Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha leo
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha leo
 Spika  wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji mke wa Marehemu Mweshimiwa Jeremia Sumari, Bi. Miriam Sumari kabla ya mazishi ya marehumu sumari kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha 
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha 
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Spika mtaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Duh hii kweli kali nimekosa maneno ya kuandika.

    ReplyDelete
  2. anony Mon Jan 23, 06:26:00 PM 2012 bora we umekosa cha kuandika manake mie nimeona nikae kimya tu.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. Anony wa Mon Jan 23, 09: 38: 00PM 2012 na wewe umeona enh? Bora kupotezea manake picha imemaliza kila kitu.

    ReplyDelete
  5. Alafu nilijua nikisema haitawekwa kama ambavyo ya mdau hapo juu wameitoa, wameitoa kwasababu atakuwa amesema kwa sauti kile wengine tunachoshindwa na kuishia kuacha picha iongee.

    ReplyDelete
  6. anony Tue Jan 24, 02:13:00 AM 2012, mie naona kuanzia sasa habari kama hizi tuziache zipite tu manake, we acha tu.

    ReplyDelete
  7. Jamani viongozi wetu hawana wawakilishi wa kuhudhuria mazishi ili wao waendelee na kuongoza nchi? Mbezi ilikuwa inatosha, wamewapa pole wafiwa, haikuwa lazima waende na Arusha.

    Ni masikitiko kuondekewa na mbunge, lakini maisha yanasonga mbele tuendelee kujenga nchi yetu. Inabidi viongozi wetu waonyeshe mfano.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...