Salaam.
Kwenye post ya Mkuu wa mkoa wa Tabora kuzindua tamasha la Mtemi Mirambo (http://issamichuzi.blogspot.com/2011/07/mkuu-wa-mkoa-wa-tabora-azindua-tamasha.html) kuna picha ikimuonyesha mkuu huyo na maelezo yanasema "Mkuu wa mkoa Mhe Abeid Mwinyimsa akirusha mshale juu kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha hili"
Swali langu ninalopenda wadau wanielimishe ni kuwa
Je!! Mshare HURUSHWA, HUFYATULIWA, HUPIGWA ama?
Baraka kwako

Mzee wa Changamoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Ninavyojua mimi msemo sahihi ni "kupiga mshale". Neno "kupiga" linatumika sana katika Kiswahili na lugha nyingine nyingi za Kibantu, hasa kusini mwa Afrika, kubeba maneno ya matendo. Kwa mfano, kupiga mswaki, kupiga bei, kupiga porojo, kupiga chenga, kupiga kelele n.k. Nawasilisha. J. Ngowi. Arusha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2011

    Mshale hufyatuliwa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2011

    "Kupiga mshale" ndo sahihi...maana unapotumia neno "kupiga" huwa ni neno linaloashiria kuwa lazima kuwe na "madhara yaani 'effect'" ndo maana tunatumia katika vitu vingi mfano; kupiga risasi, kupiga shabaha,n.k. Ila maneno kama kurusha..hayana madhara (effect) au kufyatua....waweza kufyatua mtego, ila usiwe kwenye dhamira kamili,Ukimaanisha kuwa unafyatua tu kitu kilichotegwa(pengine carelessly) ili kupunguza madhara.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2011

    neno sahihi ni kurusha mshale (siyo mshare hiyo ni aina ya ndizi uliza wachaga)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2011

    mshale hulipuliwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...