Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalumu cha Halmashauri kuu ya taifa CCM kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma.
Dr.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Dr.Ali Mohamed Mohamed shei kuchaguliwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM wakiwa katika kikao maalum kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma

HATIMAYE MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. ALLY MOHAMED SHEIN AMEIBUKA KIDEDEA KWA KURA 117 NA KUWABWAGA WAPIZANIA WAKE DR. GHALIB BILAL NA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA KATIKA KINYAG'ANYIRO CHA KUWANIA KUGOMBEA URAIS KISIWANI ZANZIBAR.

DR.SHEIN ALIWASHINDA GHALIB BILAL AMBAYE AMEPATA 54 NA KUSHIKA NAFASI PILI AKIFUATIWA NA SHAMSI VUAI NAHODHA AMBAYE AMESHIKA NAFASI YA TATU KWA KUPATA KURA 33 HABARI NDO HIYO WADAU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2010

    Huyu ndie anaetufaa Wazanzibari, hana makuu, hana majungu, hana makundi, si mtu anaefikiria visasi, anapenda kudumisha umoja

    Ee!!!! Mwenyezi Mungu mpe uzima, ili tutumie busara zake.

    Hongera brother.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2010

    Hiyo ndiyo Dodoma bwana. Mambo yote yangefanyika Zanzibar tungeweza kupata matokeo tofauti lakini Dodoma? Wewe ungetegemea nini zaidi ya Sheni?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2010

    HIVI KATIKA WAJUMBE WALIOPIGA KURA KWENYE HUO MKUTANO NI WANGAPI WAMETOKA ZANZIBAR?

    ZANZIBAR ISIWE IKAWA INACHAGULIWA MGOMBEA WA URAIS NA WATU WA BARA AMBAO WENGINE HAWAJAWAHI HATA KUFIKA ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2010

    GHALIB BILAL KWAKE NDIYO IMETOKA HIVYO, HANA LAKE TENA KWENYE URAIS WA ZANZIBAR. KAMA KWELI ANATAKA KUWA RAIS NA ANAKUBALIKA SANA HUKO ZANZIBAR BASI AGOMBEE KUPITIA CHAMA CHA UPINZANI KWANI WAKUBWA WA CCM HAWAMTAKI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2010

    SASA KIKWETE ATAMCHAGUA NANI KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2010

    KWA MTINDO HUU WA KUCHAGUA MGOMBEA KWENYE MKUTANO WENYE WAJUMBE WENGI WA BARA BASI HATA RAIS WA MUUNGANO HAWEZI KUTOKA ZANZIBAR NDANI YA CCM KWANI MTANDAO MKUBWA UKO BARA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2010

    SHENI ALISHAWEKA MTANDAO WAKE HUKU BARA AMBAKO KUNA WAJUMBE WENGI WA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM. HIVYO WENGI WALITEGEMEA ANGESHINDA TU KIRAHISI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2010

    HIYO NIMEIPENDA SANA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.KIDUMUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2010

    Sasa akapambane na Malim Seif, wote wapemba hawa. Karata mzuri ya CCM kwenye kura za wapemba hiyo, kwani kama ni sahihi atakuwa mgombea wa kwanza wa urais wa Zanzibar kutoka Pemba. Hivyo kuna uwezekano mkubwa wapemba wakaipigia CCM kura za urais safari hii.

    Seif na CUF kazi ipo hapo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2010

    Hakuna ambaye hakujua nini kitatokea. Hata wagombea wenzake walijua!
    Well. Shein anadeserve

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2010

    Ahsante kwa habari ila sijafurahishwa na matokeo hta kidogo ukisikia mapinduzi ya siasa yanakuja zenji ndio hayo. CUF watashinda tu km kawaida yao kubwa zaid kwa ushindi wa kishindo tna mara hii watashinda kwa kishindo zaid na hawatonyang'anywa serikali. Mungu ibariki zenji na tz kwa ujumla

