Ankal Asalaam Aleikhum,
Tumsifu Yesu Kristo,
Bwana Asifiwe Sana....
Samahani na pole ama hongera kwa vekesheni huko Ukwerewe. Najua utakua usharudi. Kama Bado nisalimie wadau wa Diaspora. Waambie wanamiss mambo huku home. Wasilaze damu.
Ankal shida yangu mie ni moja tu. Shemejio sijui kafurahi nini ila leo kaamka na kusema anataka kunipa zawadi ya Pasaka. Kaniwekea simu hizo mezani nichague moja iwe ndio zawadi yenyewe. Mie nimechanganyikiwa sijui nichague ipi. Naomba wadau wanisaidie na kunipa sababu ya uzuri ya watayoshauri niichague.
Ya kwanza kushoto ni iPhone ya S series yenye 16Gb na kava nyeupe. ya pili ni blackberry, ya tatu ni Blackberry Kitochi na ya nne ni Nokia N79. Naomba wadau msaada tutani hapo....
Mdau wa Mwananyamala A

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. ushauri wangu ,naomba uutilie maanani, chagua Blackberry Kitochi kwani itakusaidia sana pindi umeme utakapokatika huko mwananyamala,angalau kutafutia kiberiti na kibatari.
    cheers!
    mdau
    tokyo

    ReplyDelete
  2. Hizo simu zote bomu,
    Kuanzia kushoto kwenda kulia;
    (1) I Phone ya China, itakufa baada ya mwezi mmoja
    (2) Haina sauti wala vibration- Utamiss simu nyingi sana
    (3) na (4) Zimeiripotiwa zimepotea Utakamatwa
    Anyway chagua yeyote.

    ReplyDelete
  3. Chukua kitochi kaka. Usiku unapokuwa umelala yaweza kukusaidia kumulika mulika kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo.

    ReplyDelete
  4. Jielimishe mwenyewe, tafuta hizo simu kwenye mtandao ili ujue.

    ReplyDelete
  5. Miye nakushauri tu hiyo Blackberry ya pili kushoto usichukue...imechoka na imechubuka...kama anataka kukuzawadi kweli akununulie mpya.

    Matelefoni.

    ReplyDelete
  6. CHUKUA BLACK BERRY KITOCHI NDIO ITAKAYO KUFAA, AU KAMA HUJAIPENDA MWAMBIE AKAKUNUNULIE ZILE SIMU ZA ELFU KUMI NA TANO MPAKA ELFU 20,000 KARIAKOO. INAONEKANA NDIO ZITAKUFAA SANA.

    ReplyDelete
  7. Duh! umenipa wakati mgumu sana,lakini kwa haraka haraka ukiangalia unapoishi, hiyo location ninge kushauri utumie simu ya kichina double line,hizo i phone hazikufai utakabwa.

    ReplyDelete
  8. Kwa msaada tu ndugu yangu naomba uchague kitochi,sababu m'nyamala na iphone au bberry ni utata!

    ReplyDelete
  9. ChakubangaApril 03, 2010

    My advise; it all depend on what you want from the mobile phone because these days mobile phone is more that just receiving and making phone calls, If you are after music,video and other multimedia functions then go for iphone,although iphone has many functions than any other known mobile phone but many of those functions will not be available in Tanzania. If you are after e-mail, texting and internet then you will be better off with blackberry, blackberry is also more durable than iphone. My last advise is make sure whichever you are choosing make sure is genuine and not fake one, there are alot of substandard fake mobile phone hand set be aware.

    ReplyDelete
  10. Kaka ni kweli shemeji kakuletea uchague hizo? au yule jamaa maarufu kwa kabari za mbao na misumari?
    Hata hivyo chagua kitochi kitakusaidia na mgao wetu wa umeme usiku !

    ReplyDelete
  11. Because it is our constitutional right to stay in darkness 5 hours out of 24,I advise you to pick the flash-light one

    ReplyDelete
  12. Wewe Bahau mkubwa. Mwambie aliyekununulia siku nyingine akununulie simu moja tu. Usitupotezee muda. Kwanza zote zimechubuka.

    Mzee Tembo Mpopo,
    Makorola Tanga
    (Karibu na Kwa Njeka)

    ReplyDelete
  13. without a dought nokia N79

    ReplyDelete
  14. simu zote hizo za wizi. aliyekuletea ni kibaka mkabaji wa roba za mbao.

    ReplyDelete
  15. Chakubanga: Tunaomba utusadie sie tusiojua kimbombo kwa kutusaidia kutafsiri ulichochangia. Maana aliyeomba ushauri ameomba kwa kiswahili lakini we' kwa usomi wako, umeamua kumjibu kwa kimombo. Tusaidie maana sie tumetoka kapa.

    NGUMBARU

    ReplyDelete
  16. watu wengine bwana! yani hata kuchagua simu unaomba ushauri? tuache uzembe jamani; dunia ya leo lazima ufunuke macho, wewe wa wapi jamani? au wa chanika wewe? mdau toka bujumbura

    ReplyDelete
  17. ya tochi itakusaidia kumulika maeneo fulani fulani ucku.

    ReplyDelete
  18. ahhaha! kwanza nianze kwa kucheka! yaani nikweli kama mdau mmoja hapo juu aliyesema hata simu tu kuchagua inakuwa tabu? yaani umeona humu ndani unaweza kupata msaada?
    anyway sawa msaada tutakupa.... hiyo bberry ya tochi itakufaa kutokana na mgao na pia hata ukipigwa roba mitaani haitakuwa uchungu sana kwani ni bei poa! so kazi kwako!

    ReplyDelete
  19. we umechoka kwelii tukupe ushauri wa kuchagua simu tuite tukuchaguliee mke basi

    ReplyDelete
  20. SIMU YA NINI WEWE, KAMA ULIKUA HUNA MWANZO SIDHANI KAMA UNAITAJI HATA MOJA, UNAJIONGEZEA BILI NA MATATIZO YA BURE TU, LABDA HUYO MKEO ANATAKA AWE ANAKUCHEKI UKO WAPI SAA ZOTE, KAMA UKO TAYARI BASI CHAGUA MWENYEWE INAYOKUVUTIA, MBONA ZOTE ZIMECHOKA LAKINI, KAMA ANAKUPENDA KIASI HICHO ANGEKUPA VITU TU KILA SIKU USIKU,BASI KULIKO SECOND HAND HANDSET, NUNUA YAKO UEPUKE MATATIZO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...