Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji mke wa Marehemu Mweshimiwa Jeremia Sumari, Bi. Miriam Sumari kabla ya mazishi ya marehumu sumari kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Spika mtaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa
Duh hii kweli kali nimekosa maneno ya kuandika.
ReplyDeleteApumzike kwa Amani....Amina!
ReplyDeleteanony Mon Jan 23, 06:26:00 PM 2012 bora we umekosa cha kuandika manake mie nimeona nikae kimya tu.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteAnony wa Mon Jan 23, 09: 38: 00PM 2012 na wewe umeona enh? Bora kupotezea manake picha imemaliza kila kitu.
ReplyDeleteAlafu nilijua nikisema haitawekwa kama ambavyo ya mdau hapo juu wameitoa, wameitoa kwasababu atakuwa amesema kwa sauti kile wengine tunachoshindwa na kuishia kuacha picha iongee.
ReplyDeleteanony Tue Jan 24, 02:13:00 AM 2012, mie naona kuanzia sasa habari kama hizi tuziache zipite tu manake, we acha tu.
ReplyDeleteJamani viongozi wetu hawana wawakilishi wa kuhudhuria mazishi ili wao waendelee na kuongoza nchi? Mbezi ilikuwa inatosha, wamewapa pole wafiwa, haikuwa lazima waende na Arusha.
ReplyDeleteNi masikitiko kuondekewa na mbunge, lakini maisha yanasonga mbele tuendelee kujenga nchi yetu. Inabidi viongozi wetu waonyeshe mfano.