"Hello, Inasemekana kuwa kuna mionzi inatumwa kwenye simu, kama simu ikiita haionyeshi namba au inawaka taa nyekundu au inaonyesha manamba mengi kama namba za nje usipokee.
Salam wanalibeneke na watanzania wote nimepokea ujumbe huu na pia watu kibao wamepokea na wamedai kua ukipokea simu yoyote private ya rangi nyekundu ni mionzi ya hatari unakufa ama kupalalaizi je ni kweli na kuna mdau yeyote kasikia kua kuna mtu kafa maana nasikia uko Kenya tayari watu wamekufa kutokana na kupokea simu izo.
UJUMBE HUU APA
TAHADHARI
"Ukipigiwa simu kwa private number au ikaandika call kwa red color usipokee,ni mionzi hatar unaweza kuparalize. imetokea Kenya watu wameathiriwa vibaya na wengine wamekufa."
Naombeni msaada....
Nashangaa hii serikali yetu inafanya nini hususan TCRA au mamlaka ya mawasiliano kuhusu mambo kama haya. Wanatakiwa wawe wa kwanza kutoa taarifa kamili kwa wananchi. Mbali ya kwamba hizo simu ni za nje, lakini hii mamlaka ya Mawasiliano imeshindwa kuhakikisha simu ambazo hazijasajiliwa hazipati huduma. Leo hii hata ukinunua line mpya leo bado unaweza kuitumia bila kusajili. Tuelewe kuwa wameshindwa kazi??? Kuna maprofesa kule sisi wananchi tunashindwa kuelewa mamalaka inafanya nini.
ReplyDeletewatu wengi wamepata hio habari na mpaka sasa hakuna habari kamili. Jamani wadau tusaidieni
ReplyDeletehapana hio si kweli. kwa sababu mtu unapokuwa sametime ukipigia mtu ukiwa katika kiosk nambar unazotumia haziji kwenye simu ya mpokeaji.ao zinakuja nambar zaidi ya 20 kwa hivo uo ni uongo. na wakati mwengine watu wanachukuwa card wanaingiza kwenye simu zao wanapiga,na hapo haionyeshi nambari.kwa kweli sio ukweli.pokeeni simu zenu bila wasiwasi wa aina yeyote.satelite zinatumia ma billioni ya nambari nyingi sana kuandika kila nambar ya card haiwezikani.asanteni sana.
ReplyDeleteThis can not be done...usiwastue watu.
ReplyDeleteDuh kumbe ndio maana nampigia mama yangu bongo hapokei!!! sasa me nitawasiliana nae vipi jamani eee
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza wacha ku-panick na kutuchekesha. Hizi porojo pia nimeshazisikia. Jamaa yangu kanipigia simu kutoka UK na nikaijibu. Simu haikuonyesha namba kwa sababu alikuwa anatumia kadi maalum pre-paid. Waafrika tunaamini vitu vya ajabu. Mimi naendelea kuwapa pesa waombaji wanaostahili kwenye traffic lights bila kuogopa kuota manywele mikononi. Aidha, nawashutumu washirikna wote wanaopanda mbegu za hofu katika jamii zetu. Get a life, soma sayansi na nenda mskitini au kanisani, sawa mkuu???
ReplyDeleteHii inashangaza kidogo , kwa kuwa kama mtu kisha kufa atasemaje kuwa alikufa kutokana na mionzi hatari, labda kama kuna uchunguzi umefanyika na wataalam na hao ndio watakao toa taarifa za kifo/vifo hivyo, na sio taarifa za mitaani.
ReplyDelete