Klabu ya mazoezi ya viungo ya Obama Jana ilifanya zoezi la upandaji miti katika eneo lililokuwa likichimbwa mchanga katika kijiji cha Chechele kilichopo Donge, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Upandaji miti huo ni moja kati ya shughuli za kijamii ambazo Klabu hiyo hujihusisha nazo, shughuli nyengine inazojishughulisha nazo ni pamoja usafishaji wa mazingira katika sehemu mbali mbali zikiwemo Hospitali za Unguja na Pemba,
Zoezi hili la leo la upandaji miti lilifanyika katika eneo lililohamwa kwa uchimbaji mchanga, iumekuwa ni utaratibu wa serekali kuhifadhi mazingira ya maeneo yaliyoachwa kuchimbwa mchanga kwa kuotesha miti ili kuhifadhi uharibifu zaidi wa mazingira.
Klabu ya mazoezi ya viungo ya Obama imeendesha zoezi hili kwa nia ya kuionesha jamii na serekali kwa ujumla kwamba mbali ya shughuli za mazoezi pia inajishughulisha na mambo ya kijamii kwani wafanya mazoezi ni miongoni mwa jamii.
Wito unatolewa kwa vilabu vyengine vya mchezo huo kujitokeza katika shuguli za utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya Taifa letu.
TUYATUNZE MAZINGIRA ILI NAYO YATUTUNZE
Mimi nawapongeza sana kwa hizo juhudi zenu, isipokuwa hilo jina mhhhhhh!
ReplyDeleteHivyo hakuna jina la kiongozi wa Afrika ambaye mungeweza kutumia jina lake?
mashaalah, hongereni sana Obama, munaonyesha kwa mfano. Uongozi wa shehia usimamie kuilinda miti iliyopandwa
ReplyDeleteMdau
K