Hassan Hamisi Hafidh akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Amani, Zenji
ankal akiwa na viongozi wa CCM wa matawi mbalimbali ughabuni katika dina la mchana kwenye mgahawa wa Break Point ya mjini jana. viongozi hao ambao walikuwa Dodoma walikohudhuria mkutano mkuu wa chama kule Kizota, wapo transit Dar kabla ya kupaa kuelekea makwao.
ankal akifurahia jambo wakati wa dina hilo la nguvu la mchana
picha ya pamoja baada ya kujichana. walioketi toka shoto ni makamu mwenyekiti wa CCM tawi la Bangalore Ndg. Baraka Abdallah Kange, akifuatiwa na mwenyekiti wa tawi la Makerere, Uganda, Ndg Albert Theophil, Mwenyekiti wa CCM tawi la Napoli, Italy, Ndg. Abdulrahman A. Ali Kapaga, Mwenyekiti wa CCM tawi la Uingereza Ndg Maina Ang'iela Owini, Katibu Mkuu wa CCM tawi la Uingereza na ankal. waliosimama toka shoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Ndg Hassan Hafidh, Katibu wa Tawi la Napoli, Ndg Kagutta A. Maulidi na viongozi wa juu wa CCM matawi ya Uingereza

Katibu Mkuu wa CCM tawi la Uingereza Ndg Suzana Mzee akimpongeza Ndg. Hassan Hamisi Hafidh ambaye katika hafla hii alitangaza nia ya kugombea Ubunge kiti cha Amani, Zenji




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2010

    kweli tanzania tunakatisha tamaa kabisa !! hao wapambe mbona mbombe nyingi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2010

    Hassan Hafidh ametumia vizuri kweli hii clip.

    Wana Amani kle Zanzibar mpeni kra za ndio.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2010

    Ankal na wewe ccm imekununua kwa dinner ya mchana(kwa bei rahisi) Watanzania tubadilikeni

    tunawasema wamama wa nyumbani na watu wasiokuwa na ajira kuwa wakati wa kampeni huwa wananunuliwa kwa tishet,kofia na kanga za bure toka ccm.

    na wewe ankal na wasanii je? kulikoni?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2010

    Kofia rangi ya njano na kijani,tai nyekundu,shati light blu....na koti ranhi ya ajabu ajabu du hii sio siri kali yaani unakuwa kama chrismass tree!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2010

    kaazi kweli kweli.Kaka MISUPU tumechoka na habari za CCM kila kukicha ni CCM,CCM,CCM kha au na wewe ni CCM damu nini.ahhaa nimesahamu kumbe kaka MISUPU wewe ni CCM damu.haya kaka kazi njema na hilo libeneke la CCM.
    Mdau-Mji wa Kusoma!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2010

    mikada mikada mikada yenye njaa inatafuta mlo kupitia ccm lakini kumbukeni cha mtu akiliwi mtakuja kujieleza mbele ya safari pindi kila goti litakapopigwa siku hiyo ikifika nyamafuuuuuu pambafffff

    ankal ibane hii kama kawaida yako na blog lako la wana ccm huna mpango wowote nawewe njaa kali.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2010

    of course wenye njaa na wale wote wanaotaka kuficha madhambi yao wanakimbilia ccm, inashangawa watu kwenye misiba wa wazazi wao hawarudi bongo, ila kwenye mkutano ndio wa kwanza ama kweli hii kali ya mwaka.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2010

    wiiiiziiii mtupu eti tumekija tunataka tuwasaidie watanzania waondokane na umaskini mh mnafikiri watanzia wote ni wajinga nyie mnaishi ulaya hamjui shida wanazozipata watanzania leo mtamsaidia mkulima nini mnachekesha rudini mkabebe boksi!! watanzania msidanganywe na watu wachache waliokatiwa benefiti sasa njaa imekuwa kali !!

    ReplyDelete
  9. Kumbuka ninayo blog yangu binafsi, hivyo ukiendelea kuziweka kapuni michango yangu miwili kuhusu, wasanii na Wana ccm wa ughaibuni kutekwa na CCM. Nitaandika tu, hata ikibidi nitaandika kuhusu blog yako kwenye BBC au VOA. Usiwe biased hii siyo blog ya wana CCM.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2010

    Asante baraka kange, mkongwe hapa india,unafahamika vizuri mysore,sasa gombea ubunge tufanye kampeni za nguvu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2010

    Dr. Shayo, Nabii Yohana wako wapi Jama, hawa ndo watu ambao wataleta maendeleo, hawa wengine ni longo longo tu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2010

    Ninawaasa viongozi hao wa CCM ughaibuni waridhike na uongozi wao wa ughaibuni tu. Kamwe wasijifanye kutaka kujiingiza katika uongozi wa CCM wa nyumbani au hata kugombea ubunge kwani CCM wa nyumbani ndiyo hasa wana uchungu halali kutokana na kuwa kwenye ground ya mapambano ya njaa, umasikini, vibaka, ujambazi, wizi, uchawi, malaria, ukimwi n.k. Huu ni mwaka wa sisi tuliopo nyumbani kugombea uongozi wa nyumbani hao wa ughaibuni waendelee na vyeo vyao vya ughaibuni wala hatutowagusa. wakijifanya kugombea ubunge n.k wasishangae wakazahau hata majina ya nchi walizokuwa wanaishi huko ughaibuni. Vinginevyo wajiandae uongozi wa nyumbani hauhitaji CV wala elimu bali ni ugwiji wa kuwajua waganga wa kienyeji wenye uwezo mkubwa wa kumtia kichaa mpinzani wako, kumpiga kipande na hata mkosi mpinzani wako, kama hili hawalijui basi wajiandae kujikutwa wamenyolewa nywele za IKULU kwa kuchupa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 14, 2010

    Hivi wewe Ankal Mithupu, mshombe, stew...kweli una haja ya kupika huko kwako? Inaonyesha kuwa umejenga jina kiasi ambacho unaweza kuishi kwa kuzamia tu minuso....naona wivu kweli...kumbe hako ka-kitambi siyo ka bure maana kila siku ya Mungu unakula kama mgeni...!!
    Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2010

    mmechelewa kidogo tu vinginevyo mngekuwa mnagombea jimbo la ccm ughaibuni.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2010

    Kama ningekuwa mwanasiasa basi ningeakikisha fedha za uchaguzi mwaka huu zinatumika kuboresha huduma za maji na Mashule kwa wananchi wote na uchaguzi uairishwe mpaka miaka mitano inayokuja na kuundwa serikali ya mseto. Je wanasiasa wanawaza kama mimi au watu wengine wanaopenda nchi? Ni nini maana ya uchaguzi wakati nchi nzima inafahamu CCM itashinda? Je ni kiasi gani cha Gharama kitatumika kwenye uchaguzi? Je kiasi hicho hatuwezi kutumia kwa kazi nyingine muhimu kuboresha maisha ya wananchi?

    Mjusi

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 16, 2010

    watu wote tunakuunga mkono ila usisahau kulipa hela ya baku mara upatapo ubunge .... kila la kheri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...