Hassan Hamisi Hafidh akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Amani, Zenji ankal akiwa na viongozi wa CCM wa matawi mbalimbali ughabuni katika dina la mchana kwenye mgahawa wa Break Point ya mjini jana. viongozi hao ambao walikuwa Dodoma walikohudhuria mkutano mkuu wa chama kule Kizota, wapo transit Dar kabla ya kupaa kuelekea makwao.
ankal akifurahia jambo wakati wa dina hilo la nguvu la mchana
picha ya pamoja baada ya kujichana. walioketi toka shoto ni makamu mwenyekiti wa CCM tawi la Bangalore Ndg. Baraka Abdallah Kange, akifuatiwa na mwenyekiti wa tawi la Makerere, Uganda, Ndg Albert Theophil, Mwenyekiti wa CCM tawi la Napoli, Italy, Ndg. Abdulrahman A. Ali Kapaga, Mwenyekiti wa CCM tawi la Uingereza Ndg Maina Ang'iela Owini, Katibu Mkuu wa CCM tawi la Uingereza na ankal. waliosimama toka shoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Ndg Hassan Hafidh, Katibu wa Tawi la Napoli, Ndg Kagutta A. Maulidi na viongozi wa juu wa CCM matawi ya Uingereza
Home
Unlabelled
viongozi wa CCM ughaibuni watua dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kweli tanzania tunakatisha tamaa kabisa !! hao wapambe mbona mbombe nyingi!!
ReplyDeleteHassan Hafidh ametumia vizuri kweli hii clip.
ReplyDeleteWana Amani kle Zanzibar mpeni kra za ndio.
Ankal na wewe ccm imekununua kwa dinner ya mchana(kwa bei rahisi) Watanzania tubadilikeni
ReplyDeletetunawasema wamama wa nyumbani na watu wasiokuwa na ajira kuwa wakati wa kampeni huwa wananunuliwa kwa tishet,kofia na kanga za bure toka ccm.
na wewe ankal na wasanii je? kulikoni?
Kofia rangi ya njano na kijani,tai nyekundu,shati light blu....na koti ranhi ya ajabu ajabu du hii sio siri kali yaani unakuwa kama chrismass tree!
ReplyDeletekaazi kweli kweli.Kaka MISUPU tumechoka na habari za CCM kila kukicha ni CCM,CCM,CCM kha au na wewe ni CCM damu nini.ahhaa nimesahamu kumbe kaka MISUPU wewe ni CCM damu.haya kaka kazi njema na hilo libeneke la CCM.
ReplyDeleteMdau-Mji wa Kusoma!!!
mikada mikada mikada yenye njaa inatafuta mlo kupitia ccm lakini kumbukeni cha mtu akiliwi mtakuja kujieleza mbele ya safari pindi kila goti litakapopigwa siku hiyo ikifika nyamafuuuuuu pambafffff
ReplyDeleteankal ibane hii kama kawaida yako na blog lako la wana ccm huna mpango wowote nawewe njaa kali.
of course wenye njaa na wale wote wanaotaka kuficha madhambi yao wanakimbilia ccm, inashangawa watu kwenye misiba wa wazazi wao hawarudi bongo, ila kwenye mkutano ndio wa kwanza ama kweli hii kali ya mwaka.
ReplyDeletewiiiiziiii mtupu eti tumekija tunataka tuwasaidie watanzania waondokane na umaskini mh mnafikiri watanzia wote ni wajinga nyie mnaishi ulaya hamjui shida wanazozipata watanzania leo mtamsaidia mkulima nini mnachekesha rudini mkabebe boksi!! watanzania msidanganywe na watu wachache waliokatiwa benefiti sasa njaa imekuwa kali !!
ReplyDeleteKumbuka ninayo blog yangu binafsi, hivyo ukiendelea kuziweka kapuni michango yangu miwili kuhusu, wasanii na Wana ccm wa ughaibuni kutekwa na CCM. Nitaandika tu, hata ikibidi nitaandika kuhusu blog yako kwenye BBC au VOA. Usiwe biased hii siyo blog ya wana CCM.
ReplyDeleteAsante baraka kange, mkongwe hapa india,unafahamika vizuri mysore,sasa gombea ubunge tufanye kampeni za nguvu.
ReplyDeleteDr. Shayo, Nabii Yohana wako wapi Jama, hawa ndo watu ambao wataleta maendeleo, hawa wengine ni longo longo tu
ReplyDeleteNinawaasa viongozi hao wa CCM ughaibuni waridhike na uongozi wao wa ughaibuni tu. Kamwe wasijifanye kutaka kujiingiza katika uongozi wa CCM wa nyumbani au hata kugombea ubunge kwani CCM wa nyumbani ndiyo hasa wana uchungu halali kutokana na kuwa kwenye ground ya mapambano ya njaa, umasikini, vibaka, ujambazi, wizi, uchawi, malaria, ukimwi n.k. Huu ni mwaka wa sisi tuliopo nyumbani kugombea uongozi wa nyumbani hao wa ughaibuni waendelee na vyeo vyao vya ughaibuni wala hatutowagusa. wakijifanya kugombea ubunge n.k wasishangae wakazahau hata majina ya nchi walizokuwa wanaishi huko ughaibuni. Vinginevyo wajiandae uongozi wa nyumbani hauhitaji CV wala elimu bali ni ugwiji wa kuwajua waganga wa kienyeji wenye uwezo mkubwa wa kumtia kichaa mpinzani wako, kumpiga kipande na hata mkosi mpinzani wako, kama hili hawalijui basi wajiandae kujikutwa wamenyolewa nywele za IKULU kwa kuchupa.
ReplyDeleteHivi wewe Ankal Mithupu, mshombe, stew...kweli una haja ya kupika huko kwako? Inaonyesha kuwa umejenga jina kiasi ambacho unaweza kuishi kwa kuzamia tu minuso....naona wivu kweli...kumbe hako ka-kitambi siyo ka bure maana kila siku ya Mungu unakula kama mgeni...!!
ReplyDeleteMdau-NYC, USA
mmechelewa kidogo tu vinginevyo mngekuwa mnagombea jimbo la ccm ughaibuni.
ReplyDeleteKama ningekuwa mwanasiasa basi ningeakikisha fedha za uchaguzi mwaka huu zinatumika kuboresha huduma za maji na Mashule kwa wananchi wote na uchaguzi uairishwe mpaka miaka mitano inayokuja na kuundwa serikali ya mseto. Je wanasiasa wanawaza kama mimi au watu wengine wanaopenda nchi? Ni nini maana ya uchaguzi wakati nchi nzima inafahamu CCM itashinda? Je ni kiasi gani cha Gharama kitatumika kwenye uchaguzi? Je kiasi hicho hatuwezi kutumia kwa kazi nyingine muhimu kuboresha maisha ya wananchi?
ReplyDeleteMjusi
watu wote tunakuunga mkono ila usisahau kulipa hela ya baku mara upatapo ubunge .... kila la kheri
ReplyDelete