Mchezaji wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima akichuana na beki wa timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, Mpira umekwisha na Yanga imefanikiwa kuitandika Mtibwa Sugar Magoli 3-0 
Refarii wa mchezo huo akinyoosha mkono wake juu kuashiria timu ya Yanga ipige mpira wa adhabu kuelekea lango la timu ya Mtibwa Sugar.
Mmoja wa Mashabiki wa timu ya Yanga akiwa amejipaka masizi usoni mwake ikiwa ni moja ya staili ya ushangiliaji kwa timu yake. 
Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mhhhhh, Ankal, ukiona meusi tu basi ni masizi?! Ni rangi spesho hiyo, toa ushamba wa mwaka 47 hapa, chama kubwa hilo!

    ReplyDelete
  2. Wabongo bwana! Anapanda juu ya hilo chuma akiling'oa atasema serikali hatunzi uwanja kwani angeshangilia kawaida bila kutaka kuleta uharibifu ingekuwaje?

    ReplyDelete
  3. Washangilie hivihivi siku watakapocheza na Zamalek.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza Anonymous wa Thu Feb 09, 03:08:00 AM 2012

    Mhhhhh, Ankal, ukiona meusi tu basi ni masizi?!

    Hujamsoma ,tatizo Ankal ni Bwawa la Maini,,,sasa kwa itikadi watu wenye msimamo huo wana kale kamnyama mnyama hivi.......

    ReplyDelete
  5. Hakuna cha rangi spesho wala nini, hayo ni masizi ya mkaa. Hiyo ndio rangi spesho ya mashabiki wa Yanga kama hawa.

    ReplyDelete
  6. Wewe Mdau wa tatu hapo juu:

    ''Washangilie hivi hivi watakapocheza na Zamalek''

    Wewee Yanga Bomba bana,,,Mwarabu ataelekezwa Kibla na atakula KISU!

    ELEWA:

    1.Mchinjaji mara zote aonapo Mnyama hupata uchu!,,,na kusogeza kisu karibu!

    2.Mara zote Mchinjaji huchagua 'mnyama' aliyenona!

    3.MARA ZOTE (IKIWEPO ZAMALEK) NI KAWAIDA KWA 'WANYAMA' KUCHINJWA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...