Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akilia kwa furaha huku akibembelezwa na Mbunge wa Viti Maalum Kataru Mkoa wa Manyara, Rose Kamili (anayeangaalia kamera), baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali pingamizi la kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge Lissu.
                  Lissu akifutwa machozi na mkewe wakati wakitoka nje ya mahakama mjini Singida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Napongeza mahakama kuu kwakutoa haki, ukiona mtu mzima analia ujue yamemfika mengi.

    Mheshimiwa Tindu, mchango wako katika taifa hili ni muhimu tunakutakia kila la heri.

    ReplyDelete
  2. Alaaa!! Kwa Mbunge wa CHADEMA kushinda kesi ya uchaguzi mahakamani ni haki; lakini akishindwa uamuzi ulipangwa, he!!
    Pia sikujua kama kumbe Tundu Lisu ni 'pofu' kiasi hicho, sasa hapo kuna jambo gani la kumliza?

    ReplyDelete
  3. Mwanaume hulii hadharani kwa kupata ubunge, ungejificha basi ukaliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, ukanyamaza na kukakiwa na kwikwi.

    ReplyDelete
  4. Ubunge mtamu jama...hasa hasa zile posho na sitting allowance...mwachen baba wa watu alie machozi maana angepigwa chini familia ingeteseka!!

    ReplyDelete
  5. Pole sana kiongozi, tunajua ulikuwa unawekewa zengwe tu. Tupo pamoja.

    ReplyDelete
  6. Hongera Tundu Lisu ninyi mnaongozwa na Mungu naye atawatetea daima. Hongera kwa mahakama kuonyesha kwamba you are impartial on this

    ReplyDelete
  7. Mahakama kuu;Kesi ya Lema jimbo la Arusha tulisema kuna 'mkono wa mtu'..na hii je??Hongera bwana Lisu ndiyo siasa hiyo.Tupo pamoja

    David V

    ReplyDelete
  8. Ubunge ni utajiri! Umeshatumia kama millioni 450 kuhonga nani anajua labda umekopa, usilie mchezo...wadanganyika mpo!

    ReplyDelete
  9. Chozi la mwenye Haki, haliendi bure. Whatch out politician!

    ReplyDelete
  10. So angeshindwa kesi manake mahakama haitoi haki?? Lema nae Arusha kwahiyo kaonewa??

    ReplyDelete
  11. Hata Mkuu wetu aliposhinda urais alilia.

    Unapokandamizwa hali uijua haki ni yako na Mungu akakutetea lazima ulie.

    Mwanamume analia wala hakuna cha ajabu.

    Lema alionewa.

    Lakini Mungu akisema ndio hakuna wa kupinga

    ReplyDelete
  12. Kwa tamaduni zetu dume halilii. Haya ni mambo ya kuiga!!

    ReplyDelete
  13. Wewe unaesema dume halilii hayajakufika ngoja afe mkeo ndo utajua.

    ReplyDelete
  14. Ahhh ni hatari sana na aibu kubwa Umma ukishuhudia Mwanaume analia Mchana kweupeee!

    Lakini sio mchezo, joto ya jiwe ameiona,kamasi zimemtoka, almanusura akawe Dalali wa kuuza ngo'mbe Mnadani Kintinku-Singida kama yangemkuta kama ya Godbless Lema!

    Ni kama ndege aliyepigwa jiwe la Manati akapunyuliwa manyoya ya mkia lakini akanusurika kifo!.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2012

    Hahahaha !!!

    Kwani hawawasiliani na mwenzie Godbless Lema?,,,wanapigiana simu mara kwa mara Lissu akimpa maendeleo na mchakato wa Kesi, ila habari inayomfanya alie ni kuwa mwenzie Lema ameshakwama kurudi Bungeni, alimweka wazi kuwa yeye Lema yupo amerudi Gereji ya magari anapiga spana kitambi chake cha Bungeni kimeporomoka ghafla, pia ameota 'vigimbi' vya mikono kama mfyatua matofali na mikono imekwishaota sugu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...