwa ajili ya maafa yaliyotokea Same na Kilosa. Hafla hiyo ilifanyika katika makazi ya waziri Pinda, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Nector Foya (kushoto) na Mwamvita Makamba (kulia) wa Vodacom.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare mara baada ya kupokea msaada wa hundi yenye thamani ya shs milioni 50 na misaada mingine ya kibinadamu vilivyopatikana kupitia kampeni ya Vodafone Red Alert kwa ajili ya maafa yaliyotokea Same na Kilosa. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba.

Baadhi ya magari ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom yakiwa yameegeshwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu yakiwa yamebeba bidhaa mbalimbali za kibinadamu zilizotolewa msaada na wananchi kwa ajili ya maafa yaliyotokea same na Kilosa
Wafanyakazi wa Vodacom waliohusika katika kampeni hiyo walihudhuria pia

--------------------------
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki ilimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda hundi ya Milioni 50/- zilizokusanywa na kampeni ya kusaidia jamii ya kampuni hiyo ‘Vodafone Red Alert’ ambazo zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini.

Vodacom ilizindua kampeni hiyo inayoendeshwa takribani nchi 27 za Afrika baada ya kuguswa na maafa kutokana na mafuriko yaliyowakumba wakazi wa maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kilosa, Same, Arusha, Mtwara, Ngerengere na kusababisha vifo na uharibifu wa mali zikiwemo nyumba.

Akipokea hundi hiyo Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa atahakikisha msaada huo unatumika kwa lengo lililokusudiwa kwani watu wengi wameathirika na maafa hayo ya mafuriko na kwamba Kilosa peke yake watu 28,000 wameathirika.

Hata hivyo aliishukuru kampeni hiyo ya Vodafone Red Alert iliyoendeshwa na Vodacom Tanzania wakishirikiana na CloudsFm, asasi za kiraia na taasisi za kidini kwa kujitokeza kuwachangia waathirika na kutumia fursa hiyo kuzitaka kampuni zingine kujitokeza kuunga mkono mpango huo.

“Naishukuru kampuni ya Vodacom na Watanzania wote waliojitokeza kuchangia, na kwamba kampuni zingine ziige mfano huu utakaowezesha kuzisaidia jamii zilizoathirika na mafuriko kote nchini kwani misaada bado inahitajika,” alisema Pinda.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare alisema kampuni yake kupitia kampeni ya Vodacom Red Alert itaendelea kuisaidia jamii ya Watanzania pale yatakapojitokeza maafa mengine kote nchini.

Aidha alisisitiza kuwa bila ya ushirikiano wa wateja wapatao milioni saba wa Vodacom Tanzania zoezi hili lisingefanikiwa. Hivyo aliwashukuru wateja wa Vodacom na wananchi wengine waliojitokeza kuchangia misaada mbalimbali na kuitikia wito wa kampuni hiyo uliokuwa na lengo la kuwasaidia Watanzania wenzao.

“Baadhi ya wananchi walijitokeza kuchangia misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo magodoro, nguo, sabuni na bidhaa nyinginezo. Lakini kubwa zaidi nawapongeza wateja wa Vodacom kwa kuchangia kiasi hicho cha milioni 50/-,” alisema Mare.

Kampeni hiyo ya Vodafone Red Alert iliyozinduliwa Januari 24 ilikamilika Februari 1. Ili kuwachangia wahanga, wateja wa Vodacom walipaswa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA au REDALERT kwenda namba 15599, kila ujumbe ulikuwa ukigharimu 250/- pamoja na VAT.

Akizindua kampeni hiyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Vodacom Tanzania, alisema kampeni hiyo ilikuwa ni muhimu katika kuyarejesha kwenye hali ya kawaida maisha ya Watanzania walioathiriwa na maafa katika sehemu mbalimbali nchini.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hayo mapikapu isinyeshe mvua tu!

    ReplyDelete
  2. picha ya pili "Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati)" hahaha mbona simuoni!

    ReplyDelete
  3. kwa nini hakujakuwa na independent company ambayo itashuhurika na maswala yote ya misaada na serikali ikaoversee tu? tunajua serikali yetu ilivyokuwa slow na complication nyingi, wadau tunaanza kuwa na doubt kama hiyo misaada itawafikia walengwa bila mizengwe na kwa muda muafaka. hapa simaanishi kwamba napinga waziri Pinda hapana ili watendaji wake wa chini ndio watamlet down. otherwise waziri mkuu Pinda nakuaminia nafikiri wewe ni kati ya viongoze wakweli na watendaji Tanzania, keep up the good job.

    ReplyDelete
  4. Naomba Nitoe maoni yangu ambayo wengi hawatayapenda lakini ni ukweli. Mkullo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kilosa aliwaingiza mkenge viongozi wa upatu wa DECI na kisha akawaruka kimanga. Serikali imewafunga viongozi hawa wa Dini na kuwapiga wafuasi wao kuzuia mikutano n.k Sasa naomba nikuulize hivi unafikiri mafuriko ya kilosa yametokana na nini? Kuwaonea watu wa Mungu sio mchezo!!!!

    ReplyDelete
  5. Mbona mchango wetu hatukupewa shahada ya utambulisho. Au siye haikuwa nyingi kama hii. Au siye tuwaombe Red Cross cheti cha utambulisho.

    ReplyDelete
  6. Al Muhim uzima wangu umemweka bas! tosha

    lakini as time goes by Im getting annoyed na hii kazi yake inayomfanya awe kwenye public kila kukicha na kama unavyojua tena sie wanaume wa Kiswahili wake zetu ni kama lulu...ninachokisema hapa ni kuwa she is too visible na hii inanipa wasi wasi

    Habibty alitakiwa akae ofsini tuuu

    anyway nampa hongera kwa kazi nzui alofanya lakini i will have HEART to HEART naye kuhusu hii visibility! mafisi yamejaa tele!! na hilolantatiza sana miye....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...