
HISTORIA FUPI YA RADIO YA UMOJA WA MATAIFA
Radio ya Umoja wa Mastaifa ilianza tangu mwaka 1948 na ilianza kwa lugha ya kingereza pekee hadi mwanzoni mwa miaka ya 50 ambapo na Kifaransa kikaongezwa kwani lugha kuu mbili zinazotumiaka kwenye Umoja wa Mataifa ni Kiingereza na Kifaransa.
Ni hadi katikati ya miaka ya 50 ndipo lugha zingine rasmi zilianza kutangaza zikiwemo Kichina, Kihispania, Kirusi, na baadaye Kiarabu, Kiswahili na Kireno, ambazo zinarusha matangazo sehembu mbalimbali duniani kupitia Radio washirika. Pia kuna radio zinazotengeneza vipindi maalumu ni pamoja na Kihindi, Creole, Urdu na n.k
Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa ina washirika zaidi ya 20 katika nchi mbalimbali duniani wakiwepo TBC Tanzania, KBC Kenya, UBC Uganda, Channel Africa Afrika ya Kusini na Clouds FM Tanzania.
Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa ina washirika zaidi ya 20 katika nchi mbalimbali duniani wakiwepo TBC Tanzania, KBC Kenya, UBC Uganda, Channel Africa Afrika ya Kusini na Clouds FM Tanzania.
Wengine ni Contact FM Rwanda, Radio Rwanda, Radio Nationale du Burundi-RT NB, Radio Vatcan Roma, East Africa Radio On-line USA, Rema FM Burundi, Fadeco FM Tanzania, Voice of Nigeria, Frontier FM Kenya, Radio Maisha Tanzania, Sauti ya Zanzibar na nyingine ambazo zinaendelea kujiunga.
Pia idhaa hii ripota katika pembe ya Afrika inayounganisha pia Kenya, Somalia, Ethiopia na eritrea ambaye ni Jason Nyakundi. Katika Maziwa Makuu na DR Congo kuna Ramadhan Kibuga na Tanzania kwa sasa ni George Njogopa.
Washirika hawa wanaruhusiwa kurusha matangazo ya vipindi mbalimbali na kutumia material zote za Umoja wa Mataifa bila gharama yoyote. Pia matangazo hayo yanapatikana moja kwa moja:
1. Kwente wavuti: http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/
2. Kwenye facebook:http://www.facebook.com/UNRadioKis
3.Kwenye twitter:http://twitter.com/redioyaum
Kwenye facebook kila siku Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa inaweka mada mbalimbali ambazo msikilizaji huwa unaruhusiwa kuchangia mada na anaweza pia kuiandikia maoni au ushauri, mapendekezo na kukosoa pia.
Kwenye wavuti ya Radio hii pia unaweza kupata sauti na matukio mbalimbali, nakala za piacha, kuingia kwenye kituo chetu cha habari, kusikiliza matangazo yaliyopita, kupata taarifa mbalimbali za matukio ya Umoja wa Mataifa, kuingia kwenye idhaa ya mtandao ya Umoja wa Mataifa na kusikiliza taarifa za idhaa nyingine za Umoja wa Mataifa.
Pia mtu yeyote anaruhusiwa kuwa mwanachama wa idhaa hii kwa kujiunga kwenye facebook yake, twitter na wavuti. Aidha na waweza kuwasiliana na idhaa hii moja kwa moja kwa email nducha@un.org na kariukia@un.org
congratulations Flora, you deserve it, keep it up. you are really a fighter.
ReplyDeleteHivi wako wapi Vicky Msina na Mshigeni Deograting?
ReplyDelete