Tumsifu Yesu Kristo,
Bwana Asifiwe Sana....
Samahani na pole ama hongera kwa vekesheni huko Ukwerewe. Najua utakua usharudi. Kama Bado nisalimie wadau wa Diaspora. Waambie wanamiss mambo huku home. Wasilaze damu.
Ankal shida yangu mie ni moja tu. Shemejio sijui kafurahi nini ila leo kaamka na kusema anataka kunipa zawadi ya Pasaka. Kaniwekea simu hizo mezani nichague moja iwe ndio zawadi yenyewe. Mie nimechanganyikiwa sijui nichague ipi. Naomba wadau wanisaidie na kunipa sababu ya uzuri ya watayoshauri niichague.
Ya kwanza kushoto ni iPhone ya S series yenye 16Gb na kava nyeupe. ya pili ni blackberry, ya tatu ni Blackberry Kitochi na ya nne ni Nokia N79. Naomba wadau msaada tutani hapo....
Mdau wa Mwananyamala A
ushauri wangu ,naomba uutilie maanani, chagua Blackberry Kitochi kwani itakusaidia sana pindi umeme utakapokatika huko mwananyamala,angalau kutafutia kiberiti na kibatari.
ReplyDeletecheers!
mdau
tokyo
Hizo simu zote bomu,
ReplyDeleteKuanzia kushoto kwenda kulia;
(1) I Phone ya China, itakufa baada ya mwezi mmoja
(2) Haina sauti wala vibration- Utamiss simu nyingi sana
(3) na (4) Zimeiripotiwa zimepotea Utakamatwa
Anyway chagua yeyote.
Chukua kitochi kaka. Usiku unapokuwa umelala yaweza kukusaidia kumulika mulika kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo.
ReplyDeleteJielimishe mwenyewe, tafuta hizo simu kwenye mtandao ili ujue.
ReplyDeleteMiye nakushauri tu hiyo Blackberry ya pili kushoto usichukue...imechoka na imechubuka...kama anataka kukuzawadi kweli akununulie mpya.
ReplyDeleteMatelefoni.
CHUKUA BLACK BERRY KITOCHI NDIO ITAKAYO KUFAA, AU KAMA HUJAIPENDA MWAMBIE AKAKUNUNULIE ZILE SIMU ZA ELFU KUMI NA TANO MPAKA ELFU 20,000 KARIAKOO. INAONEKANA NDIO ZITAKUFAA SANA.
ReplyDeleteDuh! umenipa wakati mgumu sana,lakini kwa haraka haraka ukiangalia unapoishi, hiyo location ninge kushauri utumie simu ya kichina double line,hizo i phone hazikufai utakabwa.
ReplyDeleteKwa msaada tu ndugu yangu naomba uchague kitochi,sababu m'nyamala na iphone au bberry ni utata!
ReplyDeleteMy advise; it all depend on what you want from the mobile phone because these days mobile phone is more that just receiving and making phone calls, If you are after music,video and other multimedia functions then go for iphone,although iphone has many functions than any other known mobile phone but many of those functions will not be available in Tanzania. If you are after e-mail, texting and internet then you will be better off with blackberry, blackberry is also more durable than iphone. My last advise is make sure whichever you are choosing make sure is genuine and not fake one, there are alot of substandard fake mobile phone hand set be aware.
ReplyDeleteKaka ni kweli shemeji kakuletea uchague hizo? au yule jamaa maarufu kwa kabari za mbao na misumari?
ReplyDeleteHata hivyo chagua kitochi kitakusaidia na mgao wetu wa umeme usiku !
Because it is our constitutional right to stay in darkness 5 hours out of 24,I advise you to pick the flash-light one
ReplyDeleteWewe Bahau mkubwa. Mwambie aliyekununulia siku nyingine akununulie simu moja tu. Usitupotezee muda. Kwanza zote zimechubuka.
ReplyDeleteMzee Tembo Mpopo,
Makorola Tanga
(Karibu na Kwa Njeka)
without a dought nokia N79
ReplyDeletesimu zote hizo za wizi. aliyekuletea ni kibaka mkabaji wa roba za mbao.
ReplyDeleteChakubanga: Tunaomba utusadie sie tusiojua kimbombo kwa kutusaidia kutafsiri ulichochangia. Maana aliyeomba ushauri ameomba kwa kiswahili lakini we' kwa usomi wako, umeamua kumjibu kwa kimombo. Tusaidie maana sie tumetoka kapa.
ReplyDeleteNGUMBARU
watu wengine bwana! yani hata kuchagua simu unaomba ushauri? tuache uzembe jamani; dunia ya leo lazima ufunuke macho, wewe wa wapi jamani? au wa chanika wewe? mdau toka bujumbura
ReplyDeleteya tochi itakusaidia kumulika maeneo fulani fulani ucku.
ReplyDeleteahhaha! kwanza nianze kwa kucheka! yaani nikweli kama mdau mmoja hapo juu aliyesema hata simu tu kuchagua inakuwa tabu? yaani umeona humu ndani unaweza kupata msaada?
ReplyDeleteanyway sawa msaada tutakupa.... hiyo bberry ya tochi itakufaa kutokana na mgao na pia hata ukipigwa roba mitaani haitakuwa uchungu sana kwani ni bei poa! so kazi kwako!
we umechoka kwelii tukupe ushauri wa kuchagua simu tuite tukuchaguliee mke basi
ReplyDeleteSIMU YA NINI WEWE, KAMA ULIKUA HUNA MWANZO SIDHANI KAMA UNAITAJI HATA MOJA, UNAJIONGEZEA BILI NA MATATIZO YA BURE TU, LABDA HUYO MKEO ANATAKA AWE ANAKUCHEKI UKO WAPI SAA ZOTE, KAMA UKO TAYARI BASI CHAGUA MWENYEWE INAYOKUVUTIA, MBONA ZOTE ZIMECHOKA LAKINI, KAMA ANAKUPENDA KIASI HICHO ANGEKUPA VITU TU KILA SIKU USIKU,BASI KULIKO SECOND HAND HANDSET, NUNUA YAKO UEPUKE MATATIZO.
ReplyDelete