kikosi cha Kilimanjaro Stars.Kikosi cha Harambee Stars.
Manahodha wakisabahiana huku marefalii wakiwacheki.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars,Mrisho Ngassa akichuana vikali na mlinda mlango wa tumu ya Harambee katika mtanage wa kirafiki uliomalizika jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru jijini dar.hadi mwisho wa mchezo timu Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa ushindi mnono wa bao moja uliopatikana kupitia mshambuliaji Gaudence Mwaikimba.
Gaudence Mwaikimba akijarubu kutaka kumtoka beki wa timu ya Harambee stars katika mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru.
Mwaikimba akipachika bao la pekee lililoipatia ushindi timu ya Kilimanjaro stars.
fea plei...... makocha wa timu zote mbili wakipongezana mara baada ya mechi kumalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ankal,
    Ingenoga kama angalau ungeambatanisha majina ya wachezaji wa Tanganyika Stars ktk picha.

    ReplyDelete
  2. Michuzi acha uongo , anayepiga kichwa siyo Mwaikimba na kama uko makini Mwaikimba alivaa jezi namba 20 siyo 19. rekebisha hiyo.
    Mimi.

    ReplyDelete
  3. Halafu huyu kocha simuelewi kabisa, mbona forward mmoja tu kwenye timu (Mwaikimba). Duh sijui kama kweli anataka kushambulia ama anatafuta sare kila mechi maana hapo hata kupata goli inakuwa kama bahati.

    ReplyDelete
  4. Hongereni kwa ushindi. Kiwango cha Timu hakiridhishi kbs. nina mashaka sana na matokeo wakati wa Tusker ikianza. kiwango sio kizuri kabisa. Mwaikimba punguza maneno. mpira ni miguuni. acha miguu/kiwango chako kiongee sio kila saa uko na waandishi wa habari unajifanya unatoa comments tu! mdomo unakuponza. Na nyinyi waandishi wa habari punguzeni kumpamba mtu sana. Eti mwaikimba nyota wa mchezo! mnachekesha!

    ReplyDelete
  5. Tanganyika stars??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...