Salaam.
Kwenye post ya Mkuu wa mkoa wa Tabora kuzindua tamasha la Mtemi Mirambo (http://issamichuzi.blogspot.com/2011/07/mkuu-wa-mkoa-wa-tabora-azindua-tamasha.html) kuna picha ikimuonyesha mkuu huyo na maelezo yanasema "Mkuu wa mkoa Mhe Abeid Mwinyimsa akirusha mshale juu kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha hili"
Swali langu ninalopenda wadau wanielimishe ni kuwa
Je!! Mshare HURUSHWA, HUFYATULIWA, HUPIGWA ama?
Baraka kwako
Mzee wa Changamoto
Ninavyojua mimi msemo sahihi ni "kupiga mshale". Neno "kupiga" linatumika sana katika Kiswahili na lugha nyingine nyingi za Kibantu, hasa kusini mwa Afrika, kubeba maneno ya matendo. Kwa mfano, kupiga mswaki, kupiga bei, kupiga porojo, kupiga chenga, kupiga kelele n.k. Nawasilisha. J. Ngowi. Arusha.
ReplyDeleteMshale hufyatuliwa!
ReplyDelete"Kupiga mshale" ndo sahihi...maana unapotumia neno "kupiga" huwa ni neno linaloashiria kuwa lazima kuwe na "madhara yaani 'effect'" ndo maana tunatumia katika vitu vingi mfano; kupiga risasi, kupiga shabaha,n.k. Ila maneno kama kurusha..hayana madhara (effect) au kufyatua....waweza kufyatua mtego, ila usiwe kwenye dhamira kamili,Ukimaanisha kuwa unafyatua tu kitu kilichotegwa(pengine carelessly) ili kupunguza madhara.
ReplyDeleteneno sahihi ni kurusha mshale (siyo mshare hiyo ni aina ya ndizi uliza wachaga)
ReplyDeletemshale hulipuliwa
ReplyDelete