Ankal, wape hii
Ni kuwajuza tuu kuwa Tanzania, Sauzi na Zambia zinatumia biti la nyimbo ya taifa linalofanana sana. Hii ni kwa sababu kihistoria nchi zote zilipata biti hilo kutoka kwa mtunzi mmoja, anayeitwa Enoch Sontonga, mwenye asili ya Sauzi. Enoch, ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa mwalimu wa kwaya na hapo mwanzo biti hilo lilikuwa likipigwa kanisani huko Sauzi.
Ila kumbuka maneno ya nyimbo hizo za taifa, yanatofautiana sana. Ili kuelewa kufanana kwa mdundo wa nyimbo hizo embu bofya hapa:
Wimbo wa taifa wa Zambia:
Wimbo wa taifa wa Sauzi:

Kwa mujibu wa libeneke la wikipedia, nchi za Zimbabwe na Namibia ziliwahi pia kutumia biti hilo kwa muda mrefu.

Mdau John.
Sauzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ninalifahamu hili kwa muda mrefu kuna wakati nilikuwa natamani hata tubadili wimbo wetu ili tuwe Unique. Ni bora Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Au hata Tazama Ramani.

    ReplyDelete
  2. Wimbo wetu wa Taifa ni wa kuiga kutoka south africa wimbo "Nkosi Sikelei iAfrika" (God Bless Africa) wa mwaka 1912. Ni kweli mtunzi ni Enoch Sontonga,alipoutunga ulikua ni wimbo wa kawaida kitaani South Africa, then ANC wakautumia kwenye mikutano yao. Mchonga(Nyerere) akaupenda kisa umekaa ki-ukombozi zaidi na kuufanya wa taifa letu. Mwenye nao (SA) walipopata uhuru 1994 nao akaufanya kuwa wimbo wao wa Taifa. Kwa kifupi haukupaswa kuwa wimbo wetu wa Taifa tuliukwapua kutoka kwa ANC.

    ReplyDelete
  3. Mkuu Michuzi, tutafutie Mzee Kitime awe anatoa somo la muziki angalau mara moja kwa wiki. Mdau anaongelea biti kama watoto wa mtaani wanavyotumia lakini nadhani hapa anamaanisha melody (sauti) na siyo rhythm aka biti. Ana tabu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...