Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai  (wa pili kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya,  Mh. Kenneth Marende,  walipokutana katika Bunge la Uingereza jana. Waheshimiwa Wabunge wako nchini Uingereza kufuatilia malipo ya zaidi ya paundi milioni 29 kutoka BAE System baada ya Mahakama nchini hapa kuiamuru kampuni hiyo kuilipa Tanzania baada ya kugumdulika kwamba kampuni hiyo iliongeza bei ya ununuzi wa Radar.
Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu  (kulia) akiongea na Naibu Spika wa Bunge la uingereza, Mhe. Nigel Evans (Mb).katikati ni Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, anayeongoza ujumbe huo.
Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe  (kulia) akiteta jambo na Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania ambao ni toka kushoto  Mh. Job Ndugai (Naibu Spika), Mussa Azzan Zungu (Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mhe.  Angela Kairuki. Picha na mdau Assah Mwambene

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona Mh. Cheyo hajatajwa kwenye orodha au amezamia?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2011

    zamani bwana walikuwa wanasemaga wapili kushoto wa kwanza au alievaa suti ya mtumba n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...