Basi yenye namba za usajili T 140 BGS Linalofanya safari yake kati ya Dar na Maundo Tandahimba likiwa limepinduka kufuatia kuchomoka kwa matairi ya mbele na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sinza -Miteja wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi barabara kuu ya Dar -Mtwara. Picha na na habari na Abdulaziz Video Lindi
Home
Unlabelled
ajali yaua mmoja, 10 wajeruhiwa lindi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Changamoto kwa waziri husika
ReplyDeleteAina hii ajali inadhihirisha asilimia 100 kuwa tatizo ni ubovu wa basi lenyewe. Basi lililotengemaa haliwezi kuchomoka matairi kwa style hii!!!
ReplyDeleteSaid Mwema aachie ngazi. Tezama basi hili tyres zilivyo vipara! Chini kumechakaa si kawaida. Police barabarani kazi kula mlungula tuuuuu! Hawajali usalama wa abiria wala wa raia kwa namna yeyote!! Tuko pabaya na Tunakwenda pabaya zaidi.
ReplyDeleteHili basi au scraper?
ReplyDeleteKama siyo mhandisi huwezi kukisia kwa karibu sababu ya hii ajali. Madereva acheni nyodo, jeuri na upuuzi. Jamii na matrafiq mnawaendekeza mno. Madereva wa Tanzania bara ni kaidi kuliko kokote nilikofika duniani, hata Reykjavik.
ReplyDeletemagari yanayoenda kusini hususan tandahimba,yamezidi kuwa mabovu,nnao mfano umenikuta mwenyewe,bus tumetoka nalo tadahimba mchuzi juu(.tanki la mafuta limetoboka,wameweka mafuta kwenye madumu )na tunapita kwenye vituo vya polisi,hawajali usalama wa raia,tunaiomba serikali ichunguze magari yanayoenda kusini,kwakweli ni mabovu tena sana,tusisubili kuona yaLIYIWAKUTA MV SKAGET ndo tuanze kutuma tume ya uchunguzi,magari yachunguzwe,ZUIA AJALI,EPUKA RUSHWA
ReplyDeleteMabasi siyo mabovu tu bali ni mikweche na kwa staili hii wengi wataumia na kufa.
ReplyDeleteAskari wa Usalama barabarani wafanye uhakiki wa kila basi kama ni mkweche basi liyeyushwe na kuwa chuma chakavu.
Wewe uliyepanda basi ambalo ni michuzi tupu na mkawapita polisi bila kusema na wewe hufai. Ulitaka nani akusemee. Ungewaeleza hao polisi mliowakuta njiani na kama wangepuuza ungekuwa umetimiza wajibu wa kuokoa maisha ya watu. Lakini ulikula jiwe kwa kuwa ulikuwa na shida. Usimlaumu mtu na wewe jilaumu kwani gari lingeanguka ukafa haya uliyoandika tusingeyajua wala kuyasikia.
ReplyDelete