Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Fatma Mwassa ( kulia) akivishwa vazi na hatimaye urembo kutoka kwa mmoja wa wanawake wa Jamii ya Kimasai kutoka Kijiji cha Wami Sokoine, kabla ya kupokea Mwenge wa Uhuru Wilayani humo mwashoni mwa wiki , kama alivyokutwa kijiji hapo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2010, Dk Nassoro Ally Matuzya, ( kulia ), akiwasha gesi kuashiria kuzinduliwa rasmi maabara ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa masomo ya sayansi wa shule ya Sekondari Nassoro Seif iliyopo Mtibwa , Turiani , Wilayani Mvomero. kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Fatma Mwassa, hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki wakati wa mbio za mwenge wa uhuru. ( Picha zote na John Nditi) .
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mwashibanda Lucas Shibanda akiwa wamejitwishwa ndoo ya maji kichwani, mara baada ya kuzindiliwa mradi wa usambazaji maji Makao Makuu ya Wilaya ya Mvomero na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2010, Dk Nassoro Ally Matuzya, ( wa kwanza kushoto), mwanzoni mwa wiki, Wilayani humo wakati wa mbio za mwenge. Picha zote na John Nditi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. HABARI ZA KAZI BROTHER MICHUZI, NAOMBA NIULIZI SWALI BRO. HIVI HUU MWENGE WA UHURU, NINI FAIDA YAKE, MIMI NAFIKIRI UNAPOTEZA PESA ZA SEREKARI BURE. AU NINI KUSUDIO LA MWENGE HUU.

    ReplyDelete
  2. jamani mimi niko nje ya mada naomba mnijuze namna ya kupata habari ya siku za nyuma maana compyuta yangu ilikuwa na matatizo kidogo sasa sijuii namna kupata habari za nyuma pls

    ReplyDelete
  3. Kwa mazingira tunayoishi sasa mwenge hauna maana wala faida yoyote, kwa kweli ni kupoteza sio muda tu, bali fedha na rasilimali nyingi za walipa kodi, wakati umefika sasa serikali iachane na upuuzi huu.

    ReplyDelete
  4. Mbona wakimbiza mwenge wanavaa nguo za kimbowe mbowe? Nadhani wangelibadilisha kuondoa fikra za itikadi za vyama vya siasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...