--------------------------
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki ilimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda hundi ya Milioni 50/- zilizokusanywa na kampeni ya kusaidia jamii ya kampuni hiyo ‘Vodafone Red Alert’ ambazo zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini.
Vodacom ilizindua kampeni hiyo inayoendeshwa takribani nchi 27 za Afrika baada ya kuguswa na maafa kutokana na mafuriko yaliyowakumba wakazi wa maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kilosa, Same, Arusha, Mtwara, Ngerengere na kusababisha vifo na uharibifu wa mali zikiwemo nyumba.
Akipokea hundi hiyo Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa atahakikisha msaada huo unatumika kwa lengo lililokusudiwa kwani watu wengi wameathirika na maafa hayo ya mafuriko na kwamba Kilosa peke yake watu 28,000 wameathirika.
Hata hivyo aliishukuru kampeni hiyo ya Vodafone Red Alert iliyoendeshwa na Vodacom Tanzania wakishirikiana na CloudsFm, asasi za kiraia na taasisi za kidini kwa kujitokeza kuwachangia waathirika na kutumia fursa hiyo kuzitaka kampuni zingine kujitokeza kuunga mkono mpango huo.
“Naishukuru kampuni ya Vodacom na Watanzania wote waliojitokeza kuchangia, na kwamba kampuni zingine ziige mfano huu utakaowezesha kuzisaidia jamii zilizoathirika na mafuriko kote nchini kwani misaada bado inahitajika,” alisema Pinda.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare alisema kampuni yake kupitia kampeni ya Vodacom Red Alert itaendelea kuisaidia jamii ya Watanzania pale yatakapojitokeza maafa mengine kote nchini.
Aidha alisisitiza kuwa bila ya ushirikiano wa wateja wapatao milioni saba wa Vodacom Tanzania zoezi hili lisingefanikiwa. Hivyo aliwashukuru wateja wa Vodacom na wananchi wengine waliojitokeza kuchangia misaada mbalimbali na kuitikia wito wa kampuni hiyo uliokuwa na lengo la kuwasaidia Watanzania wenzao.
“Baadhi ya wananchi walijitokeza kuchangia misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo magodoro, nguo, sabuni na bidhaa nyinginezo. Lakini kubwa zaidi nawapongeza wateja wa Vodacom kwa kuchangia kiasi hicho cha milioni 50/-,” alisema Mare.
Kampeni hiyo ya Vodafone Red Alert iliyozinduliwa Januari 24 ilikamilika Februari 1. Ili kuwachangia wahanga, wateja wa Vodacom walipaswa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA au REDALERT kwenda namba 15599, kila ujumbe ulikuwa ukigharimu 250/- pamoja na VAT.
Akizindua kampeni hiyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Vodacom Tanzania, alisema kampeni hiyo ilikuwa ni muhimu katika kuyarejesha kwenye hali ya kawaida maisha ya Watanzania walioathiriwa na maafa katika sehemu mbalimbali nchini.
Hayo mapikapu isinyeshe mvua tu!
ReplyDeletepicha ya pili "Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati)" hahaha mbona simuoni!
ReplyDeletekwa nini hakujakuwa na independent company ambayo itashuhurika na maswala yote ya misaada na serikali ikaoversee tu? tunajua serikali yetu ilivyokuwa slow na complication nyingi, wadau tunaanza kuwa na doubt kama hiyo misaada itawafikia walengwa bila mizengwe na kwa muda muafaka. hapa simaanishi kwamba napinga waziri Pinda hapana ili watendaji wake wa chini ndio watamlet down. otherwise waziri mkuu Pinda nakuaminia nafikiri wewe ni kati ya viongoze wakweli na watendaji Tanzania, keep up the good job.
ReplyDeleteNaomba Nitoe maoni yangu ambayo wengi hawatayapenda lakini ni ukweli. Mkullo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kilosa aliwaingiza mkenge viongozi wa upatu wa DECI na kisha akawaruka kimanga. Serikali imewafunga viongozi hawa wa Dini na kuwapiga wafuasi wao kuzuia mikutano n.k Sasa naomba nikuulize hivi unafikiri mafuriko ya kilosa yametokana na nini? Kuwaonea watu wa Mungu sio mchezo!!!!
ReplyDeleteMbona mchango wetu hatukupewa shahada ya utambulisho. Au siye haikuwa nyingi kama hii. Au siye tuwaombe Red Cross cheti cha utambulisho.
ReplyDeleteAl Muhim uzima wangu umemweka bas! tosha
ReplyDeletelakini as time goes by Im getting annoyed na hii kazi yake inayomfanya awe kwenye public kila kukicha na kama unavyojua tena sie wanaume wa Kiswahili wake zetu ni kama lulu...ninachokisema hapa ni kuwa she is too visible na hii inanipa wasi wasi
Habibty alitakiwa akae ofsini tuuu
anyway nampa hongera kwa kazi nzui alofanya lakini i will have HEART to HEART naye kuhusu hii visibility! mafisi yamejaa tele!! na hilolantatiza sana miye....