Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Bi. Flora Nducha jijini New York, Marekani.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Bi. Flora Nducha (nguo nyekundu) akiwa na kikosi kazi chake kwenye studio za radio hiyo jijini New York
HISTORIA FUPI YA RADIO YA UMOJA WA MATAIFA
Radio ya Umoja wa Mastaifa ilianza tangu mwaka 1948 na ilianza kwa lugha ya kingereza pekee hadi mwanzoni mwa miaka ya 50 ambapo na Kifaransa kikaongezwa kwani lugha kuu mbili zinazotumiaka kwenye Umoja wa Mataifa ni Kiingereza na Kifaransa.
Ni hadi katikati ya miaka ya 50 ndipo lugha zingine rasmi zilianza kutangaza zikiwemo Kichina, Kihispania, Kirusi, na baadaye Kiarabu, Kiswahili na Kireno, ambazo zinarusha matangazo sehembu mbalimbali duniani kupitia Radio washirika. Pia kuna radio zinazotengeneza vipindi maalumu ni pamoja na Kihindi, Creole, Urdu na n.k

Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa ina washirika zaidi ya 20 katika nchi mbalimbali duniani wakiwepo TBC Tanzania, KBC Kenya, UBC Uganda, Channel Africa Afrika ya Kusini na Clouds FM Tanzania.
Wengine ni Contact FM Rwanda, Radio Rwanda, Radio Nationale du Burundi-RT NB, Radio Vatcan Roma, East Africa Radio On-line USA, Rema FM Burundi, Fadeco FM Tanzania, Voice of Nigeria, Frontier FM Kenya, Radio Maisha Tanzania, Sauti ya Zanzibar na nyingine ambazo zinaendelea kujiunga.
Pia idhaa hii ripota katika pembe ya Afrika inayounganisha pia Kenya, Somalia, Ethiopia na eritrea ambaye ni Jason Nyakundi. Katika Maziwa Makuu na DR Congo kuna Ramadhan Kibuga na Tanzania kwa sasa ni George Njogopa.
Washirika hawa wanaruhusiwa kurusha matangazo ya vipindi mbalimbali na kutumia material zote za Umoja wa Mataifa bila gharama yoyote. Pia matangazo hayo yanapatikana moja kwa moja:

1. Kwente wavuti: http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/
2. Kwenye facebook:http://www.facebook.com/UNRadioKis
3.Kwenye twitter:http://twitter.com/redioyaum

Kwenye facebook kila siku Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa inaweka mada mbalimbali ambazo msikilizaji huwa unaruhusiwa kuchangia mada na anaweza pia kuiandikia maoni au ushauri, mapendekezo na kukosoa pia.

Kwenye wavuti ya Radio hii pia unaweza kupata sauti na matukio mbalimbali, nakala za piacha, kuingia kwenye kituo chetu cha habari, kusikiliza matangazo yaliyopita, kupata taarifa mbalimbali za matukio ya Umoja wa Mataifa, kuingia kwenye idhaa ya mtandao ya Umoja wa Mataifa na kusikiliza taarifa za idhaa nyingine za Umoja wa Mataifa.

Pia mtu yeyote anaruhusiwa kuwa mwanachama wa idhaa hii kwa kujiunga kwenye facebook yake, twitter na wavuti. Aidha na waweza kuwasiliana na idhaa hii moja kwa moja kwa email nducha@un.org na kariukia@un.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. congratulations Flora, you deserve it, keep it up. you are really a fighter.

    ReplyDelete
  2. Hivi wako wapi Vicky Msina na Mshigeni Deograting?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...