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2010

    WIZI MTUPU HAYA WANGEFANYIA ZNZ wananchi wa ZNZ ndio waamuwe DR BILAL ndio wanaomtaka.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 10, 2010

    kipekee nimefurahi sana, pia ninauzuni..kwa sababu nilikuwa nataka agombee uraisi wa muungano 2015..lakini si inawezekani kuongaza Zanzibar kwa kipindi kimoja na kurudi muungano kuongoza serikali baada ya Jk
    Ninamuombea Mungu andelee kumlinda
    there is doubt this is right leader we have in hand tunatakiwa kumlinda kwa gharama zozote. hata wakati wa kuongea utamwelewa siyo mzee wa longo longo ni facts and kufanya kazi

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2010

    Hongera sana Dr. Shein kwa kuibuka kidedea,hiyo ndio demokrasia.Ila basi nina wasi2 na Dr Bilal kama kweli atalidhia kushindwa kwake maanakwa asilimia 100 alikuwa anjua kuwa ni yeye,lakini kumbe Shein ndie aliyeshinda.Basi ningemwomba Dr Bilal akukabali matokeo hayo,hakuna haja ya kuanzisha mjadala wa mara sikutendewa haki,hiyo ndio haswa demokrasia was asilete fujo watu wa Usalama tutamdhibiti bila tatizo lolote,akukubali na huo ndio uwe mwisho wake wa kugombea tena Urais wa Visiwani kwani umri umemtupa mkono.
    Hongera sana Shein,mie nilijua tu kuwa utakuwa wewe.Hili mwaka 2015 uje na uraisi Tz.Kubali yamekishwa mambo ndio yalivyo.
    mdau Wa Ipinda Lusungo Kyela

    ReplyDelete
  15. I am also coming to vie for an office in TZ as long as I denounce my kenyan citizeship

    Mujomba Paulo Kamau
    Nakuru-Kenya

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2010

    @ Paulo, kwani mbona usigombee kwa Mungiki? au wewe ni Gikuyu fake?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 10, 2010

    Uncle Kamau do u see us guys they way we practice democracy.. ithink this is a very big lesson lesson to you and ur country men..Us Guys we very far... karbu but dont bring ur Kenyan attitude n tribalistic

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 10, 2010

    Shein for presidency 2015..after JK
    I really admire you so much, u have astand and u work on ur stand.
    Vamos Shein

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 10, 2010

    Na Mgombea mwenza wa JK ni...........................
    Rais Karume, hapo wamekuda deal kuswapu madaraka. Tuwe na subira

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 10, 2010

    Mimi kitu kinachonikera ni kwamba kwa nini raisi wa zanzibar anachaguliwa na majority ya wabara?hapo hakuna demokrasia kwani rais anatakiwa achaguliwe na wananchi anaowaongoza.Hivi leo tuseme kenya ndio watuchagulie raisi tungekubali?Hii ni moja ya tatizo la muungano.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 10, 2010

    HAYA UCHAGUZI NDIO USHAFANYIKA TAYARI NA RAISI KISHAJULIKANA ,MWEZI OCTOBER NI KUMHAKIKISHA TU LAKINI ALOCHAGULIWA KIZOTA NDIO RAISI WA ZANZIBAR HATA AKIPATA KURA MOJA.SEMA HAPA IPOKAZI SHEIN ANA UWEZO WA KUKATAA MATOKEO?(Thierry-handball)

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 10, 2010

    KESHO RAIS KARUME ANATANGAZWA KUWA MGOMBEA MWENZA WA JK, WERA WERAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
    PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 10, 2010

    ijapokuwa mimi ni mtanzania kutoka bara (kwetu kilimanjaro), naamini kuwa huu ni uteuzi mzuri kwa kuwa dr shein ni mwadilifu, mchapakazi, hana majungu, hana vikudi, ni mwaaminifu. tunahitaji viongozi ambao ni watendaji na wasiopenda majungu na conspiracy.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 10, 2010

    BOOOOOOOOOOOOOORING!!!
    YAANI KWA KIFUPI SIASA ZA BONGO ZINABOA! VIONGOZI WANABOA! SIONI HATA KWA NINI KUNA UCHAGUZI,WATU NI WALEWALE, RANGI NI ILE ILE,SERA/STORY NI ZILE ZILE!

