Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya, Mh. Kenneth Marende, walipokutana katika Bunge la Uingereza jana. Waheshimiwa Wabunge wako nchini Uingereza kufuatilia malipo ya zaidi ya paundi milioni 29 kutoka BAE System baada ya Mahakama nchini hapa kuiamuru kampuni hiyo kuilipa Tanzania baada ya kugumdulika kwamba kampuni hiyo iliongeza bei ya ununuzi wa Radar.
Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) akiongea na Naibu Spika wa Bunge la uingereza, Mhe. Nigel Evans (Mb).katikati ni Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, anayeongoza ujumbe huo.
Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kulia) akiteta jambo na Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania ambao ni toka kushoto Mh. Job Ndugai (Naibu Spika), Mussa Azzan Zungu (Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mhe. Angela Kairuki. Picha na mdau Assah Mwambene
Mbona Mh. Cheyo hajatajwa kwenye orodha au amezamia?
ReplyDeletezamani bwana walikuwa wanasemaga wapili kushoto wa kwanza au alievaa suti ya mtumba n.k
ReplyDelete