Balozi Mteule wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi akiwasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala za hati za utambulisho ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.
mbona wazungu wana washilisha Ikulu kwamwenye nchi mwenyewe?
ReplyDeletemdau paris
Tafadhali soma vizuri. Hizo ni "nakala"; huwa zinawasilishwa Wizara ya Mambo ya Nje. Originals huwa zinawasilishwa kwa Rais, Ikulu.
ReplyDeleteHakuna cha wazungu hapa, bali ni taratibu zinafuatwa.
bila kuwakumbatia wazungu hatujafurahi ,tupendane afrika kila balozi walitakiwa wawakilishe kwa huyo waziri lakini !!!!!!
ReplyDeleteMdau Paris wacha ujinga! Kumbe kukaa huko hakujakusaidia: protocali ni kwamba kwanza unawakilisha nakala Wizara ya Mambo ya Nje na kisha hatua ya pili ndo anawasilisha hati original kwa Mkuu wa nchi!
ReplyDeleteMh. Michuzi,
ReplyDeleteAsante sana blog yako inatupa sana elimu nyingi.
Vijana wetu wajuvaji (wajuvi) lakini hawajui chochote, waambie kushabikia siasa ambayo vilevile hawaijui
ReplyDeletewatalaam wa foreign affairs naona mmewakilisha vizuri kwa majibu
ReplyDelete