    Usinibanie comment yangu.
    Ni mimi Shushushu.uk

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 10, 2010

    Hi,wadau!
    Rangi hiyo iliyo tanda hapo na nyuso zote ndo zimeifanya Tanzania ionekana ilivyo hadi sasa. Msijali tutasonga kwa rushwa,udungu na ushosti.

    Eh MWENYEZI MUNGU NIEPUSHE ZAMBI HIZI.AMINA

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 10, 2010

    Hasabu za haraka haraka:
    Jumla ya kura: 117+54+33=204
    Mikoa:ZNB=5,TZB=21,jumla=26
    Uwiano wa wajumbe:
    Zanzibar=(5/26)*204=39.2 tuchukue40
    Tanzania Bara = 204-40=164
    HITIMISHO
    Rais wa zanzibar anachaguliwa na watu wa bara ndio maana tunaambiwa kwamba ZANZIBAR SI NCHI!!!!!
    Kazi kwenu Wanzanzibari manake kwa stahili hii bado HAMJAWA HURU MSIJIDANGANYE

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 10, 2010

    MUUNDO WA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA NDIO UNAPELEKEA WAJUMBE WA BARA KUWACHAGULIA ZANZIBAR MGOMBEA URAIS.WAZANZIBAR WANAMTAKA BILAL ILI HALI VIONGOZI WA CCM BARA WANAMTAKA SHEIN.KURA 117 DHIDI YA 54 ? HAKUNA USHINDANI HAPO. AU 117 DHIDI YA NAHODHA 33 ? BILAL + NAHODHA = 87.BADO HAWAJAMKARIBIA SHEIN HATA KIDOGO !
    MDAU WA NE,DC.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 10, 2010

    HII SIO HAKI KABISA WAZANZIBARI WANA HAKI YA KUSIKILIZWA WANAMTAKA NANI KUWA RAISI WAO , NA WENGI WANAMTAKA BILALI LAKINI WABARA NDIO WANA NGUVU SHAME !!!NAJUA KUNA WANA CCM WANAWEZA WAGOME KUPIGA KURA MWAKA HUU NA TUTAONA HUYO SHEIN AKISHINDA ATASHINDA WA ASILIMIA NDOGO SANA HII NI HATARI KWANI CUF ITAWEZA KUSHINDA!!!DUUU RAISI MPEMBA MAAJABU HATA KAMA CUF HAITOSHINDA PRACTICALY IMESHINDA

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 10, 2010

    HII SIO HAKI KABISA WAZANZIBARI WANA HAKI YA KUSIKILIZWA WANAMTAKA NANI KUWA RAISI WAO , NA WENGI WANAMTAKA BILALI LAKINI WABARA NDIO WANA NGUVU SHAME !!!NAJUA KUNA WANA CCM WANAWEZA WAGOME KUPIGA KURA MWAKA HUU NA TUTAONA HUYO SHEIN AKISHINDA ATASHINDA WA ASILIMIA NDOGO SANA HII NI HATARI KWANI CUF ITAWEZA KUSHINDA!!!DUUU RAISI MPEMBA MAAJABU HATA KAMA CUF HAITOSHINDA PRACTICALY IMESHINDA

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 11, 2010

    Bila shaka CCM ilikuwa inachagua mgombea wake ktk nafasi ya Uraisi zanzibar na haikuwa inachagua Raisi wa zanzibar, kwa mantiki hiyo wanzazibar hawajachaguliwa Raisi wao na watanganyika maana uchaguzi mkuu wanzazibar ndio watakao piga kula za kuchagua Kiongozi wanaomtaka na siyo Watanganyika, Katika hilo sio nadhalia ya nyie mnao lalama eti wanzabari wanachaguliwa Kiongozi. Ujumbe umefika....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...