Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akilia kwa furaha huku akibembelezwa na Mbunge wa Viti Maalum Kataru Mkoa wa Manyara, Rose Kamili (anayeangaalia kamera), baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali pingamizi la kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge Lissu.
Lissu akifutwa machozi na mkewe wakati wakitoka nje ya mahakama mjini Singida
Napongeza mahakama kuu kwakutoa haki, ukiona mtu mzima analia ujue yamemfika mengi.
ReplyDeleteMheshimiwa Tindu, mchango wako katika taifa hili ni muhimu tunakutakia kila la heri.
Alaaa!! Kwa Mbunge wa CHADEMA kushinda kesi ya uchaguzi mahakamani ni haki; lakini akishindwa uamuzi ulipangwa, he!!
ReplyDeletePia sikujua kama kumbe Tundu Lisu ni 'pofu' kiasi hicho, sasa hapo kuna jambo gani la kumliza?
Mwanaume hulii hadharani kwa kupata ubunge, ungejificha basi ukaliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, ukanyamaza na kukakiwa na kwikwi.
ReplyDeleteUbunge mtamu jama...hasa hasa zile posho na sitting allowance...mwachen baba wa watu alie machozi maana angepigwa chini familia ingeteseka!!
ReplyDeletePole sana kiongozi, tunajua ulikuwa unawekewa zengwe tu. Tupo pamoja.
ReplyDeleteHongera Tundu Lisu ninyi mnaongozwa na Mungu naye atawatetea daima. Hongera kwa mahakama kuonyesha kwamba you are impartial on this
ReplyDeleteMahakama kuu;Kesi ya Lema jimbo la Arusha tulisema kuna 'mkono wa mtu'..na hii je??Hongera bwana Lisu ndiyo siasa hiyo.Tupo pamoja
ReplyDeleteDavid V
Ubunge ni utajiri! Umeshatumia kama millioni 450 kuhonga nani anajua labda umekopa, usilie mchezo...wadanganyika mpo!
ReplyDeleteChozi la mwenye Haki, haliendi bure. Whatch out politician!
ReplyDeleteSo angeshindwa kesi manake mahakama haitoi haki?? Lema nae Arusha kwahiyo kaonewa??
ReplyDeleteHata Mkuu wetu aliposhinda urais alilia.
ReplyDeleteUnapokandamizwa hali uijua haki ni yako na Mungu akakutetea lazima ulie.
Mwanamume analia wala hakuna cha ajabu.
Lema alionewa.
Lakini Mungu akisema ndio hakuna wa kupinga
Kwa tamaduni zetu dume halilii. Haya ni mambo ya kuiga!!
ReplyDeleteWewe unaesema dume halilii hayajakufika ngoja afe mkeo ndo utajua.
ReplyDeleteAhhh ni hatari sana na aibu kubwa Umma ukishuhudia Mwanaume analia Mchana kweupeee!
ReplyDeleteLakini sio mchezo, joto ya jiwe ameiona,kamasi zimemtoka, almanusura akawe Dalali wa kuuza ngo'mbe Mnadani Kintinku-Singida kama yangemkuta kama ya Godbless Lema!
Ni kama ndege aliyepigwa jiwe la Manati akapunyuliwa manyoya ya mkia lakini akanusurika kifo!.
Hahahaha !!!
ReplyDeleteKwani hawawasiliani na mwenzie Godbless Lema?,,,wanapigiana simu mara kwa mara Lissu akimpa maendeleo na mchakato wa Kesi, ila habari inayomfanya alie ni kuwa mwenzie Lema ameshakwama kurudi Bungeni, alimweka wazi kuwa yeye Lema yupo amerudi Gereji ya magari anapiga spana kitambi chake cha Bungeni kimeporomoka ghafla, pia ameota 'vigimbi' vya mikono kama mfyatua matofali na mikono imekwishaota sugu !