Habari Kaka Michuzi,
Nimekuwa nikipoea mail na sms yenye ujumbe huo hapo chini, je ni kweli au basi wabongo tumezusha ilimradi siku iende?

"Hello, Inasemekana kuwa kuna mionzi inatumwa kwenye simu, kama simu ikiita haionyeshi namba au inawaka taa nyekundu au inaonyesha manamba mengi kama namba za nje usipokee.
Kuna mwalimu ameshakufa tayari kwa mionzi hiyo, Kuwa makini na waambie wengine."
mdau wa Globu ya Jamii
========


Salam wanalibeneke na watanzania wote nimepokea ujumbe huu na pia watu kibao wamepokea na wamedai kua ukipokea simu yoyote private ya rangi nyekundu ni mionzi ya hatari unakufa ama kupalalaizi je ni kweli na kuna mdau yeyote kasikia kua kuna mtu kafa maana nasikia uko Kenya tayari watu wamekufa kutokana na kupokea simu izo.

UJUMBE HUU APA

TAHADHARI
"Ukipigiwa simu kwa private number au ikaandika call kwa red color usipokee,ni mionzi hatar unaweza kuparalize. imetokea Kenya watu wameathiriwa vibaya na wengine wamekufa."


Naombeni msaada....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nashangaa hii serikali yetu inafanya nini hususan TCRA au mamlaka ya mawasiliano kuhusu mambo kama haya. Wanatakiwa wawe wa kwanza kutoa taarifa kamili kwa wananchi. Mbali ya kwamba hizo simu ni za nje, lakini hii mamlaka ya Mawasiliano imeshindwa kuhakikisha simu ambazo hazijasajiliwa hazipati huduma. Leo hii hata ukinunua line mpya leo bado unaweza kuitumia bila kusajili. Tuelewe kuwa wameshindwa kazi??? Kuna maprofesa kule sisi wananchi tunashindwa kuelewa mamalaka inafanya nini.

    ReplyDelete
  2. watu wengi wamepata hio habari na mpaka sasa hakuna habari kamili. Jamani wadau tusaidieni

    ReplyDelete
  3. hapana hio si kweli. kwa sababu mtu unapokuwa sametime ukipigia mtu ukiwa katika kiosk nambar unazotumia haziji kwenye simu ya mpokeaji.ao zinakuja nambar zaidi ya 20 kwa hivo uo ni uongo. na wakati mwengine watu wanachukuwa card wanaingiza kwenye simu zao wanapiga,na hapo haionyeshi nambari.kwa kweli sio ukweli.pokeeni simu zenu bila wasiwasi wa aina yeyote.satelite zinatumia ma billioni ya nambari nyingi sana kuandika kila nambar ya card haiwezikani.asanteni sana.

    ReplyDelete
  4. Mtaalam wa kompyutaSeptember 03, 2010

    This can not be done...usiwastue watu.

    ReplyDelete
  5. Duh kumbe ndio maana nampigia mama yangu bongo hapokei!!! sasa me nitawasiliana nae vipi jamani eee

    ReplyDelete
  6. Wewe mdau wa kwanza wacha ku-panick na kutuchekesha. Hizi porojo pia nimeshazisikia. Jamaa yangu kanipigia simu kutoka UK na nikaijibu. Simu haikuonyesha namba kwa sababu alikuwa anatumia kadi maalum pre-paid. Waafrika tunaamini vitu vya ajabu. Mimi naendelea kuwapa pesa waombaji wanaostahili kwenye traffic lights bila kuogopa kuota manywele mikononi. Aidha, nawashutumu washirikna wote wanaopanda mbegu za hofu katika jamii zetu. Get a life, soma sayansi na nenda mskitini au kanisani, sawa mkuu???

    ReplyDelete
  7. Hii inashangaza kidogo , kwa kuwa kama mtu kisha kufa atasemaje kuwa alikufa kutokana na mionzi hatari, labda kama kuna uchunguzi umefanyika na wataalam na hao ndio watakao toa taarifa za kifo/vifo hivyo, na sio taarifa za mitaani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...