Ankal, wape hii
Ni kuwajuza tuu kuwa Tanzania, Sauzi na Zambia zinatumia biti la nyimbo ya taifa linalofanana sana. Hii ni kwa sababu kihistoria nchi zote zilipata biti hilo kutoka kwa mtunzi mmoja, anayeitwa Enoch Sontonga, mwenye asili ya Sauzi. Enoch, ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa mwalimu wa kwaya na hapo mwanzo biti hilo lilikuwa likipigwa kanisani huko Sauzi.
Ila kumbuka maneno ya nyimbo hizo za taifa, yanatofautiana sana. Ili kuelewa kufanana kwa mdundo wa nyimbo hizo embu bofya hapa:
Wimbo wa taifa wa Zambia:
Wimbo wa taifa wa Sauzi:
Kwa mujibu wa libeneke la wikipedia, nchi za Zimbabwe na Namibia ziliwahi pia kutumia biti hilo kwa muda mrefu.
Mdau John.
Sauzi


Ninalifahamu hili kwa muda mrefu kuna wakati nilikuwa natamani hata tubadili wimbo wetu ili tuwe Unique. Ni bora Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Au hata Tazama Ramani.
ReplyDeleteWimbo wetu wa Taifa ni wa kuiga kutoka south africa wimbo "Nkosi Sikelei iAfrika" (God Bless Africa) wa mwaka 1912. Ni kweli mtunzi ni Enoch Sontonga,alipoutunga ulikua ni wimbo wa kawaida kitaani South Africa, then ANC wakautumia kwenye mikutano yao. Mchonga(Nyerere) akaupenda kisa umekaa ki-ukombozi zaidi na kuufanya wa taifa letu. Mwenye nao (SA) walipopata uhuru 1994 nao akaufanya kuwa wimbo wao wa Taifa. Kwa kifupi haukupaswa kuwa wimbo wetu wa Taifa tuliukwapua kutoka kwa ANC.
ReplyDeleteMkuu Michuzi, tutafutie Mzee Kitime awe anatoa somo la muziki angalau mara moja kwa wiki. Mdau anaongelea biti kama watoto wa mtaani wanavyotumia lakini nadhani hapa anamaanisha melody (sauti) na siyo rhythm aka biti. Ana tabu!!
ReplyDelete